Waimbaji kumi bora wa nyimbo za injili kuwahi kutokea hapa Tanzania mpaka sasa

Aliyoyapitia hayatupi sisi uhalali wa kum'judge..

Kila mtu ana mapito yake...tunaanguka ila Neema ya Mungu inatunyanyua tena....

Kwanza umeshausikiliza au kuuona wimbo wake wa 'Simba'? She is back like nothing happened.
Hawa majamaa wana matatizo sana.

Wao ni kina nani mpaka waweke standards za kupima morality ya watu.

Huku ni kujiona watakatifu
 
Albam ya Jipange sawasawa kuna ule wimbo Amina hatari....Mtoa mada wewe ni nan mpaka uanze kuwahesabia watu dhambi kwamba unasema Rose mhando sio mcha Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni muhimu sana kupima kazi ya mtu, huduma na ushuhuda. Hakuna mahali pataweza kudumu bila kusimamia misingi.

Huwezi kutangaza mtu kuwa ni mfano wa kuigwa kwenye jamii fulani ikiwa publicly anajulikana hafuati maadili ya jamii hiyo.

Huu ndio msingi wa kuwaondoa baadhi yao. Ni maombi yetu kwa Mungu kwamba watasimama tena na kurudia zile nafasi za mwanzoni.
 
Faustine Munishi...huyu anaimba real gospel
 
Kwa vigezo hivi unavyotaja lazima aongoze yeye. Hakuna wa kukupinga. Hapa tumewapima kwa vigezo tajwa hapo juu.
 
Kama ni kweli hawajui waimbaji hawa,bandiko lake linakosa uhalali.
Ni muhimu awafahamu kwa
kina waimbaji mashuhuri&maarufu,ili aweze kuweka fair judgement.
 
Haujistulkii kila mtu anamtaja Rose.

Mnyonge Mnyongeni , ila hakuna wa kushindana nae hapo.
Umesoma vigezo pale juu? Unaweza kuleta list nyingine kwa vigezo vingine mkuu. Wala hakuna kulazimisha chochote.
 
Sijawahi kumsikia.. ajitahidi sasa na neema ya Mungu imsaidie afikie viwango vya kitaifa.
Hujawahi msikia labda kwa sababu ya umri wako,kuna waimbaji wengi wazuri,Jangalason,Mzungu four japo kwa sasa nafikiri yuko busy na kuchunga zaidi...huyu mzungu 4 miaka ya 90 mwishoni nyimbo zake ilikua lazima ufufuke kiroho.
 
Kwa vigezo hivi unavyotaja lazima aongoze yeye. Hakuna wa kukupinga. Hapa tumewapima kwa vigezo tajwa hapo juu.
Vigezo ulivyoweka hapo juu vinatakiwa vitumiwe na Mungu sio wewe mwanadamu.

We unajuaje mtu ana imani thabiti au la ?

We umekuwa Mungu mpaka uthibitishe imani ya mwanadamu mwenzako ?
 
Hawa majamaa wana matatizo sana.

Wao ni kina nani mpaka waweke standards za kupima morality ya watu.

Huku ni kujiona watakatifu
Standard ya morality na christian ethics ipo kwenye biblia. Neno la Mungu linaturuhusu kupima mambo yote.
 
Mwansasu yupo kwenye list ya pili pale maana namfahamu sana.. ila huyo Jangalason hajafikia level ya kitaifa.

Kumbuka hapa hatupimi kipawa, tunapima namna alivyoweza kukua kwenye kipawa na kugusa watu wengi nchini.
Wewe humfahamu Jangalasoni...huyu ni mtumishi wa Mungu ambaye ameimba ktk upako kwa miaka mingi kabla hajaondoka nchini,kizazi cha miaka ya 80' mpk 90' +2000 mwanzon kinamjua vzr
 
Kama ni kweli hawajui waimbaji hawa,bandiko lake linakosa uhalali.
Ni muhimu awafahamu kwa
kina waimbaji mashuhuri&maarufu,ili aweze kuweka fair judgement.
Hapa tumeangalia mwimbaji mmoja mmoja na sio vikundi. Mwansasu yupo pale kwenye list ya pili ametajwa. Huyo mwingine hajawahi kufikia viwango vya kitaifa.
 
Hujawahi msikia labda kwa sababu ya umri wako,kuna waimbaji wengi wazuri,Jangalason,Mzungu four japo kwa sasa nafikiri yuko busy na kuchunga zaidi...huyu mzungu 4 miaka ya 90 mwishoni nyimbo zake ilikua lazima ufufuke kiroho.
Sijui ilikuwaje kwamba sikuwahi kuwasikia hao miaka ile ingawa nilikuwa mfuatiliaji sana.
 
Vigezo ulivyoweka hapo juu vinatakiwa vitumiwe na Mungu sio wewe mwanadamu.

We unajuaje mtu ana imani thabiti au la ?

We umekuwa Mungu mpaka uthibitishe imani ya mwanadamu mwenzako ?
Biblia inasema mtawatambua kwa matendo yao. Sasa hapa hatuhukumu mtu yeyote maana kila mtu anakosea na kutubu.

Hapa tunazingumzia ubora wa kazi na ushuhuda kwa kuzingatia maadili ya kikristo kwa tunavyoona public life.

Huwezi kutangaza mtu kuwa ni mfano wa kuigwa kwenye jamii fulani ikiwa publicly anajulikana hafuati maadili ya jamii hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…