Waislam tulio wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji n.k

Waislam tulio wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji n.k

Assalaam alaykum,

Leo bhana wakati nimemaliza kuftari na kushiba basi yakawa yanakuja mawazo kedekede kuhusu mafundisho ya dini....

Nimetafakari nimeona waislam wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji, kuliko kamari na kadhalika! Kitu ambacho binafsi nimegundua sio sahihi kabisa, TUNAKOSEA MNO, hiki ni kiumbe cha Allah mtukufu, na hajatuamrisha tukichukie!

Hiki kiumbe kama vilivyo viumbe vingine kinaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa jamii yetu, "sasaiv" nasikia unaweza kuungwa mguu wake kama wako umekatika🥴 hivyo basi nawasii mno MSIMCHUKIE HANA HATIA KABISA!

Nb:-Allah mtukufu kaharamisha nyama ya nguruwe kuliwa na muumini., kama alivyoharamisha DAMU, NYAMAFU, KAMARI NA ZINAA🙂

Nimeambatanisha na picha ya KIUMBE CHA ALLAH MTUKUFU, kikiwa kimepozi kinakuangalia kwa huruma wewe unaekipiga rungu na kukiua, na wewe unaekichukia bila elimu..! Asanteni kwa kuja🤝

Na sisi
 
Mimi ni Mkristo ila Huwa nashindwa kumtetea mdudu ,dhidi ya kaazo la Agano la Kale! Mwisho wa siku nyama ile.ni tamu ,kama ni dhambi ,tunafanya ngapi!
 
Kwa mujibu wa Biblia Mzoga wa Ngombe Sio Najisi..
Kuna Tofauti kati ya Uchafu na Najisi..
Soma Post #10!

Kwa mujibu wa quran mizoga yote ni najis isipokuwa wa samaki, nzige na mwanaadamu!

Kwa mujibu wa Biblia Mzoga wa Ngombe Sio Najisi..
Kuna Tofauti kati ya Uchafu na Najisi..
Soma Post #10
Anhaa kumbe! Asante sana mkuu! Sasa kwa mujibu wa quran mizoga yote ni najis isipokuwa wa nzige, samaki na binaadamu!
Nb:- Najisi ni Uchafu, uchafu huu waweza kuwa hauonekani, kwa maana wa kiroho zaidi! UCHAFU ambao unaweza kukuzuia kufanya baadhi ya ibada! 🙂
 
Allah na mtume wake waliona mbali sana, walijua tukiruhusu kila ale huyu kiumbe ,,atatoweka duniani,
Imagine angekuwa analiwa na waarabu daaah,
Hivi kati ya ng'ombe na nguruwe yupi analika sana!? Yupi ambae wapo wengi kuliko wenzie!?
Halafu shangaa sasa Ng'ombe anabeba mimba miezi tisa na anaza mtoto mmoja tu🙂
Ngubi anabeba mimba miezi minne na anazaa watoto 12....lakini shangaa anazidiwa wingi na Ng'ombe hujiulizi wala hushangai!? 🙂🙂🙂🙂
 
Wa alaykum salaam,

Umetafakari jambo la msingi sana. Mara nyingi, hisia za watu kuhusu vitu vilivyoharamishwa zinaweza kuathiriwa na malezi na mitazamo ya kijamii badala ya kufuata mizani sahihi ya dini.

Katika Uislamu, nguruwe si adui, bali ni kiumbe wa Allah aliyekatazwa kwa matumizi ya chakula kwa waumini. Kama ulivyosema, haramu si nguruwe peke yake—damu, mizoga, kamari, zinaa, na mengineyo pia ni haramu, lakini mara nyingi watu hukazia sana baadhi ya mambo huku wakapuuza mengine.

Muhimu zaidi ni kuelewa kuwa uislamu haukufundisha kuchukia wanyama, bali umetufundisha kuwa na huruma kwa viumbe vyote vya Allah. Mtume Muhammad (SAW) aliwahimiza Waislamu kuwa na huruma hata kwa wanyama, akitufundisha kuwahudumia kwa upole na kutowadhulumu.

Kwa hiyo, mtazamo wako unahimiza usawa katika kufahamu dini—tusihamasishe chuki isiyo na msingi kwa nguruwe, lakini pia tuelewe mipaka ya halali na haramu kama ilivyoelekezwa katika Qur'an na Sunnah.

Jazaka Allahu khayran kwa tafakuri yako yenye manufaa!
 
Waislam wanapiga vita nguruwe sio kwasababu wanafuta tu maandiko ila ni njia yao ya kuwaonyesha imani zingine kuwa wao ni bora zaidi.

Sababu fikiria, mtu anaweza kula nguruwe hata miaka 10 na hayo madhara wanayosema yasionekane. Ila fanya zinaa mwaka tu lazima utakutana na balaa aidha la magonjwa,au fumanizi,au kujishushia heshima
 
Assalaam alaykum,

Leo bhana wakati nimemaliza kuftari na kushiba basi yakawa yanakuja mawazo kedekede kuhusu mafundisho ya dini....

Nimetafakari nimeona waislam wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji, kuliko kamari na kadhalika! Kitu ambacho binafsi nimegundua sio sahihi kabisa, TUNAKOSEA MNO, hiki ni kiumbe cha Allah mtukufu, na hajatuamrisha tukichukie!

Hiki kiumbe kama vilivyo viumbe vingine kinaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa jamii yetu, "sasaiv" nasikia unaweza kuungwa mguu wake kama wako umekatika🥴 hivyo basi nawasii mno MSIMCHUKIE HANA HATIA KABISA!

Nb:-Allah mtukufu kaharamisha nyama ya nguruwe kuliwa na muumini., kama alivyoharamisha DAMU, NYAMAFU, KAMARI NA ZINAA🙂

Nimeambatanisha na picha ya KIUMBE CHA ALLAH MTUKUFU, kikiwa kimepozi kinakuangalia kwa huruma wewe unaekipiga rungu na kukiua, na wewe unaekichukia bila elimu..! Asanteni kwa kuja🤝

kwa hiyo hapa ndo unatuambiaje ndugu yangu? maana kama vile sijakupa uzuri hivi
 
Back
Top Bottom