Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Pole nyingi sana kwake. Pengine alijisahau enzi hizo. Mungu amrehemu na kumfungulia mlango apate kufanikiwa.
 
Kama Yesu na baadae mitume walitumia kwanini wewe uone tatizo wakristo wa leo wakiyatumia?
 
List imekaa poa vibaya mno, ila kuna ambao hawakutakiwa kuwepo kabisa kama joel lwaga, paul clement, Goodluck nk, kama kuna vigezo ulitumia ili kuwaondoa kina rose muhando basi na hawa ulitakiwa uwatoe kabisa.
 
List imekaa poa vibaya mno, ila kuna ambao hawakutakiwa kuwepo kabisa kama joel lwaga, paul clement, Goodluck nk, kama kuna vigezo ulitumia ili kuwaondoa kina rose muhando basi na hawa ulitakiwa uwatoe kabisa.
Asante mkuu.

Vigezo vipi vilivyotajwa hapo vitawaondoa Lwaga na Clement?
 
Mkuu Biblia ipi imeruhusu wanaoachana wana weza oana tena?Math 19:9,imesema anayeacha na kuachwa akioa au kuolewa azini.
 
Sio vizuri kuwataja kwa majina,lakini fuatilia hao waimbaji baadhi uliowataja kama wako na ndoa zao za mwanzo,...Yuko mwimbaji mmoja nimemtaja hapo mkewe alimwacha na huyo mwimbaji makanisa ya kiroho yalikataa kumpa ruhusa ya kuoa...na ndio maana tunasisitiziwa kuomba ili Mungu atupe wa kufanana,lkn ukikosea kuoa au kuolewa hilo jaribu ni kubwa na inaweza kua ngumu sana kumuona Mungu...ni.Mungu tu aingilie kati kama ilivyokua kwa Ruthu.
 
Mkuu Biblia ipi imeruhusu wanaoachana wana weza oana tena?Math 19:9,imesema anayeacha na kuachwa akioa au kuolewa azini.
Huu mstari unauelewaje?

Mathayo 5:32 SRUV
lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
 
Ongeza kigezo kingine kuwa waimbaji kutoka Makanisa ya Kiprotestant, maana ukilinganisha na waimbaji wa Kanisa Katoliki kuna vichwa hatari sana kwa utunzi na uimbaji hao uliowataja wanasubiri mbali sana.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Lakini biblia inaruhusu kuacha na kuoa mwingine kwenye jambo moja tu, iwapo mtu ni mzinzi. Sasa hatujui utaratibu wa hilo kanisa.

Mimi kanisani ninaposali hairuhusiwi kuacha na kuoa mwingine kwasababu yoyote ingawa mimi naona clearly biblia haijazuia endapo mtu ni mzinzi.

Na mzinzi hapa ni hasa pale mtu anaporudia hiyo tabia na wala habadiliki.
 
Walete hapa hao wakatoliki ili tuwafahamu na pengine wanaweza kuingia hapo kwenye list.
 
Taja pia na kwaya bora za muda wote.
 
Huyu Fanuel Sedekia nilimjua kwa mara ya kwanza kwa kusikia nyimbo yake ikipigwa kwenye msiba wa classmate kipindi hiki tupo university.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…