Waimbaji wa Nyimbo za Dini za Zamani Walikuwa na Ujumbe Zaidi Kuliko Sasa

Mchana unaweka albamu ya nyimbo za Tabata Mennonite Choir na usiku mkiwa mnakula unasikiliza nyimbo za Mtoni Evangelical Choir na sauti ya kipekee ya Marehemu George Njabili.
Huyu njabili ndo yule kibonge aliyeimba around the corner, jesus is coming..? Alizikwa tukuyu
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu! Marehemu Mama Mkubwa alikuwa ni vocalist sauti ya kwanza kwenye kwaya ya Muungano Kwaya Christian Nasa Magu ๐Ÿ˜” yaani walikuwa wanasoma biblia halafu ndo wanatengeneza wimbo kutoka humo ๐Ÿ˜Š safi sana
Ulokole (wokovu)wa zamani ulikua wokovu kweli kweli, mtu akitengwa na kanisa anaona ametengwa na Mungu na vilio juu, siku hizi ni kanyaga twende ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€
 
Wewe sema tu zamani walilenga zaidi injiri siku hizi ni uwanja wa majungu, vijembe na tambo na zaidi sana vibunda. Au unawaogopa Mkuu?
 
EAGT Utemini Gospel Singers (UGS)Singida, KILA GOTI LITAPIGWA ilishasambaratika, waimbaji wake wengine wanaimba kwa kujitegemea kama Elineema Babu, Sarah Nkumbi ambaye pia ni daktari wa binadamu ni mtumishi wa umma, kuna Emanuel Enock yeye ni producer mwenye studio yake, waimbaji wengine walijiunga na kwaya zingine
 
Sijawahi kuwaamini au kuwatilia maanani waimbaji wa nyimbo za dini hata siku moja na sitokuja kubadilika juu ya hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ