Nimekaa mahali hapa kuna redio ya kanisa moja la Arusha inanguruma. Kama kawaida ya hawa wahubiri mada kuu ni utoaji.
Nilishasema habari za fungu la kumi si mafundisho ya kikristo. Hata hao wayahudi waliopewa agizo hilo wana mfumo tofauti kabisa wa utoaji tofauti na haya mafundisho ya matapeli wa imani.
Kwa mfano kuna mwaka wa Sabato ( sabbatical year) ambapo fungu la kumi halitolewi maana ardhi ya Israeli ilitakiwa kupumzishwa mwaka huo na kwa sababu fungu la kumi lilitakiwa kutokana na mazao yaliyopatikana katika ardhi basi mwaka huo hakuna myahudi alitoa fungu la kumi.
Haya yanafundisha kuwaibia watu kila uchwao. Basi wafuate torati ya Musa. Wanasema pale Kalvari yote yalikwisha lakini agizo la fungu la kumi wamelikumbatia bado.
Hakuna fundisho hilo kwenye maandiko ya agano jipya.