Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Unajua maana ya kuhukumu? Kazi ya kuhukumu? Kuhukumu ni kutoa hitimisho la huyu asiende mbinguni na huyu aende. Ambayo ni kazi ya Mungu baba. Sasa Mimi Wala sijahukumu Bali nakataa huu ujinga wa baba yangu sijui nani.

Umeniuiza baba wa manabii wa kweli ni nani. Nikakwambia ni Yesu Kristo. Halafu unanihoji huyo Yesu Kristo ni wa kanisa gani na ministry gani.Hili swali ni mtu ambaye kwanza Hana msingi mzuri wa kumjua Kristo na kazi zake.

Ina maana naongea na mtu ambaye hata hajui anachouliza. Yesu Kristo ndio mwasisi wa kanisa, na ndiye aliyemtokea mtume Paulo na kumbadilisha na kuanza kumtumikia. Kwa hivyo kila nabii wa kweli lazima baba yake awe ni Yesu Kristo. Sio mtu anaamka asubuhi anadai baba yake ni TB Joshua.

Kasome Mathayo 23:9 inayokataza kuitana baba na ujinga mwingine. Kuna Mtume mmoja anaitwa Nabii Passion , aliasi akawa mnywa pombe, akawa shoga anavaa nguzo za kike na kuvaa mawigi, akawa dj kwenye ma club, ila bado anadai ana watoto wengi duniani. Juzi juzi ndio amerudi Tena kudanganya watu. Na Kama kawaida bado wapo wanaomuamini.
Uko sahihi. Lakini pia kuna inshu ya Paulo anasema tumfuate kama anavyomfuata kristo. Maana yake mtu akiacha kumfuata kristo tumuache pia. Wapo wengi walioanza vyema na kumaliza vibaya so hapo na sisi tuache ukristo kwa kuwa kiongozi wetu ameacha hapana. Ramani yetu mi biblia. Na alama yetu ni Yesu.
 
William Marrion Branham ndo no 1 kwangu.
Hata Uebert Angel anakiri kwamba Branham hakua mtu wa kawaida.
Huyu mwamba sana. Ingawa nilisikia kama alipata jaribu moja zito sana. Nafkiri nilisoma sehemu kama vile kifo cha mtoto au mke. Alikuwa anaombea watu waliokufa wanafufuka. Ila alivyokufa mmoja kati ya hao niliowataja hakuweza kumfufua. Aliomba sana na kufunga lakini wapi.
 
Wa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle

Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.

Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.

Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.

2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.

3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.

Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.

Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.

4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.

5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.

6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.

7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.

8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.

Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.

NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.

Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.

Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.

Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.

Karibu!!!

Katika hao wote mwalimu wako ni nani?
 
Jina la Yesu linawatajirisha watu.
Na wanatajirika haswa sio mchezo na wewe tumia jina la Yesu ujenge hekalu lako, uwe na domo tu la kubwabwaja na ujue kumeza vifungu vya Bibilia namaanisha Bibi Lia basi umewashika
 
Dr Myles Munroe (of blessed memory), kwangu he is the best of all times. Huyu jamaa ni viwango vya tofauti sana.

Kisha kuna Dr Mensah Otabil, Sam Adeyemi, TD Jakes, Creflo Dollar, Bishop David Oyedepo, Prophet Uebert Angel and Pastor Chris Oyakhilome.

Kuna hawa sio waalimu sana lakini ni fire kwelikweli: Pastor EA Adeboye, Johnson Suleiman, Joshua Selman na Dr Paul Enenche.

Tanzania ni Mwalimu Christopher Mwakasege.
 
Wa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle

Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.

Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.

Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.

2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.

3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.

Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.

Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.

4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.

5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.

6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.

7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.

8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.

Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.

NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.

Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.

Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.

Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.

Karibu!!!

Kuna kichwa kinaitwa Felician Makarios Phos ni hatari sana. Shule yake lazima uwe na akili timamu ndio utaelewa. Bibilia inawekwa wazi kama juanla mchana, hakuna mafumbo wala giza.

I highly recommend this man.

Ana channel yako telegram inaitwa Kainosmedia

Pitia hapo utanishukuru sana baadae
 
Kama wote hao unawasikiza unatoa wapi muda wa kufanya kazi mkuu? Sina Nia mbaya
Mimi namfahamu mark Finley (Nje)
Mwakasege Tz
David mbaga Tx sda hasa kwenye afya huyu jamaa namkubali sana.
 
Uebert Angel alinijibu swali ambalo niliwauliza watalaamu wa theologia wakatoa majibu ambayo sijawahi kuridhika ,huyu mwamba alifundisha "the origin of God ".Toka nikiwa mdogo nilikuwa nauliza Mungu alitoka wapi na anakaa wapi.Huyu mwamba alijibu haya maswali mawili nikanyanyua mikono juu .
Jazia nyama kidogo tujifunze alichojibu
 
huyo Uebert Angel, umepotea. mwalimu wenu pia ni mhubiri mzuri ila huwa hajui hata anachohubiri kwasababu hajawahi kuexperience wokovu wa kweli. the same kwa kimaro. mwenye kuelewa ameelewa.
Mwl Mwakasege hajaexperience wokovu, are you kidding?
 
Msikilize
Kwangu mimi mpaka sasa kwa hapa Tanzania ni hawa.
1. Mwalimu Christopher Mwakasege
2. Pastor Carlos Kirimbai

Jamaa wanaijua bible fresh, wanaisoma kila siku, na wanatamani kila mtu aisome Bible fresh na kuitambua. Yote kwa yote wanakufanya umjue Yesu at personal level bila kubabaishwa na chochote au yoyote.

Naambiwa walifanikiwa kuukwepa upepo wa kidini (kidhehebu) uliokuwa ukivuma vilivyo miaka ya 90, na wamefanikiwa pia kuuvuka huu upepo wa sasa wa tamaa za mali na umungu mtu unaotikisa kanisa la Tz kwa zaidi ya 80%.

Yote kwa yote jamaa wanaweza kukushawishi umjue Yesu na kuijua Bible fresh hata kama wewe sio mkristo au wewe ni mpagani.
Msikilize Emmanuel Makandiwa
 
hao hawana tofauti na waganga wa kienyeji. waganga wa kienyeji wamekuwa wakifanya hayo miaka nenda rudi.
Tena kwa kuongezea mganga wa kienyeji pia anaeza tabiria mtu mpaka mtoto jinsia yake mtu atakaejifungua na huyo mtoto wanajua atakuja na baraka gani..very interesting...

Mungu atusaidie sana kujua hawa manabii wanaoibuka kama uyoga..
 
Back
Top Bottom