Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa mkuu, ngoja nijaribu!GoldDhahabu kuna maswali hapo juu karibu useme chochote Akilibora
Mzee aliipiga Injili bwanaa, aliipiga Injili, yani alikua anahubiri mtu anaanza kulia mwenyewe anaiona jehanamu hii hapa.. akianza kuitafsiri Ufunuo. Huyu Mzee mwendo aliumaliza aiseee, kibinadamu naona kabisa hakubakiza alichopewa. Nimetafuta sana pia Cd zake imekua ngumu kuzipata. Huyu mzee alifunga mwaka mzima akiomba nguvu za kupiga Injili. Depal huna mzigo uliopewa wakufanya ufunge mwaka mzima?Binafsi watumishi wengi wa kiroho nawakubali,hasa wenye misimamo thabiti ya kiroho...lkn mtumishi wangu pendwa ni MAREHEMU DR MOSES KULOLA..huyu mtumishi hua nasikiliza sana injili yake...pia mwenye mikanda ya mahubiri ya huyu mzee niko tayari kuinunua tuwasiliane,natunza kumbukumbu yaweze nisaidia.
Unasinzia kwenye semina ya Mwakasege?😃Mwakasege ni Mtumishi wa Mungu haswa,nampenda sababu semina zake hazina udhehebu mule ndani mpka waislamu unawakuta.
ila nikienda semina ya mwakasege ndugu zangu NASINZIA,mahuburi ya vile binafsi siyawezi siwi Active napenda mahubiri ya nakshi nakshi ku refresh ubongo.
Kina Kimaro
Kina Mastai
Kina Mtokambali (TAG pastors wote)
Sina mtumishi mmoja wala favourite mimi yeyote mtoa Mawe nayapokea nayafanyia kazi.
Unaniuliza mimi?Samahani wewe ni Me/Ke .
Sure kwa Dini na imani tu umebobea professor wa Havard kabisa kwa huko
🙏🙏🙏Hujaja huku katoliki kila padre yupo NONDO
Mkuu, japo sina uthibitisho wa "kisayansi" kwamba watumishi wengi wanapenda kuheshimiwa kulikopitiliza, nitajaribu kujibu kwa kadiri ya uelewa wangu.Eti kuna jambo nimekuwa silielewi Naomba kusaidiwa,
Hivi ni kwa nini watumishi wengi wa bongo wanapenda kuheshimiwa kulikopitiliza Yaani kuogopwa na waumini?
Kwanini?
Inawezekana ni kwa sababu ya muda. Kuna wachache wanaotoa nafasi ya maswali kabla au baada ya mafundisho. Namfahamu mtumishi mmoja ambaye yeye wakati mwingine, kabla hajaanza kuhubiri, atauliza kwanza maswali au atatoka fursa ya kuulizwa maswali. Maswali ndiyo yatakayoamua somo litakalofundishwa siku hiyo.Halafu enzi za Yesu iliruhusiwa kuuliza maswali baada ya mahubiri siku hizi Mbona wahubiri hawatoi nafasi ya kuulizwa maswali na wafuasi wao?
Je Hawajiamini?
Je wanaona watachoreka na kuumbuka?
Soma na kitabu cha Historia ya maisha yake. Alikuwa mnyenyekevu sana. Unaambiwa hata Nyerere alikuwa akimheshimu. Ilikuwa ni kawaida ya Mwl Nyerere kupitia Mwanza kwa ajili ya kumsalimia Askofu Kulola alipokuwa akienda Musoma. Na alikuwa haendi mikono mitupu, alikuwa akimpelekea ng'ombe aliyekwishachinjwa kwa ajili ya mboga.Mzee aliipiga Injili bwanaa, dlipiga Injili, yani alikua aahubiri mtu anaanza kulia mwenyewe anaion jehanamu hii hapa.. akianza kuitafsiri Ufunuo. Huyu Mzee mwendo aliumaliza aiseee, kibinadamu naona kabisa hakubakiza alichopewa. Nimetafuta sana pia Cd zake imekua ngumu kuzipata. Huyu mzee alifunga mwaka mzima akiomba nguvu za kupiga Injili.
Kinaweza kupatikana sehemu gani hicho kitabu chake mkuu..Soma na kitabu cha Historia ya maisha yake. Alikuwa mnyenyekevu sana. Unaambiwa hata Nyerere alikuwa akimheshimu. Ilikuwa ni kawaida ya Mwl Nyerere, alipokuwa akienda Musoma apitie Mwanza kumsalimia Mzee Kulola. Na alikuwa haendi mikono mitupu, alikuwa akimpelekea ng'ombe aliyekwishachinjwa kwa ajili ya mboga.
Lakini pamoja na kuheshimiwa na viongozi wakubwa Serikalini, "hakuvimba" kichwa.
Bookshops zenye Vitabu vya Kikristo, au kwenye mikutano ya wahubiri "wakubwa" kama akina Mwakasege. Wauzaji wa vitabu huwa hawakai mbali na mikutano ya aina hiyo.Kinaweza kupatikana sehemu gani hicho kitabu chake mkuu..
Shukran sana mkuu.. nipo dar nitajitahidi kufatilia..Bookshops zenye Vitabu vya Kikristo, au kwenye mikutano ya wahubiri "wakubwa" kama akina Mwakasege. Wauzaji wa vitabu huwa hawakai mbali na mikutano ya aina hiyo.
Kwani uko wapi mkuu? Ukikosa, tafuta Namba za ofisi za EAGT wapigie uwaulize unakoweza kupata.
Au kama upo Dar, kakiulizie Kanisani kw Askofu Floran Katunzi. Na kama upo Mwanza, ulifika EAGT Bugando sidhani kama utakikosa. Lakini pia kwa Mwanza, unaweza kuangalia kwenye duka la SOMA BIBLIA lililopo Mabatini Mwanza.
👏👏👏✅🙏Shukran sana mkuu.. nipo dar nitajitahidi kufatilia..
Jaribu kuwasiliana na HOUSE OF WISDOM BOOKSHOP 0759349964, uwaulize kama wanacho, japo vitabu vyao vingi ni vya lugha ya English. Ndiko mara nyingi ninakochukulia vitabu vyangu vya kuvisoma. Jaribu, pengine huenda wakawa nacho.Shukran sana mkuu.. nipo dar nitajitahidi kufatilia..
Nashukuru zaidi mkuu.. kesho nikimaliza ratiba zangu nitawasiliana naoJaribu kuwasiliana na HOUSE OF WISDOM BOOKSHOP 0759349964, uwaulize kama wanacho, japo vitabu vyao vingi ni vya lugha ya English. Ndiko mara nyingi ninakochukulia vitabu vyangu vya kuvisoma. Jaribu, pengine huenda wakawa nacho.
Wapo Posta jijini Dar Es Salaam maeneo ya Samora Avenue.
Jaribu kuwasiliana nao hata kwa WhatsApp.
👏👏👏✅Nashukuru zaidi mkuu.. kesho nikimaliza ratiba zangu nitawasiliana nao