Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Fungu la kumi lilikuwepo kabla ya Torati ya Mussa.
Mwanzo 14
18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.
Yakobo naye alitoa fungu la kumi na hii ni kabla ya Torati.
Mwanzo 28
22 Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Katika Agano jipya Paulo anasisitiza kuhusu kutoa kwa makuhani wa Injili na akisisitizia kuwa Ibrahimu alimpa fungu la Kumi Melkizedeki
Waebrania 7
2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
Hao wote hawakutoa fungu la kumi kwa sheria kwani kipindi hiko sheria haikuwepo walikuwa katika kioondi cha dhamiri. Dhamiri zao ziliongozwa kwa upendo wa Mungu walimtolea Mungu fungu la kumi.
Hata sasa hatutoi fungu la kumi kwa kufuata torati ila tunatoa kwa Upendo wetu kwa Mungu.
NASHAURI: Nyie vijana mjitahidi kuwa wanyenyekevu kwenye utumishi Mungu anaowapa. Acheni ujuaji kwani mambo mengi hamjui.
Fungu la kumi wanapewa Makuhani.
Siku hizi kuna makuhani?
Kulingana na Sheria za Dini hasa kama ulivyonukuu Biblia, embu Tupe sifa kuu Tatu za Mambo au masharti ya mtu kuwa Kuhani.
Ili watu wajue hizo Zaka(fungu la kumi) wanatoa sehemu sahihi au Laa.
Nasifikiri unajua Biblia yote sio Sheria. Hivyo vifungu utakavyonukuu utatoa Aya za Sheria