Tatizo ni tabia yetu weusi kujiona wanyonge kupita kiasi...tatizo ni nini ? mnataka wazungu watuite weupe ? tuache ujinga....Huyo mzungu akikuita nyani na wewe si umuite nyani mweupe..? tofauti si rangi ya ngozi tu ?
Na kwa nini mtake weupe watusaidie eti kupigania haki zetu za kubaguliwa, kama wanavyofanya FIFA na wengine ?...huu ni upuuzi....
Just be happy people of colour...hakuna kitakachobadilika watuite au wasituite watakavyo.....
Mbona albino ni uzao wetu na bado tunawahesabu kama walemavu ? kama tatizo ni weupe nao si weupe ?...utaona ni udhalili kuitwa mweusi iwapo tu unatamani na kumuonea wivu aliye mweupe...na huu ni ujinga wa mwisho.
Tupambane duniani kwa mambo muhimu, kama sayansi na teknolojia, na kama yanatushinda bado tunamiliki urithi muhimu wa uumbaji wa dunia....mnahitaji thawabu gani zaidi ya rasilimali hizo tulizokabidhiwa na muumba.....wanyama, maliasili kibao ambazo hata kuzitunza zinatushinda, Tembo wanamalizwa tunakenua tuuu...mkiulizwa tatizo mtasema wazungu......
Mimi ninapokutana na mzungu na akaonyesha dalili ya kunibagua..huwa namwambia tu kimoyomoyo kuwa siku akiutambua ukweli atarudi na kuniabudu....
kwa mfano NUHU wa safina, anayeongelewa na vitabu vya kale, sio wengi watakubali kuwa alikuwa mweusi...na ndio maana hadi leo asilimia tisini ya wanyama walionusurika na gharika wanaishi afrika (mother land)
Hata ukifanya hesabu ya binaadamu walio/wanaofanya vizuri kwenye upande wa uwezo/vipaji vya asili (talents) ni weusi....ukianzia kwenye kandanda (Pele), boxing (Mohamed ally), music (Michael Jackson), kujenga safina (Nuhu), tenis (seren), Golf (Tiger woods).........