Wahenga wenzangu njoo tukumbushane vipindi vilivyobamba RTD enzi hizoo

Nakumbuka baada ya kuacha kusikiliza TBC na kuhamia RFA nilikuwa napenda kusikiliza hiki kipindi cha Sitasahau kilikuwa kinarushwa saa mbili asubuhi siku ya jumapili kikifuatiwa na kile cha vitu vilivyovunja record sijui kiliitwaje baada ya hapo kilifuatiwa na Je huu ni uungwana???? Nlikuwa shabiki sana wa hilki kipindi wakati huo mtangazaji alikuwa Fredua ( sijui ndio inaandikwa hivi? ) baadae akaja mwingine anaitwa nani sijui mtani.

Baada ya Sitasahau, kilikuwa kinafuatiwa na kipindi cha ''Je wajua?" mtangazaji alikuwa Samada Maduhu(kama sijakosea)
 
Yes ni je wajua daah nimezeeka hadi nasahau jina la kipindi nilichokuwa nakipenda. Ila nilikuwa sikipendi kihivyo nilikuwa natamani kiishe haraka nisikilize Je huu ni uungwana???? Kabla hakijaisha nilikuwa natimuliwa kwenda kanisani uzuri kanisa lilikuwa karibu kwa hiyo nilikuwa hata sipati tabu. Nilikuwa nagoma kwenda Sunday school nadai mi mkubwa kumbe nipo addicted na vipindi jamani.. Maisha yale
 
Mimi kipindi cha Sitasahau kilikuwa kinanivutia sana na stori za watu mbalimbali kuhusu misukosuko ya maisha yao.

Simulizi zingine zilikuwa zinachukua zaidi ya mwezi bado hazijakamilika na nilikuwa naifuatilia hadi mwisho
 
Shikamoo Muhenga Ses. 🙈🙈🙈🙈

Japo sivijui hivyo vipindi huku na mie ni Muhenga pia Ses kwa hili naomba nikazie tu maana sina jinsi.💃💃💃💃💃
Hahahaaaa, kazia tu Hajar maana wewe utakua muhenga mamboleo

Tena wakati huo hakuna bongo fleva, halafu wanamuziki waimbaji wa kiume walikua wanajivisha uhusika wa wanawake wakati wanapotaka kufikisha ujumbe wa kimuziki unaomhusu mwanamke
 
Nilikua nakaa na bibi enzi hizo... nilikua naamshwa kila asubuhi na kipindi cha majira... kiasi kwamba mpaka leo ile soundtrack yake ndo alarm tone yangu yani inlmekaa kichwani balaa
 
Mimi nakumbuka ile ya RFA watanzania tuzungumze magazeti. Ilikuwa kama ile ngoma ikinikuta nipo najiandaa najua nimeshachelewa ila ikinikuta ndio natoka mlangoni najua nimeshawahi ilikuwa saa ngapi sijui ile
 
Ha ha memories back then mi nilikua nachukia sana nikiiskia tu majiraaaa najua ndo naamshwa sasa niende shule.... ila sasa nakumbuka sana zama hizo
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji23] Kijaruba na Misakato cha marehemu nyaisanga
 
Mimi nakumbuka ile ya RFA watanzania tuzungumze magazeti. Ilikuwa kama ile ngoma ikinikuta nipo najiandaa najua nimeshachelewa ila ikinikuta ndio natoka mlangoni najua nimeshawahi ilikuwa saa ngapi sijui ile
Hizo jingle zote mbili ninazo kutoka kwa wapigaji Original, nitafuteni kwa SMS 0752 220 649 niwatumie saivi
 
Kipindi cha Pwagu na Pwaguzi siku hz TBC wanakirushaga saa sita dk 45 kila siku mchana
 
Back
Top Bottom