Wahanga wa Moto wa soko la Karume wachangiwe pesa, ikiwa ni janga la bahati mbaya

Wahanga wa Moto wa soko la Karume wachangiwe pesa, ikiwa ni janga la bahati mbaya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Wakuu Kwema!

Ajira Hakuna!
Tumetoka familia Masikini Sana.

Nina rafiki zangu wengi waliokuwa wanauza uza mitumba Yao pale Karume.

Mitaji Yao wameipata Kwa mbinde Jamani! Ndugu zangu wote tunajuana humu nchini, Sisi ni masikini Sana, tunatafuta pesa Kwa taabu na nguvu nyingi, hatuwezi sema ni Mateso lakini hatutakataa mtu akisema tunataabika Mno.

Suala hili tusilipeleke Kisiasa, suala hili linagusa maisha ya watu moja Kwa moja, tena waganga njaa. Tunaowajibu WA kufanya Jambo Kama taifa lenye umoja.

Janga la Moto ni Kama majanga mengine Kama vile Mafuriko na tetemeko.

Tusiishie kuwapa pole tuu hao Machinga wa hapo Karume, ikiwezekana tuwachangie.

Vyombo vya habari ingefaa mpaka sasa wawe wameshaandaa Program za kuwasaidia HAO ndugu zetu.
Viongozi wa serikali nao halikadhalika, Viongozi wa Dini.

Wasanii na watu wote mashuhuri mpaka sasa wangepaswa wawe wameshajua chakufanya, lakini inashangaza kuona ukimya WA kutisha zaidi ya pole isiyo na msaada.

Kama tulivyowachangia walihanga wa tetemeko Bukoba kwani majanga makubwa Kama haya ya Moto tusichange?

Sitaki kuingilia masuala ya uchunguzi kuhusu chanzo cha Moto huo lakini itasikitisha endapo hakuna hatua zozote zitakazo chukuliwa kujua chanzo hiko.

Maisha ya hapa Duniani niya muda mfupi Sana, tuache kuumizana hata Kama wapo wanaoonekana wanastahili kuumizwa kutokana na ujinga wao, unyonge wao, upole wao, umasikini wao au sababu yoyote Ile.

Siku zote nasemaga kuwa, lolote utakalolitenda Kwa wenzako nawe utatendwa Vivo hivyo Kwa kipimo cha kujaa na kufurika.

Usidhani upo salama wewe na familia yako kuwaumiza wengine Kwa vile unacheo cha muda ambacho ni hakika hukuwa nacho na hautakuwa nacho hata nusu ya Uhai wako.

Inaumiza,
Lazima tujali maisha ya wengine.
Lazima tupendane.
Tuwapende hata Wale wanaoonekana dhaifu, sio tuwapenda wenye wadhfa na sifa za kutukuka.

Tuache kuumizana,
MUNGU atalipa Kwetu na hata Kwa watoto wetu.
Kama tuliwaumiza wao na watoto wao, basi nasi tutaumizwa Sisi na watoto wetu.

Kwa nini isiandaliwe programu ya kuwachangia hawa watu?
 
Wazo lako ni zuri ila kawaida michango ambayo inahitaji uratibu mzuri ni kama huu unouzungumzia. Kwanza tathmini za uharibifu zifanyike na zifanywe kwa waledi kuepuka mamluki na baada ya hapo mahitaji ndo yatajulikana kwa mfanyabiashara aliyeathirika na hali yake kikipato. Kabla ya hapo ndo yale unasikia kala rambirambi.
 
Naam MKUU.

Uongozi wa soko unaowajibu wa kuwa sehemu ya tathmini ingawaje hofu ya ufisadi kwenye michango huweza kujitokeza
 
Serikali itafute namna ya kuwarudishia sehemu ya kile walichopoteza, kama wahanga wameamua kujenga tena vibanda vyao ili waendelee kujitafutia kipato kwanini polisi wawavunjie usiku na kuweka ulinzi mkali?

Hawa jamaa wanaokula kwa urefu wa kamba zao hawajui maratizo ya watu wa hali ya chini, ndio maana walianza kwa kuwavunjia machinga.
 
Serikali itafute namna ya kuwarudishia sehemu ya kile walichopoteza, kama wahanga wameamua kujenga tena vibanda vyao ili waendelee kujitafutia kipato kwanini polisi wavunje usiku?

Na ndio maana nikasema lolote lifanywalo likadhuru wengine, Mkono huo huo utadhuriwa mara elfu elfu
 
Shida ya hapa bongo ni takwimu, kuna wengine unakuta wanafanya kazi humo sokoni bila kujulikana kwa uongozi wa soko.
Hao hata wakidai hawatapewa pesa.

Ila hawa watu wanatesaka sana. Serikali na wadau wafanye namna.
 
Serikali itafute namna ya kuwarudishia sehemu ya kile walichopoteza, kama wahanga wameamua kujenga tena vibanda vyao ili waendelee kujitafutia kipato kwanini polisi wawavunjie usiku na kuweka ulinzi mkali?

Hawa jamaa wanaokula kwa urefu wa kamba zao hawajui maratizo ya watu wa hali ya chini, ndio maana walianza kwa kuwavunjia machinga.
Hii ni kazi ya serekali kuna wizara ya majanga kila baje upitishwaji pesa kwajili majanga kama moto nk wamuulize waziri
 
Shida ya hapa bongo ni takwimu, kuna wengine unakuta wanafanya kazi humo sokoni bila kujulikana kwa uongozi wa soko.
Hao hata wakidai hawatapewa pesa.

Ila hawa watu wanatesaka sana. Serikali na wadau wafanye namna.

Umeongea point Mkuu
 
Back
Top Bottom