Wairan washangilia Marekani kuifunga timu yao

Axel Lloyd

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
4,170
Reaction score
9,500
Aiseee hili litakua ni ajabu la Tisa la Dunia.

Wairan washangilia timu Yao kufungwa na Marekani kwenye michuano ya kombe la Dunia, wengine waonyesha bendera ya Marekani na kuimba "Marekani, tuko nyuma yako".

Nini kimefanya mpaka wamefika hapa, bado nipo kwenye mshangao!
 
Kumuua mtu kisa hajafunika kichwa ni imani za kijinga sana. Inaonekana wairan wamechoka.

Mbona Qatar wanaiman yao lkn haijafikia hatua ya kuua mtu.

Pale Zanzibar kipindi cha Ramadhan wanatembea na fimbo kuchapa watu wanaokula.
 
Hili ni kweli ama
 
Hili ni kweli ama
Chanzo cha vurugu yote Iran ni baada ya mwanamke mmoja kukamatwa na askari akiwa hajafunika kichwa.
Baada ya kumkamata wakamuua, wanawake na baadhi ya wanaume wakasema hii haiwezekani.
Wakaanza maandamo huku baadhi ya wanawake wakiwa vichwa wazi, wakahukumiwa tena kifo wanawake 6.
Vurugu likapamba moto maandamo kila kona mpk leo hii.
 
Kumuua mtu kisa hajafunika kichwa ni imani za kijinga sana. Inaonekana wairan wamechoka.

Mbona Qatar wanaiman yao lkn haijafikia hatua ya kuua mtu.

Pale Zanzibar kipindi cha Ramadhan wanatembea na fimbo kuchapa watu wanaokula.
Unajuaa maana ya neno "ujinga"?
 
Chanzo cha vurugu yote Iran ni baada ya mwanamke mmoja kukamatwa na askari akiwa hajafunika kichwa.
Baada ya kumkamata wakamuua, wanawake na baadhi ya wanaume wakasema hii haiwezekani.
Wakaanza maandamo huku baadhi ya wanawake wakiwa vichwa wazi, wakahukumiwa tena kifo wanawake 6.
Vurugu likapamba moto maandamo kila kona mpk leo hii.
Wale wamezidisha chumvi, hakuna mahali dini imesema atakaekaa kichwa wazi auwawe, nadhani ndio maana huko qatar hakuna hizo kesi.

Mie nijuacho tumeambiwa tusilazimishane katika dini, we toa elimu tembea atakaetaka kufata atafata asiyetaka aache, tutajuana kesho kwa mungu.

Hawa wanaifanya dini ionekane kama gunia la miba,
Ameambiwa mwanamke ajistiri ila sijasoma sehemu kuwa asipojistiri auawe.
 
Zanzibar ukitafuna pipi mwezi wa ramadhani bakora za mgongo zinakuhusu
 
Back
Top Bottom