Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Eti kuna jambo nimekuwa silielewi Naomba kusaidiwa,

Hivi ni kwa nini watumishi wengi wa bongo wanapenda kuheshimiwa kulikopitiliza Yaani kuogopwa na waumini?

Kwanini?
 
Halafu enzi za Yesu iliruhusiwa kuuliza maswali baada ya mahubiri siku hizi Mbona wahubiri hawatoi nafasi ya kuulizwa maswali na wafuasi wao?

Je Hawajiamini?

Je wanaona watachoreka na kuumbuka?
 
Ambavyo hawaoni haya akifa Nabii Eti anamrithisha mkewe au mwanae uchungaji [emoji848][emoji848]

Hiyo yote ni ushahidi wa kutaka kuendeleza maslahi ya fedha na mali.

Makanisa na huduma za kifamilia [emoji848][emoji848]
 
Binafsi watumishi wengi wa kiroho nawakubali,hasa wenye misimamo thabiti ya kiroho...lkn mtumishi wangu pendwa ni MAREHEMU DR MOSES KULOLA..huyu mtumishi hua nasikiliza sana injili yake...pia mwenye mikanda ya mahubiri ya huyu mzee niko tayari kuinunua tuwasiliane,natunza kumbukumbu yaweze nisaidia.
Mzee aliipiga Injili bwanaa, aliipiga Injili, yani alikua anahubiri mtu anaanza kulia mwenyewe anaiona jehanamu hii hapa.. akianza kuitafsiri Ufunuo. Huyu Mzee mwendo aliumaliza aiseee, kibinadamu naona kabisa hakubakiza alichopewa. Nimetafuta sana pia Cd zake imekua ngumu kuzipata. Huyu mzee alifunga mwaka mzima akiomba nguvu za kupiga Injili. Depal huna mzigo uliopewa wakufanya ufunge mwaka mzima?
 
Mwakasege ni Mtumishi wa Mungu haswa,nampenda sababu semina zake hazina udhehebu mule ndani mpka waislamu unawakuta.

ila nikienda semina ya mwakasege ndugu zangu NASINZIA,mahuburi ya vile binafsi siyawezi siwi Active napenda mahubiri ya nakshi nakshi ku refresh ubongo.

Kina Kimaro
Kina Mastai
Kina Mtokambali (TAG pastors wote)

Sina mtumishi mmoja wala favourite mimi yeyote mtoa Mawe nayapokea nayafanyia kazi.
Unasinzia kwenye semina ya Mwakasege?😃

Kumbe watu tunatofautiana sana. Nafikiri, ni kila mtu na "ladha" yake anayoikubali. Ninapenda sana mafundisho.

Sivutiwi na mahubiri ya Kiinjilisti, labda yawe na miujiza!

Kati ya watumishi ambao huwa sichoki kuwasikiliza ni Mwakasege.
 
Samahani wewe ni Me/Ke .
Sure kwa Dini na imani tu umebobea professor wa Havard kabisa kwa huko
Unaniuliza mimi?

Kwa wiki nanyoa ndevu zaidi ya mara moja.

Kwa kuwa sijui umri wako, nakisia kuwa unaweza ukaniita jina mojawapo kati ya haya:

1. Mwanangu
2. Kijana wangu
3. Mdogo wangu
4. "Msela" au "mshikaji" wangu (ila hayo majina nilishayakataa tokea nikiwa Sekondari, maclassmate wangu walikuwa wakiniita kaka...)
5.Rafiki
6. Kaka
7. Baba

Mojawapo kati ya hayo, na si zaidi.
 
Kuna huyu wa radio kicheko anaitwa Mgisha Mtebe kama sijakosea
 
Eti kuna jambo nimekuwa silielewi Naomba kusaidiwa,

Hivi ni kwa nini watumishi wengi wa bongo wanapenda kuheshimiwa kulikopitiliza Yaani kuogopwa na waumini?

Kwanini?
Mkuu, japo sina uthibitisho wa "kisayansi" kwamba watumishi wengi wanapenda kuheshimiwa kulikopitiliza, nitajaribu kujibu kwa kadiri ya uelewa wangu.

Jambo la kwanza, watumishi nao ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Kuwa watumishi hakuwaondolei ubinadamu wao. Na kati ya kiu kubwa ya karibia kila binadamu kama siyo wote ni shauku ya kutambuliwa. Profesa mashuhuri wa SAIKOLOJIA toka Chuo Kikuu cha Harvard anasema, "The craving nature of the human being is the desire to be appreciated".

Pili, inategemeana na kiwango cha ukomavu au ukuaji wake wa kiroho. Ukomavu wa kiroho haupimwi kwa karama za Roho Mtakatifu zinazothihirika kwenye huduma ya mtumishi kama vile uponyaji, miujiza, n.k. Bali, kwa kiwango ambacho roho yake imeweza kuuthibiti mwili wake, sawasawa na Wagalatia 5:22.

Mtumishi ambaye roho yake inaitawala nafasi yake na mwili wake anaongozwa na upendo. Na kama anatawaliwa na upendo, lazima awe mnyenyekevu.
 
Halafu enzi za Yesu iliruhusiwa kuuliza maswali baada ya mahubiri siku hizi Mbona wahubiri hawatoi nafasi ya kuulizwa maswali na wafuasi wao?

Je Hawajiamini?

Je wanaona watachoreka na kuumbuka?
Inawezekana ni kwa sababu ya muda. Kuna wachache wanaotoa nafasi ya maswali kabla au baada ya mafundisho. Namfahamu mtumishi mmoja ambaye yeye wakati mwingine, kabla hajaanza kuhubiri, atauliza kwanza maswali au atatoka fursa ya kuulizwa maswali. Maswali ndiyo yatakayoamua somo litakalofundishwa siku hiyo.
 
Mzee aliipiga Injili bwanaa, dlipiga Injili, yani alikua aahubiri mtu anaanza kulia mwenyewe anaion jehanamu hii hapa.. akianza kuitafsiri Ufunuo. Huyu Mzee mwendo aliumaliza aiseee, kibinadamu naona kabisa hakubakiza alichopewa. Nimetafuta sana pia Cd zake imekua ngumu kuzipata. Huyu mzee alifunga mwaka mzima akiomba nguvu za kupiga Injili.
Soma na kitabu cha Historia ya maisha yake. Alikuwa mnyenyekevu sana. Unaambiwa hata Nyerere alikuwa akimheshimu. Ilikuwa ni kawaida ya Mwl Nyerere kupitia Mwanza kwa ajili ya kumsalimia Askofu Kulola alipokuwa akienda Musoma. Na alikuwa haendi mikono mitupu, alikuwa akimpelekea ng'ombe aliyekwishachinjwa kwa ajili ya mboga.

Lakini pamoja na kuheshimiwa na viongozi wakubwa Serikalini, "hakuvimba" kichwa.
 
Soma na kitabu cha Historia ya maisha yake. Alikuwa mnyenyekevu sana. Unaambiwa hata Nyerere alikuwa akimheshimu. Ilikuwa ni kawaida ya Mwl Nyerere, alipokuwa akienda Musoma apitie Mwanza kumsalimia Mzee Kulola. Na alikuwa haendi mikono mitupu, alikuwa akimpelekea ng'ombe aliyekwishachinjwa kwa ajili ya mboga.

Lakini pamoja na kuheshimiwa na viongozi wakubwa Serikalini, "hakuvimba" kichwa.
Kinaweza kupatikana sehemu gani hicho kitabu chake mkuu..
 
Kinaweza kupatikana sehemu gani hicho kitabu chake mkuu..
Bookshops zenye Vitabu vya Kikristo, au kwenye mikutano ya wahubiri "wakubwa" kama akina Mwakasege. Wauzaji wa vitabu huwa hawakai mbali na mikutano ya aina hiyo.

Kwani uko wapi mkuu? Ukikosa, tafuta Namba za ofisi za EAGT wapigie uwaulize unakoweza kupata.

Au kama upo Dar, kakiulizie Kanisani kw Askofu Floran Katunzi. Na kama upo Mwanza, ulifika EAGT Bugando sidhani kama utakikosa. Lakini pia kwa Mwanza, unaweza kuangalia kwenye duka la SOMA BIBLIA lililopo Mabatini Mwanza.
 
Shukran sana mkuu.. nipo dar nitajitahidi kufatilia..
 
Shukran sana mkuu.. nipo dar nitajitahidi kufatilia..
Jaribu kuwasiliana na HOUSE OF WISDOM BOOKSHOP 0759349964, uwaulize kama wanacho, japo vitabu vyao vingi ni vya lugha ya English. Ndiko mara nyingi ninakochukulia vitabu vyangu vya kuvisoma. Jaribu, pengine huenda wakawa nacho.

Wapo Posta jijini Dar Es Salaam maeneo ya Samora Avenue.

Jaribu kuwasiliana nao hata kwa WhatsApp.
 
Nashukuru zaidi mkuu.. kesho nikimaliza ratiba zangu nitawasiliana nao
 
Back
Top Bottom