Pre GE2025 Wahandisi na Wakandarasi wamnunulia Rais Samia helkopta kwaajili ya Kampeni za Urais 2025 pamoja na mafuta ya Tsh. 100,000,000/-

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Acha stori za kufikirika zisizo na msingi
 
Unajichekesha na nini hapa, wakati mambo mnayowafanyia waTanzania ni ya kishenzi. Wakitokea watu wa kuwateka vikaragosi kama nyinyi nisinge jihangaisha kabisa, kwa sababu nyinyi sasa ndio maadui wakubwa wa nchi hii.
Kama mambo gani?
 
Hiyo sio Rushwa kweli?🤔
Mkuu hamna hela yoyote imetolewa, hilo ni tukio la hadaa ili kuonyesha rais anakubalika sana. Na kama ni kweli wametoa hiyo hela ujue kumefanyika vitisho vya kutosha ili wakandarasi watoe hiyo hela, kwa matarajio kuwa watapewa upendeleo wa tender huko mbeleni.
 
Usidanganyike. Hao hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Wanatumiwa tu kama njia ya kupitishia pesa toka kwa wafadhili; kama waarabu kuziingiza hapa kutununulia serikali mwakani.
Uko sahihi kabisa, hilo ni jambo la kupanga ili kutakatisha pesa chafu za kuuza nchi. Na lengo la hilo igizo ni ili kuhadaa umma kuwa rais anakubalika na makundi yote. Ni so outdated strategies.
 
umma kuwa rais anakubalika na makundi yote. Ni so outdated strategies.
Kwa bahati mbaya sana ni wewe na mimi, na wachache wetu watakaloliona igizo la namna hii na kutambua lengo lake mahsusi. Matukio ya namna hii yanawazoa watu wengi sana akili katika jamii yetu hii. Na hawa watu wanatambua hivyo ndiyo maana matukio ya aina hii yatakuwepo mengi sana kuelekea 2025.

Kuyadhibiti haya ni kwa vyama vya upinzani kama CHADEMA kuyazungumzia waziwazi kwenye mikutano yao na wananchi ili waweze kuutambua uhuni huu kama ulivyo.
 
"sehemu ya kurudisha fadhila kwa Rais Dkt. Samia"
hawa ndio wanaotajirika na miradi mikubwa nchini ya mabilioni kutokana na ulaji na upigaji - ndipo kurudisha fadhila
 
Wangekua walimu wamefanya hivyo Uzi mzima ungejaa matusi...
 
Your browser is not able to display this video.

Kuna kundi au chama au muungano wa wajenzi wameingia siasa ghafla bin vuu. Hili kundi sijui ni chama gani cha wajenzi, wabunifu majenzi au mainjinia kiko nyuma yao.

Wadau hebu tushirikiane, ni nani hawa waliochangia chopa ya mama pamoja na mafuta kwa Tsh. Milioni 100?
 
Kila taasis wanajikomba kwa rais, kutukuza kujikomba and anything else you name it

Kuna shida kwenye jamii ya kitanzania, kuanzia ngazi ya familia, tuna produce kizaz cha ajab kweli
 
mtu mmoja mwenye akili timamu anifafanulie wajenzi huru lina maana gani!

wako huru kufanya maamzi kadri ya utashi wao, alimradi wako sambba na maelekezo ya sheria.
 
Hawajachanga hata mia. Wamepewa hela na mhusika wakanunue halafu ionekane wamemzawadia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…