Wahariri Tv zetu hebu wastueni watangaza mpira kati ya Guinea na Equatorial Guinea. Guinea ziko mbili Guinea Bissau na Guinea conakry

Kuna Equatorial guinea mji mkuu ni Malabo, Kuna Guinea yenye mji mkuu Conakry, Kuna Guinea mji mkuu wake ni Bissau zote hizi zipo Africa. Lakini ipo Guinea ya Oceania inaitwa Papua New Guinea mji mkuu unaitwa Port Moresby hii nchi inapatikana kwenye mpaka wa bara Asia na Australia kwenye vijisiwa vingivingi viitwavyo Micronesia, pia Kunapatika visiwa jirani kama vile Tuvalu, Fiji, Vanuatu etc.
 
mchezaji wa Guinea alipokosa penalti mtangazaji akawa anamkashifu kila dakika kwa ndevu zake mtangazaji mpumbavu sana unamkashimu mtu ndevu zake kila mara kila mara huoni aibu niikuite mbwa wewe mtangazaji
 
Ujuaji tu!

Guinea 🇬🇳 jina lake lipo hivyo-hivyo na Conakry ni mji mkuu. Pia, kuna Guinea-Bissau na Equatorial Guinea kwa Africa na Papua New Guinea kwa Oceania.
na kuna pa mdomo guinea ipo uwingereza
 
ziko 3 na equatoria guinea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchambuzi wa mpira na anayejuwa historia ni dr leaky tu
Wengine wote blah blah

Ova
 
Hata wewe ni kilaza vile vile
Kuna guinea 3 Africa na moja IPO Asia

Equitorial guinea
Guinea Conakry
Guinea Bissau
Haya yote ni mataifa matatu tofauti na yapo Africa
Nyingine ni new Papua Guinea hiyo IPO Asia na Kuna black people vile vile

basi na wewe pia ni kilaza mkubwa, kwa sababu hakuna nchi duniani inaitwa Guinea Conakry, kama ambavyo hakuna inchi inayoitwa Tanzania Dodoma.

Kuna:

Republic of Guinea
Republic of Guinea-Bissau
Republic of Equatorial Guinea
 
Nchi ziko tatu
1. Guinea
2. Guinea-Bissau
3. Equitorial Guinea

Guinea ya kwanza, inatamkwa hivyo hivyo kama Guinea bila kuongeza neno lolote
Ww ndo upo sahihi huyo mtoa mada nae kakosea. Hlf hz timu zote mwaka huu zimeshiriki afcon
 
Ukiweza waambie Mods waffute huu uongo. Hakuna nchi duniani inaitwa Guinea Conakry. Hiyo ni Sawa na kusema kuna nchi inaitwa Kenya Nairobi. Conakry ni Mji Mkuu wa nchi inayoitwa Guinea.
 
Watangazaji wengi wa bongo ni vihiyo..wanasema wenyewe hawakaguliwi vyeti...wanaangaliwa vipaji..na ndio maana hawana wanachokijua..
 
New Papua guinea, guinea bissau , equatorial guinea, maneno mengine wanaweka Ili kutofautisha kama Congo brazaville na Dr congo
 
Hakuna nchi inayoitwa Guinea Conakry. Inaitwa Guinea.
 
Ujuaji tu!

Guinea 🇬🇳 jina lake lipo hivyo-hivyo na Conakry ni mji mkuu. Pia, kuna Guinea-Bissau na Equatorial Guinea kwa Africa na Papua New Guinea kwa Oceania.
nilikuwa nasubiria comment yako mkuu nifunge mada

case closed

GGMU
 
Hata wewe ni kilaza vile vile
Kuna guinea 3 Africa na moja IPO Asia

Equitorial guinea
Guinea Conakry
Guinea Bissau
Haya yote ni mataifa matatu tofauti na yapo Africa
Nyingine ni new Papua Guinea hiyo IPO Asia na Kuna black people vile vile
Faza na wewe ni kilaza ni PNG PAPUA NEW GUINEA
 
TBC fm ndiyo usiseme watangazaji muda mwingi wanaongea yakwao badala ya kutangaza mpira
 
Ukiweza waambie Mods waffute huu uongo. Hakuna nchi duniani inaitwa Guinea Conakry. Hiyo ni Sawa na kusema kuna nchi inaitwa Kenya Nairobi. Conakry ni Mji Mkuu wa nchi inayoitwa Guinea.
Hujasoma uandishi wa habari wewe .Mwandishi sio kasuku anapayuka tu Kuna kufanya analysis mfano Guinea ziko nyingi msikilizaji hutakiwi kumchukulia kama mtaalamu mbobezi wa jiografia anatakiwa aeleze Guinea ipi inacheza kusaidia hata mbumbumbu aliyefeli la saba kuelewa huo mpira anaotangaza anatangaza kwenye mass .Na mass communication Ina principle zake kuwa inatakiwa majority mass waelewe sio wasomi tu hicho unatangaza unageuka mtangazaji na mwalimu pia

Chombo Cha habari ni mass communication moja ya sifa za message ya mass communication ni kuwa message must be understood by masses not few ndio maana nikasema waongeze neno kuwa Timu inayocheza ni Guinea Conakry na pale waweza chomekea kuelimisha mass kuwa why wanasema Guinea Conakry kuwa Kuna Guinea nyingi wakazitaja kukoleza vionjo huku wakitoa elimu kufanya jiografia iwe hai Kwa wasikilizaji hata kesho wakikutana vijiwe vya kahawa watamsifu mtangazaji kuwa mchambuzi na mtangazaji mahiri na wai kugeuka wachambuzi mahiri kuhusu mchezo na chombo Cha habari kupata viewers wengi baadaye kuwa kule Kuna watangazaji mahiri

Kutangaza sio kazi ya ukasuku
 
TBC fm ndiyo usiseme watangazaji muda mwingi wanaongea yakwao badala ya kutangaza mpira
Vyombo vingi vya habari vina shida Hadi wapiga kamera unakuta mtu anatangaza taarifa ya habari ya mafuriko kamera badala ya kuonyesha mafuriko inamlenga tu mtangazaji wakati mtangazaji alitakiwa asikike tu audio picha za mafuriko ndizo zitawale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…