Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 7,093
- 10,469
Katika muendelezo wangu wa kufanya Utafiti Binafsi wa kuweza kupata au kujaribu kupata majibu ya kwa nini sisi tuko nyuma sana kimaendeleo kulinganisha na jamii nyingine hapa Duniani, nimegundua kifuatacho!
Nimejaribu kufanya Jaribio dogo la kuzunguka kwenye Maduka ya Wahindi na sehemu zao za Uzalishaji, nilichoona ni kwamba hakuna Duka hata moja nililoingia la Muhindi au Ofisi au kiwanda cha Muhindi ambapo nimekuta kuna TV na wanaangalia Bunge moja kwa moja (live), lkn nilipo jaribu kuzunguka kwenye Ofisi na sehemu za shughuli za Waswahili wenzangu nimekuta wafanyakazi wako makini na kuangalia Bunge live badala ya kufanya kazi na kuongeza kipato chao!
Nilichojifunza ni kwamba sisi tuko maskini kwa sababu hatupendi na hatuthamini kazi, hawa Wahindi ktk Nchi nzima wako chini ya 300, 000 (laki tatu) katika Nchi ya watu zaidi ya milioni 40, lakini wanamiliki zaidi ya asilimia 85% ya Uchumi wa Tanzania, Hapo tuna tatizo!
Serikali piga Marufuku Bunge Kuonyeshwa Muda wa Kazi, Ili tuweze Kufanya kazi kwa Bidii na Umakini na tuweze kushindana na Wahindi na jamii nyingine Duniani!