Wahasibu wasiwe wanahusishwa kesi za wizi wa manunuzi, upigaji huwa unafanywa na maafisa manunuzi, wahasibu huwa wanatoa pesa tu na hawana kosa.

Wahasibu wasiwe wanahusishwa kesi za wizi wa manunuzi, upigaji huwa unafanywa na maafisa manunuzi, wahasibu huwa wanatoa pesa tu na hawana kosa.

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Afisa manunuzi anaenda kwa muhasibu kuomba kupewa Bilioni 2 amlipe mkandarasi tenda ya ujenzi, hio kazi ya kwenye tenda ni wazi kabisa kiuhalisia haivuki hata milioni 200 lakini muhasibu akijaribu kufungua mdomo ataambiwa afanye kazi yake hayo mambo ya manunuzi hayamhusu, hapo muhasibu anaingia vipi kwenye wizi ?

Afisa manunuzi anaenda kwa muhasibu kuomba kupewa Milioni 500 ili alipie manunuzi ya computer za taasisi, hizo computer ni wazi kabisa sokoni unazipata zikiwa mpya kwa milioni 100 tu lakini muhasibu akijaribu kufungua mdomo ataambiwa afanye kazi yake hayo mambo ya manunuzi hayamhusu, hapo muhasibu anaingia vipi kwenye wizi ?
 
Wahasibu hawana makosa sema tunafeli kwenye kujitetea hawa afisa manunuzi wanajua kujitetea but sisi tunasainishana tu
 
Afisa manunuzi kampa mkandarasi tenda ya bilioni 2 kufanya kazi ya milioni 300, mhasibu katoa hizo milioni 300, kosa lake lipi ?

Afisa manunuzi ametumia shilingi milioni 200 kununua computer ambazo sokoni zina thamani ya milioni 50, mhasibu katoa hizo milioni 200, kosa lake lipi ?

Afisa manunuzi ametumia milioni 2 kwajili ya kutafuta mchoraji wa nembo ya shirika, mchoraji kapewa elf 80, mhasibu katoa hizo milioni 2, Kosa lake ni lipi ?
Askari wa anga karudi
 
Aliyetoa na aliyepokea , wote manzi ga nyanza.
 
Aliyetoa na aliyepokea , wote manzi ga nyanza.
Alietoa anahusika kivipi hapo ?

Afisa manunuzi yeye anaomba shilingi milioni 10 kununua peni ambazo ukipiga hesabu kwa peni moja moja unakuta ni elf 5 kwa kila peni, tena ni hizi peni za 500 madukani. Muhasibu ukijaribu kufungua mdomo kwamba hizo peni ni 500 unaambiwa "fanya kazi yako ya uhasibu kusaini imetoka shilingi milioni 10 ya manunuzi, kama hutaki nenda kwa mkurugenzi" mambo ya manunuzi hayakuhusu" Hapo muhasibu una kosa lipi ?
 
Kwenye internal controls kuna controls zinaitwa detective controls..muhasibu una wajibu wa kuzuia
 
Kwenye internal controls kuna controls zinaitwa detective controls..muhasibu una wajibu wa kuzuia
hayo mambo kwa nchi hasa za Africa yapo kinadharia sana utabaki kujifunza tu darasani, kiuhalisia ni tofauti
 
hayo mambo kwa nchi hasa za Africa yapo kinadharia sana utabaki kujifunza tu darasani, kiuhalisia ni tofauti
Pre-audit ipo kinadharia? Wewe ni muhasibu garasa. Muhasibu anawezaje kulipa bila kupitia nyaraka muhimu za manunuzi kwenye subject file? Hiyo control ni detective. Kama wanasema funga mdomo waambie waweke kwa maandishi hiyo funga mdomo. Wakigoma waambie walipe wao kama wanaweza bila muhasibu.
Mkaguzi akija huwezi kumwmabia huo ujinga
 
Hayo mambo yangekuwa yanafuata msisitizo wala tungekuwa hatuoni madudu kwenye ripoti ya cag.

Napozungumzia hayo madudu nadhani unanipata vema, hata cag kila mwaka anatoa mapendekezo lakini hayo makaratasi ya mapendekezo yanafungiwa maandazi
 
Hayo mambo yangekuwa yanafuata msisitizo wala tungekuwa hatuoni madudu kwenye ripoti ya cag.

Napozungumzia hayo madudu nadhani unanipata vema,
Nachosema mimi ni wewe kufanya sehemu yako. Usipotimiza wajibu wako huyo CAG na PCCB wanakuja kukuokota tu hata kama huusiki
 
Alietoa anahusika kivipi hapo ?

Afisa manunuzi yeye anaomba shilingi milioni 10 kununua peni ambazo ukipiga hesabu kwa peni moja moja unakuta ni elf 5 kwa kila peni, tena ni hizi peni za 500 madukani. Muhasibu ukijaribu kufungua mdomo kwamba hizo peni ni 500 unaambiwa "funga bakuli lako ufanye kazi yako ya uhasibu kusaini imetoka shilingi milioni 10 ya manunuzi, mambo ya manunuzi hayakuhusu" Hapo muhasibu una kosa lipi ?
Hiyo Quotation kwani yeye haioni? hawezi kujudge chochote? Kwamba yeye ni kutoa tu? Mhasibu gani ambaye huwezi kuhisi/kubaini udanganyifu wa taarifa za manunuzi, na kwanini usitiliwe mashaka huo uhasibu wako? Kwamba kwa kuwa pesa ni ya umma basi ni kutoa tu bila kufikiria marambilimbili kuhusiana na kiasi cha fesha kinachoombwa, ingekuwa ni fedha za kampuni ungeweza kufanya vivyo hivyo? Au kwa kuwa ni fedha za serikali ambapo mtumishi huyo ana kinga ya kiutumishi ndo maana anatoa tu, hebu Acha kutuletea utetezi wako wa hovyohovyo hapa.
 
Back
Top Bottom