Wafanyakazi na wanaojitolea zaidi ya elfu mbili wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing wamepiga picha ya pamoja ya ukumbusho tarehe 21 mwezi huu katika Uwanja wa Michezo wa Taifa mjini Beijing, China baada ya michezo hiyo kumalizika. Waliosimama kwenye barafu ni wahudumu waliofanya kazi katika eneo lililozingirwa na waliosimama kwenye stendi ya ghorofa ya pili ni waliofanya kazi nje ya eneo hilo. Wanafurahia kupiga picha wakifuata hatua za kukinga na virusi.