Wahitimu wanne wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamefanikiwa kubuni gari inayotumia umeme

Wahitimu wanne wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamefanikiwa kubuni gari inayotumia umeme

rudia kusoma quote zangu za mwanzo utanielewa nilikuwa nakuuliza nini na unajibu nini😁😁
Uliniambia sijitambui na sijielewi kwa hiyo nikupe ushahidi kuhusu sensor za Sony kutumika kwenye iPhone
Nimekupa ushahidi unaanza kuzuga. Naelewa sana conversation yote hamna haja ya kurudia kusoma huko juu
 
Hii logic yako haimake sense
Hao waliotengeneza wakiwa form 5 ndio wana nafasi ya kuboresha gari lao waliloanza kulitengeneza
Hao wa NIT unaowaona huenda hawakuwahi kutengeneza wakiwa form 5 kwa hiyo ndio wametengeneza waliwa chuo. Ukiwekeza kupitia wao ndio watapata pesa na nafasi ya kuboresha
Sijui kwa nini nyinyi mnaona sawa, ila mimi sioni kama ni sawa kujisifu eti tuna wanafunzi wa form 5 wanatengeza gari la umeme halafu hata hatuwaendelezi. The same to hawa wa NIT kama tukiendelea kuwapuuza kuwa walichotengeneza ni kibaya na hakijafikia cha fulani inakuwa haina maana.
Kwanza sielewi hata watu kwenye comments wanakereka nini kuona wanafunzi wanafanya hivi chuoni. Ila Tanzania, eeh 🙌
Nabii hakubaliki kwao bro
 
Hivi kwa nini huwa hatupendi kuendeleza project za watu
Mfano huyo Kipanya inaonekana Bongo hata ukiwa na ubunifu, kama hauna mtaji na support haufiki popote. Labda hatuna mpango wa kuwa na viwanda, wanasiasa wanatudanganya tu 🤔
CCM ni baba wa uongo.
Matunda mengi sana yanaharibika kwa ukosefu wa viwanda vya kusindika/kuongeza thamani, sasa ndio waweze kiwanda/viwanda vya magari!!???

Hao vijana wabunifu na wengine wengi waliopo huko mitaani, kama serikali ya CCM ingethamini bunifu zao na kuziendeleza, hakika kama taifa tungenufaika sana.

Nilishangaa Askofu ambaye Dayosisi yake ina wakulima wengi wa ndizi ambapo bei ya juu ya mkungu mkubwa kabisa wa ndizi ni tsh 3000 (DSM ni 48,000), akimuomba VP serikali iwasaidie katika wazo lao la kufungua kiwanda cha kutengeneza bottled water, na serikali ikatoa 20 milioni kama mchango wake kwenye hicho kiwanda cha maji chupa!
 
Kwenye hizi comment nimegundua wabongo wngi hawapendi kuona wabongo wengine wakifanikiwa hata kidogo roho mbaya na wivu vimetawala sna

Magari yamegunduliwa miaka zaidi 200 iliyopita lakini Kila siku Kuna brand mpya na inauza vizuri

Asilimia kubwa ya products za china ni copy and paste ya mataifa mengine lakini wanaongoza Kwa uzalishaji duniani

Wanafunzi wanastahili kupongezwa sio Kwa sababu ya kutengeza gari ila Kwa sababu ya kuwa na mindset ya kuzalisha ndani ya nchi yetu

KUna mdada mmoja aliniambia Yuko London kwenye sekta ya afya lakini hudhubutu kuunganisha mbongo huko
 
Wahitimu wanne wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamefanikiwa kubuni gari inayotumia umeme baada ya kusukumwa na udadisi wa kutatua changamoto za usafiri hususani upande wa uchafuzi wa mazingira na unafuu wa gharama.

Tafadhali serikali, najua vitu vingi mnaboronga lakini kuhusu hili la magari walau mlichukulie serious. Burkina Faso tayari wanatengeneza magari ya umeme. Kwa wasioyajua yanaitwa "ITAOUA"
Na sisi hapa Tanzania tuwe na kiwanda chetu cha magari ya umeme. Anzeni na hawahawa vijana wa NIT. Mara nyingi ubunifu wa watu mnaacha upite tu mwisho wa siku kunakuwa hamna faida yoyote
Hebu safari hii badilikeni muwe serious na mageuzi ya viwanda Tanzania
View attachment 3531286
Okay. Vp Chuo Kikuu Mliman?
 
Back
Top Bottom