Huyo jamaa anaitwa Dr. Ellie huwa simuelewi na wala sijawahi kumuelewa. Nimejaribu kukaa zaidi ya mara tano kumsikiliza (Clauds Tv), lakini sikupata chochote na wala haeleweki. Sio mimi pekee yangu hata watangazaji wanaokuwa naye kwenye kipindi huwa hawamuelewi mbali na watu wengi wanaofuatilia kipindi kutokumuelewa kabisa. Jamaa haeleweki kama anahubiri, anafundisha au anafafanua chochote. Ni mwendo wa kuibuka na vifalsafa vya ovyo ovyo vya hapa na pale na kuongea kwa mapozi fulani ya mbwembwe za kisomi na sasa kubleach nywele, too much scrubing na make up.
Jamaa ni msanii fulani anayeiga namna marehemu mchungaji Mitimingi (ambaye alikuwa anaeleweka vyema) alivyokuwa akifanya vipindi vyake kwenye Tv.
Nina mashaka sana kama jamaa kweli ana usomi wa level ya udaktari (PhD), nahisi kwa 90% jamaa ni msanii.