Wahusika: Tunaomba album ya nyimbo za ujio wa Baba Mtakatifu Yohanne II Septemba 1990 mtuwekee youtube

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
Kwa watumishi wa Mungu wanaohusika kwa namna yoyote ile;
Tunaomba Album hiyo iliyotoka mwaka 1990 baada ya ujio wa Baba Mtakatifu Yohanne Paul II, nyimbo zake mtuwekee kwenye youtube. We are terribly missing the album!

Kwa kipindi hiki kwenye youtube kuna wimbo mmoja tu wa album hiyo, ambao ni huu hapa chini

Tunatanguliza shukrani zetu,.
MUBARIKIWE NA BWANA
 
Mleta mada acha ubahili nenda kanunue usipende vya bure kanisani wakati sadaka yenyewe kuitoa mpaka utishiwe kuwa kanisa halitakupa huduma ndio unaitoa shingo upande
 
Naunga mkono hoja!

Wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu!
...... wala malango ya kuzimu hayatalishinda.

Halafu nadhani huo wimbo ndiyo uko namba moja; ndiyo ule ambao ni wa kwanza kwenye mpangilo wa nyimbo zilizo kwenye album hiyo
 
Mleta mada acha ubahili nenda kanunue usipende vya bure kanisani wakati sadaka yenyewe kuitoa mpaka utishiwe kuwa kanisa halitakupa huduma ndio unaitoa shingo upande
Siyo ubahili; ni muda. Kama utaratibu wao ni kwamba hawawezi kuziweka humu kwa sababu za kibiashara, nitajitahidi kupata muda nikanunue. Kwa sasa nina dhana kuwa pengine wamejisahau tu kuziweka na si kwa lengo la biasahara
 
Tumpokee kwa shangwe na herii, tumpokee papaa Yohane Paulo,
Mtumishi, kiongozi mchungaji wetu mwema wa kanisa katoliki.
Kuna binti wa nyumbani kwetu alikuwa anaimba kwenye kwaya hiyo. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwangu kumuona mtu wa nyumbani ninayemfahamu, akiwa amerekodiwa na kuonekana kwenye video
 
Kwa watumishi wa Mungu wanaohusika kwa namna yoyote ile;
Tunaomba Album hiyo iliyotoka mwaka 1990 baada ya ujio wa Baba Mtakatifu Yohanne Paul II, nyimbo zake mtuwekee kwenye youtube. We are terribly missing the album!

Kwa kipindi hiki kwenye youtube kuna wimbo mmoja tu wa album hiyo, ambao ni huu hapa chini

Tunatanguliza shukrani zetu,.
MUBARIKIWE NA BWANA
Hiyo album yenye nyimbo kama vile Utukufu na ukuu, Wewe ndiwe Petro, Bwana Mfalme ameketi milele, Nimemkuta Daudi, n.k. ninayo. Naitafuta ile nyingine yenye nyimbo za Tumpokee Kiongozi wetu na mchungaji wetu mwema, Tumpokee kwa shangwe, n.k.
 
Tumpokee kwa shangwe na herii, tumpokee papaa Yohane Paulo,
Mtumishi, kiongozi mchungaji wetu mwema wa kanisa katoliki.
Ukiipata hii album please tuwasiliane. Kuna wimbo mwingine unaimbwa "Waumini, tujiandae kwa ujio wa Papa wetu"
 
Hiyo album yenye nyimbo kama vile Utukufu na ukuu, Wewe ndiwe Petro, Bwana Mfalme ameketi milele, Nimemkuta Daudi, n.k. ninayo. Naitafuta ile nyingine yenye nyimbo za Tumpokee Kiongozi wetu na mchungaji wetu mwema, Tumpokee kwa shangwe, n.k.
Nimemkuta Daudi, mtumishi wanguuuuu nikampaka mafuta, ili mkono wangu uwe naye daima.
Hadi kufikia mwaka 2007 nilikuwa nazo zote sijui nani alikuja akzichomoa, hazipo tena. Naamini hadi leo RC hawajawahi kutoa Album yenye kuipiku album hii

Nenda St Joseph Cathedral zipo, mimi sijapata tu muda wa kwenda kuzichukua pale
 
Hiyo album yenye nyimbo kama vile Utukufu na ukuu, Wewe ndiwe Petro, Bwana Mfalme ameketi milele, Nimemkuta Daudi, n.k. ninayo. Naitafuta ile nyingine yenye nyimbo za Tumpokee Kiongozi wetu na mchungaji wetu mwema, Tumpokee kwa shangwe, n.k.
Baadhi ya nyimbo hizi nimezipta kwenye link hii hapa:

Walioziimba wanaitwa CATHOLIC MELODIES
 
Kwa watumishi wa Mungu wanaohusika kwa namna yoyote ile;
Tunaomba Album hiyo iliyotoka mwaka 1990 baada ya ujio wa Baba Mtakatifu Yohanne Paul II, nyimbo zake mtuwekee kwenye youtube. We are terribly missing the album!

Kwa kipindi hiki kwenye youtube kuna wimbo mmoja tu wa album hiyo, ambao ni huu hapa chini

Tunatanguliza shukrani zetu,.
MUBARIKIWE NA BWANA

Kwa watumishi wa Mungu wanaohusika kwa namna yoyote ile;
Tunaomba Album hiyo iliyotoka mwaka 1990 baada ya ujio wa Baba Mtakatifu Yohanne Paul II, nyimbo zake mtuwekee kwenye youtube. We are terribly missing the album!

Kwa kipindi hiki kwenye youtube kuna wimbo mmoja tu wa album hiyo, ambao ni huu hapa chini

Tunatanguliza shukrani zetu,.
MUBARIKIWE NA BWANA

Ninazo zote, ngoja niwawekee kwenye hii thread, zipo nyimbo 16, nyimbo 2 nimeshaziweka hapo juu.
 
Back
Top Bottom