SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la stories of change. Ni tumaini langu nyote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao.

Naanza kwa kuelezea maisha ya mtaani na baadhi ya fursa zenye kuhitaji mitaji na zisizohitaji mitaji na changamoto zake na vipi tunaweza kuzikabili changamoto na kutuwezesha kupita katika baadhi ya hizo fursa na tuweze kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kichumi kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi za jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa sio siri imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

NITAANZA KUELEZEA CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kutokujiamini na kutokubaliana na hali halisi iliyopo. Wengi hawa jiamini na wanashindwa kufikiria nje ya kitu walichosomea na kukianza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanoyowazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Kukosa kampani au muunganiko na watu waliotangulia kwenye mitaa, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye mitaa kiutaftaji. Japo hio sio sana.

4. Kutokua na mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kutokua na uelewa wa mitaa na utaftaji wenyewe. Yaani kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Hii inahusika saana baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata gunia wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba gunia.

JINSI GANI WANAWEZA KUPAMBANA NA HIZI CHANGAMOTO:-

1. Kujikubali na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

2. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ina muwia ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

3. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utaftaji mtaani ni ushindani.

4. Kuyajua mazingira ya biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji muunganiko na wanaoitambua biashara husika unayotaka kuanzisha kwenye mazingira unayopanga.

5. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu, hapa matumizi yale yasiyomuhimu ambayo yanafuja pesa hainabudi kuyaacha. Mfano unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

6. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufwata mkumbo. Je mhitimu unaweza kitu gani kama ni kilimo basi fanya kilimo kama ni ufundi fanya ufundi.

7. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZILIZOPO KATIKA JAMII ZETU AMBAZO WAHITIMU AU MTAFUTAJI YEYOTE ANAWEZA KUZITAZAMA NA KUANZA KUJIPATIA KIPATO KUPITIA HIZO FURSA

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuliko na viwanda kuna upatikanaji wa vibarua wa kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki kwenye viwanda. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo, mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi mia 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba viwanja nk
Hii nayo haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Inafaa japo haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila itataka utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk, (Ufundi wa aina yoyote).

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.

Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kujichanganya kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji
Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo kama mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima. Uvuvi pia utahitaji mtaji kununua nyavu nk.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa. Hii ni baadhi ya mifano.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo kama pana uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MAMBO YANAYO WEZA KUTEKELEZWA NA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KUWASAIDIA VIJANA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha na muongozo wa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali. Hapa serikali inapaswa kuwa mhusika mkuu wakuwapa vijana wasio na kazi usaidizi.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa. (Bajeti ya kila mwaka iwepo kiasi cha kuwasaidia)

Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha wanaowajibu wakuwawezesha kwa mikopo isiyo na riba

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Serikali inapaswa kuwawekea mazingira mazuri vijana wanaoanza utafutaji kwa maana itasaidia kuwa inua. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi.

4. Kuwapatia semina mbali mbali za kiujasirimali. Hapa lazima kuwapa semina juu ya fursa zilizopo na vipi wataweza kukabiliana na changamoto katika utafutaji.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi.

6. Serikali na sekta binafsi kuwa husisha vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala iwe rahisi kuwa andaa vijana kujitegemea kulingana na elimu waipatayo.

8.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi uwazi uwepo.

9. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

10. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

11. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

Hitimisho
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ufuatao:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimwamini kila mtu katika kufanya utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa hawa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele. (Hitaji la wateja).

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao.

(viii). Kuwa msafi au zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri na boresha mazingira ya ofisi yako.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

Hapa nimefikia mwisho wa andiko langu. Natumaini kidogo kitaeleweka kwa wengi haijaelezea kila.kitu ila nimeelezea kwa uchache kwa yale niliyojionea na kujifunza mtaani.

MUHIMU:
Msisahau kupigia kura andiko hili [emoji1317].
Nimelikubali hili andiko lina maana sana
 
Nimelikubali hili andiko lina maana sana
Shukran mkuu na.karibu ukiwepo uzoefu katika utafutaji iwe changamoto au.lolote kiutafutaji karibu [emoji1317][emoji1303]
 
Hongera andiko ni zuri, i think kwenye kilimo kuna potential, serikali ijimilikishe mashamba, igawe kwa watu,tuna ardhi kubwa kumtosha kila kijana, tuki utilise fully ardhi tuliyopewa wala hakuna haja ya tozo!,,Kilimo kina potential ya kuongeza our tax base,system ikiwekwa kwa mfano kwa kila mmiliki wa shamba kadri anavyoajiri watu shambani kwake ndivyo anavyolipa less tax itawamotivate watu kumiliki mashamba na kuajiri more,then small tax iwekwe kwa hao waliokuwa employed kwenye hilo shamba,sababu ni wengi then revenues zitaongezeka
 
Shukran kwa mawazo yako mazuri yanayolenga kuwainua vijana na taifa kwa ujumla. Kupitia uliyosema mfano hilo la kugawia vijana mashamba ambayo serikali.itajimilikisha na kuufanya kama mradi mahususi kuwawezesha vijana kwa watakao ona kilimo kinawafaaa kuanza utafutaji.

Tanzania ni.nchi yenye ardhi nzuri, ardhi iliyobarikiwa nadhani kwa mikoa mingi mfano morogoro, tanga, pwani, manyara nk aridhi zipo za kutosha.

Ila serikali itapaswa pia kuwa na uhusiano bora wa kimataifa utakao rahisish uuzaji wa mazao ya kilimo nje ya nchi kuepuka kutegemea soko la ndani tu. Pili viwanda viongezwe kuinua soko la ndani. Na iwawezeshe maana kilimo ni maandali mazuri kwa kila hatua
 
Kuna mikoa inalima saana unaweza kutuelezea kidogo maana nimeona sana sana unauelewa na kilimo maadam Rebecca . Karibu uwanja wako
 
Ni kweli ,serikali iki deal na ku identify masoko ya mazao ndani na nje ya nchi then kulima iwe kazi ya wananchi/vijana tutamove foward. i think vijana wengi wanasita kuingia kwenye kilimo sababu ya unpredictability ..wakiwa na uhakika wa kuuza na kupata faida wengi wataingia kwenye kilimo.

Pili nahisi hii ya kuuza mazao ya kilimo nje ya Tanzania inahitaji mjadala mpana, in my opinion kuwe na Brand ambayo ni ya serikali, ndiyo itumike kuuza mazao nje ya nchi, people are more willing to buy something from trusted source, a brand that they can rely on, that can be traced. (trustability/dependability/traceability), hivyo basi serikali iji brand na kuchukua jukumu la kununua mazao kutoka kwa wananchi na kuuza nje. Trust me zikiwekwa brand mbili moja ya serikali nyingine ya random person from the country utashangaa hio ya serikali inanunuliwa zaidi. Sijui mnaonaje hili??lol

Umegusia viwanda,ni kweli tunahitaji sana vitu kama nyanya ingependeza kuwa proccessed,packed,kuna wakati zinakuwa bei mno na kuna wakati ni nyingi mno, proccessed makopo yangesaidia...lol
 
Kuna mikoa inalima saana unaweza kutuelezea kidogo maana nimeona sana sana unauelewa na kilimo maadam Rebecca . Karibu uwanja wako
Mkuu wala sina uelewa huo...nimezamia huku kiembe samaki siku nyingi,tunavua samaki hatulimi lol
 
Ni kweli ,serikali iki deal na ku identify masoko ya mazao ndani na nje ya nchi then kulima iwe kazi ya wananchi/vijana tutamove foward. i think vijana wengi wanasita kuingia kwenye kilimo sababu ya unpredictability ..wakiwa na uhakika wa kuuza na kupata faida wengi wataingia kwenye kilimo.

Pili nahisi hii ya kuuza mazao ya kilimo nje ya Tanzania inahitaji mjadala mpana, in my opinion kuwe na Brand ambayo ni ya serikali, ndiyo itumike kuuza mazao nje ya nchi, people are more willing to buy something from trusted source, a brand that they can rely on, that can be traced. (trustability/dependability/traceability), hivyo basi serikali iji brand na kuchukua jukumu la kununua mazao kutoka kwa wananchi na kuuza nje. Trust me zikiwekwa brand mbili moja ya serikali nyingine ya random person from the country utashangaa hio ya serikali inanunuliwa zaidi. Sijui mnaonaje hili??lol

Umegusia viwanda,ni kweli tunahitaji sana vitu kama nyanya ingependeza kuwa proccessed,packed,kuna wakati zinakuwa bei mno na kuna wakati ni nyingi mno, proccessed makopo yangesaidia...lol
Kweli. Ila nimepata wazo baada yankusoma tena hii reply yako. Dunia ya sasa biashara zinafanyika kwa kampuni moja na nyingine. Hata vijana wakiwezeshwa wanao uwezo wakufungua kampuni zao zima deal.na uuzaji wa mazao ndani na nje ya nchi na sio kwenda kizamani au kichwa kichwa.
 
Mkuu wala sina uelewa huo...nimezamia huku kiembe samaki siku nyingi,tunavua samaki hatulimi lol
Sio mbaya. Pia tunapoteza mazao mengi kama taifa kwa kukosa soko la uhakika, hifadhi za kutunza mazao kama matunda. Mfano msimu wa machungwa ukiingia wakulima wanapoteza mamia ya machingwa shambani kwa kuoza kutokana na uhaba au kutokuwa na maghala ya kisasa ya kuhifadhia matunda kwa muda mrefu.

Tena katika nchi hii ambayo tumebarikiwa ardhi nzuri lakini suala la sukari inayotokana na miwa lilitutia aibu na kuonesha jinsi gani hatuwezi kuzitumia rasilimali zetu kujiinua.

Hivi kuna mtu mmoja mmoja anaelima miwa na kuuzia viwanda nchini..?
 
Kuwa na kampuni binafsi inawezekana kuna sourcing sites kibao,lakini kukiwa na brand ya serikali kuna uzito zaidi,
 
Kuwa na kampuni binafsi inawezekana kuna sourcing sites kibao,lakini kukiwa na brand ya serikali kuna uzito zaidi,
Hapo napo nimekuelewa. Brand itakayokuwa km kiwakilishi au utambukisho wa bidhaa za kutoka nchini. Itakayo zingatia ubora kwa ajili ya kuilinda brand.
 
Mkuu wala sina uelewa huo...nimezamia huku kiembe samaki siku nyingi,tunavua samaki hatulimi lol
Uvuaji wa samaki nayo ni fursa samak inalika sana mjini na ni biashara nzuri nadhani pia. Kuna maziwa mito na bahari ya hindi samaki wanapatikana tulione na hilo.
 
Uvuaji wa samaki nayo ni fursa samak inalika sana mjini na ni biashara nzuri nadhani pia. Kuna maziwa mito na bahari ya hindi samaki wanapatikana tulione na hilo.
Waliokulia maeneo ya mito mikubwa bahari n maziwa watu wa Tanga, mtwara, mwanza, mara, kigoma, bagamoyo, zanzibar, nk mtupe uzoefu katika uvuaji wa samaki
 
Waliokulia maeneo ya mito mikubwa bahari n maziwa watu wa Tanga, mtwara, mwanza, mara, kigoma, bagamoyo, zanzibar, nk mtupe uzoefu katika uvuaji wa samaki
Ndio watuambie maana wengine tumekulia maeneo ambayo hata samaki kumuona akiwa mbichi tumeona ukubwani
 
Hapo napo nimekuelewa. Brand itakayokuwa km kiwakilishi au utambukisho wa bidhaa za kutoka nchini. Itakayo zingatia ubora kwa ajili ya kuilinda brand.

Sawa sawa, serikali itahakikisha jina lake halichafuliwi so watahakikisha wanauza bidhaa za ubora,na kwa vile bidhaa za ubora ndio zinatakiwa huko nje ita create demand ya products zetu,which means more job opportunities kwa vijana
 
Kweli itakua inafanania na tbs sema.kwa ajili mahususi ya kuzingatia biashara na mataifa ya nje inakuwa na bidhaa bora tu ili kulinda soko la bidhaa zetu[emoji1303]
 
Sio mbaya. Pia tunapoteza mazao mengi kama taifa kwa kukosa soko la uhakika, hifadhi za kutunza mazao kama matunda. Mfano msimu wa machungwa ukiingia wakulima wanapoteza mamia ya machingwa shambani kwa kuoza kutokana na uhaba au kutokuwa na maghala ya kisasa ya kuhifadhia matunda kwa muda mrefu.

Tena katika nchi hii ambayo tumebarikiwa ardhi nzuri lakini suala la sukari inayotokana na miwa lilitutia aibu na kuonesha jinsi gani hatuwezi kuzitumia rasilimali zetu kujiinua.

Hivi kuna mtu mmoja mmoja anaelima miwa na kuuzia viwanda nchini..?

changamoto zetu watanzania kwenye kilimo ambayo nadhani serikali inabidi waweke mkakati nayo ni maghala ya kuhifadhia ya kisasa ya mazao, na viwanda vya ndani wangeanza na hivyo kwanza..LOL...Thanks mkuu for this useful topic...all the best kwenye shindano... 👍 👍 👍 👍 👍 👍
 
changamoto zetu watanzania kwenye kilimo ambayo nadhani serikali inabidi waweke mkakati nayo ni maghala ya kuhifadhia ya kisasa ya mazao, na viwanda vya ndani wangeanza na hivyo kwanza..LOL...Thanks mkuu for this useful topic...all the best kwenye shindano... [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
Shukran kubwa kwako maadam Rebeca 83 kwa uhusika wako nadhani bado yapo mengi ya wewe kutujuza hususani huko.kwenye uvuvi. I hope ukikaa sawa tena utakuja na hitimisho la hapo kwenye uvuvi[emoji1317][emoji106][emoji2532]
 
Back
Top Bottom