Musa17 , hizi inshu za majigambo na dharua zisizo na vichwa ni sisi wenyewe tunalipa kichwa ,
tatizo letu ni dogo sana ukilinganisha na wenzetu wa fani nyingine (mfano biashara) ambao wanapenda sana kudharauliana kutokana na vyuo walivyosoma , tumeshajifunza kwamba haisaidii chochote hivyo hatuna haja ya kuendeleza ushindani usio na tija kwetu .
Ningependa kukueleza tu bwana Musa ,ukimuona mtu wa UDSM Eng anapiga porojo nyingi na kejeli, kuna uwezekano mkubwa huyo mtu hajiamini na anasubiria title ya UDSM imubebe ,kitu ambacho ni kujidanganya tu.
Mimi nimesoma UDSM , najivunia kusoma chuo kikongwe tz ila kamwe siwezi kukudharau wewe kwa sababu tu umesoma DIT wakati najua wapo wengi tu wenye uwezo wao huko DIT