Imeshadhihirika kwa kila mtu kuwa Hersi ni mwiba mchungu sana kwasasa, na inaipaisha Yanga kwa muda mfupi sana. Hivyo namna pekee ya kuidondoaha Yanga nii kumuondoa Hersi Said. Wana Yanga wakiingia kwenye huu mtego watapoteana mazima maana hapa inatengenezwa migogoro na makundi.
Katiba ya Yanga ilipatikana kupitia mchakato mrefu uliongozwa na GSM kupitia huyo huyo Hersi Saidi kwa kufuata muongozo wa mfumo wa uendeshaji wa timu ulitolewa kwa msaada wa La Liga. Mpaka sasa Yanga sio jambo sahihi kwa Yanga kuitumia hiyo katiba kwasababu bado mchakato wa mabadiliko haujakamilika.
Hakuna wadhamini watatu, na pia mchakato wa
Yanga kuwa kampuni ado haujakamilika, n.k na uzuri Hersi aliwahi kuzungumzia huo mchakato na kama kuna mwana Yanga ana akili timamu ataelewa na atapata picha ni wapi huyu mtu anaikusudia kuipeleka Yanga. Ana mawazo na maono mazuri sana kiutendaji.
Yangu ni hayo tu