Huku kwetu wali nazi 100 ukifika unakutana na tabasamu la Odo Mammi, hujakaa sawa unafuatwa na Chonge mrembo mweupe, hapo Saumu Mashauzi anakukonyeza kwa kukuminyia jicho, Miza nae anakuegemea bega anakuuliza utakula samaki wa kupwaza na maharage ya kukata au samaki makange Maarufu kama Samaki Makange Nuksi..... unaulizwa utakula na wali wa nazi ngapi 3, 6, 9 kbl hujajibu Mama mkubwa anajibu huyo anakulaga wali wa nazi 3, mwingine anadaki mchicha je unataka wa kuloweka kwa tui au wakulowekwa kwa maji ya madafu...
Njooni huku kwetu barabara ya 17 ali maarufu kwa jina la wali nazi 100 hutalalamika, unahudumiwa hadi unahisi kabisa unamlipa pesa pungufu. Mbarikiwe nyie kina mama hapo Barabara ya 17, nazunguzia Tanga hiyo wazeee, njooni!!!