Wahitimu shule za vipaji maalum

Wahitimu shule za vipaji maalum

paqwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
2,106
Reaction score
2,831
Wadau, kuna shule ambazo serikali kwa utashi wake ilizitambua na kupeleka wanafunzi ambao inaamini ni vipaji maalum kiakili, mfano, Ilboru, Tabora school(boys and girls), Kibaha, Mzumbe, Kilakala na Msalato.

Lengo lilikuwa kuwatumia watu hawa katika kujenga taifa, je, wanaomaliza/waliomaliza shule hizi wanatambulikaje katika jamii? Wanathaminiwaje? Wapo wapi?
 
Zilikuwa sifa za kijinga tuuu. , Unaona kuwa unasoma ilboru , weru weru eti ya vipanga kumbe sifa tuuu za kisenge ,

kama hivi hiv vyuoni tumekutana , supplementary kama zote tumezipata ...now ni jobless era....

Hence. Sifa za kijinga tuu. Tofauti ilikuwa ni Serikali kuwekeza resources nyingi kwenye hizo shule...............na kuwekeza kiduchu shule hizu tulizosomaaa.....
 
Mimi nilisoma Tabora boys advanced level leo hii naona umuhimu mkubwa wa kusoma shule za vipaji maana nilipata kazi kirahisi sana baada ya mwajiri wangu kuona kuwa nimesoma hiyo shule.
Nami nimesoma Tabora girls aka Warsaw advanced level na sikusota mtaani after graduation,nikapiga interview leo hii niko govt naisaidia serikali yangu kukusanya mapato 🙏
 
Wadau, kuna shule ambazo serikali kwa utashi wake ilizitambua na kupeleka wanafunzi ambao inaamini ni vipaji maalum kiakili, mfano, Ilboru, Tabora school(boys and girls), Kibaha, Mzumbe, Kilakala na Msalato.

Lengo lilikuwa kuwatumia watu hawa katika kujenga taifa, je, wanaomaliza/waliomaliza shule hizi wanatambulikaje katika jamii? Wanathaminiwaje? Wapo wapi?
Mimi na Alumni wenzangu ninao wajua..almost 90% yetu ndo tuko vizuri kimaisha na tumefanya mambo mengi kulisaidia Taifa.

Binafsi naona Taifa lilitutendea haki nasi tumerudisha kwa Taifa.

Tunajitahidi kadri ya uwezo na vipaji vyetu japo kuna mazingira ambayo siyo rafiki. Tumezungukwa na vilaza wengi ambao wao kazi yao ni kupenda pesa bila kujali output na outcome .
 
Acha sifa wewe umelitendea nini hiii taifa,,km sio mwalimu hakuna ulicholitendea hili taifa
 
Zilikuwa sifa za kijinga tuuu. , Unaona kuwa unasoma ilboru , weru weru eti ya vipanga kumbe sifa tuuu za kisenge ,

kama hivi hiv vyuoni tumekutana , supplementary kama zote tumezipata ...now ni jobless era....

Hence. Sifa za kijinga tuu. Tofauti ilikuwa ni Serikali kuwekeza resources nyingi kwenye hizo shule...............na kuwekeza kiduchu shule hizu tulizosomaaa.....
Appreciate waliokuzidi uwezo wakati Fulani hiyo kuwa na hasira na chuki zidi yao haikusaidii kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami nimesoma Tabora girls aka Warsaw advanced level na sikusota mtaani after graduation,nikapiga interview leo hii niko govt naisaidia serikali yangu kukusanya mapato 🙏
Kumbe wewe Ni mwoso. Haya bana usikute nilishakubambia kwenye disco Basi humu mtandaoni hatufahamiani. Berlin Wall ,umemaliza mwaka gani
 
Wadau, kuna shule ambazo serikali kwa utashi wake ilizitambua na kupeleka wanafunzi ambao inaamini ni vipaji maalum kiakili, mfano, Ilboru, Tabora school(boys and girls), Kibaha, Mzumbe, Kilakala na Msalato.

Lengo lilikuwa kuwatumia watu hawa katika kujenga taifa, je, wanaomaliza/waliomaliza shule hizi wanatambulikaje katika jamii? Wanathaminiwaje? Wapo wapi?
Kama wameajiriwa utajuaje.
 
Shule yangu ya Pugu secondary imechangia maendeleo ya nchi kama ifuatavyo:
1. Imetoa rais mkapa wa awamu ya tatu, ambaye alifanikiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kimfumo
2. Imetoa waziri Pinda
3.Imetoa spika wa bunge la JMT MH. Pius Msekwa
4. Kwa awamu hii, imetoa waziri wa maji, mh.Uwesu, anapiga kazi sana
5.Pugu sekondari ipo jimbo la ukonga, hivyo hata mbunge wa sasa Mh.Slaa ametokana na shule ya Pugu
Inaendelea..........

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom