Glory Thomas
New Member
- Jun 12, 2023
- 2
- 4
KUCHOCHEA USAWA WA AJIRA: WAHITIMU MASKINI WAPEWE KIPAUMBELE KWENYE SOKO LA AJIRA.
KWA KUIGA MFANO WA TASAF
UTANGULIZI:
Katika juhudi za kujenga jamii yenye usawa na maendeleo, ni muhimu kuangalia njia za kuwezesha wahitimu kutoka kaya maskini kupata fursa sawa za ajira. Programu ya Tanzania Social Action Fund (TASAF) imedhihirisha ufanisi wake katika kusaida wanufaika wake kupata ya elimu ya juu, ili wapate kuendelea na Masomo. Barua wanazopewa wanufaika kutoka TASAF wanapokuwa wanaomba mikopo ya elimu ya juu huwapa uhakika wa mkopo na inakuwa chachu ya uwajibikaji wakati wa masomo yao. Kwa kujifunza kutoka mfano huu wa TASAF, serikali inaweza kuongeza kipaumbele kwa wahitimu kutoka kaya maskini katika soko la ajira.
MCHANGO WA TASAF KATIKA KUSAIDIA WANAFUNZI KUTOKA KAYA MASKINI:
TASAF imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia wanafunzi kutoka kaya maskini kupata mikopo ya elimu ya juu. TASAF wanatoa barua za utambulisho kwa wanufaika wake, ambazo wanaweza kuziambatanisha katika maombi yao ya mikopo. Barua hizi zinaonyesha kuwa wanafunzi hao wanatoka kwenye kaya maskini na wanahitaji msaada wa kifedha kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu. Kwa kufanya hivyo, wanapewa kipaumbele na fursa ya kupata mikopo ya elimu ya juu kwa asilimia 100.
KUZINGATIA MFANO WA TASAF NINI KIFANYIKE:
Kupitia mfano wa TASAF, serikali inaweza kuiga utaratibu huu katika kipaumbele cha ajira kwa wahitimu kutoka kaya maskini. Kwa kutoa barua za utambulisho na kuzingatia historia ya mahitaji yao ya kifedha, serikali inaweza kuwatambua wahitimu hawa kama kundi maalum ambalo linahitaji fursa za ajira zaidi. Kama vilema wavyatambulika kuwa kundi maalumu, Kipaumbele hiki kitawawezesha kupata nafasi ya kushiriki katika mchakato wa kuajiriwa kulingana na ujuzi walionao.
NINI KITATOKEA:
wahitimu wa Kaya maskini wakipewa kipaumbele kwenye ajira, itasaidia Kukuza Uwajibikaji na Kujiamini kwa Wahitimu
Kipaumbele cha ajira kwa wahitimu kutoka kaya maskini kitaleta matokeo chanya kwa kuchochea uwajibikaji na kujiamini. Kwa kuwa wanatambulika kama wanufaika wa programu ya kijamii kama TASAF, wahitimu hawa watajihisi kuthaminiwa na kujisikia na nguvu zaidi katika kushiriki katika masoko ya ajira. Pia, kutambuliwa huku kutawapa motisha zaidi kujituma katika masomo yao na kujenga uwezo wao ili kukudhi uhitaji wa soko la ajira, uhakika wa ajira kwa wahitimu wa elimu ya juu unaongeza ufanisi wa wanafunzi vyuoni .
HITIMISHO:
Kipaumbele hiki kitachochea maendeleo ya taifa kwa kuchangia katika kupunguza umaskini na kuleta maendeleo ya kilamii na kiuchumi. Kwa pamoja, tunaweza kujenga jamii yenye fursa sawa na inayojali mahitaji ya wote.
Chini ni kielelezo cha mfano wa barua TASAF inayowapa wanufaika wake ili kupata kimaupembele
Kwenye mikopo ya elimu ya juuView attachment 2696036

Upvote
2