Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Video moja inatembea mtandaoni kuanzia leo mchana, kinadada watatu wamejirekodi wakiongelea kwa uchungu namna walivyobaguliwa na kuletewa pozi na wafanya kazi wa mgahawa maarufu wa Fish Market.
Kwamba wateja wakija weusi na kinadada wanaletewa maringo ya kuchelewa kuhudumiwa, ya kuchelewa kusafishiwa viti vyao lakini meza ya wateja wazungu hata kama ni mmoja wapo miongoni mwa kundi la weusi wanachangamkiwa na kuhudumiwa haraka.
Ni video iliyorushwa na kinadada wakilalamika, hivyo hatujui kwa kina uhalali wa malalamiko yao, maana kinadada huwa wanaoneana sana wivu na kuumiza wao kwa wao.
Lakini kama hao wahudumu wa Fish Market wanaishiriki hiyo dhambi ya ubaguzi bila ya wao wenyewe kujua basi wanajitafutia laana zitakazokaa nao kwa miaka mingi ijayo. Huu ubaguzi wanaowafanyia weusi wenzao ndio huu huu tunaokutana nao tukiwa Ulaya na Marekani kwa wazungu.
Labda kinadada hawa hawajui madhara ya hicho wanachokifanya. Lakini ni hawa hawa wakiwa wanasota mitaani wakitafuta kazi wanakuwa wakitia sana huruma namna wanavyokuwa wachovu na mkono ukiwa shavuni.
Ubaguzi ni dhambi mbaya inayoumiza nafsi ya yule anayefanyiwa, mbaya zaidi ni kama hawa wahudumu wanajisahau wakiwachukulia poa wateja wanaowaona kwa mara ya kwanza.