Waislam tulio wengi wetu tunamchukia nguruwe kuliko zinaa, kuliko pombe, kuliko usengenyaji n.k

Na sisi
 
Mimi ni Mkristo ila Huwa nashindwa kumtetea mdudu ,dhidi ya kaazo la Agano la Kale! Mwisho wa siku nyama ile.ni tamu ,kama ni dhambi ,tunafanya ngapi!
 
Kwa mujibu wa Biblia Mzoga wa Ngombe Sio Najisi..
Kuna Tofauti kati ya Uchafu na Najisi..
Soma Post #10!

Kwa mujibu wa quran mizoga yote ni najis isipokuwa wa samaki, nzige na mwanaadamu!

Kwa mujibu wa Biblia Mzoga wa Ngombe Sio Najisi..
Kuna Tofauti kati ya Uchafu na Najisi..
Soma Post #10
Anhaa kumbe! Asante sana mkuu! Sasa kwa mujibu wa quran mizoga yote ni najis isipokuwa wa nzige, samaki na binaadamu!
Nb:- Najisi ni Uchafu, uchafu huu waweza kuwa hauonekani, kwa maana wa kiroho zaidi! UCHAFU ambao unaweza kukuzuia kufanya baadhi ya ibada! 🙂
 
Allah na mtume wake waliona mbali sana, walijua tukiruhusu kila ale huyu kiumbe ,,atatoweka duniani,
Imagine angekuwa analiwa na waarabu daaah,
Hivi kati ya ng'ombe na nguruwe yupi analika sana!? Yupi ambae wapo wengi kuliko wenzie!?
Halafu shangaa sasa Ng'ombe anabeba mimba miezi tisa na anaza mtoto mmoja tu🙂
Ngubi anabeba mimba miezi minne na anazaa watoto 12....lakini shangaa anazidiwa wingi na Ng'ombe hujiulizi wala hushangai!? 🙂🙂🙂🙂
 
Wa alaykum salaam,

Umetafakari jambo la msingi sana. Mara nyingi, hisia za watu kuhusu vitu vilivyoharamishwa zinaweza kuathiriwa na malezi na mitazamo ya kijamii badala ya kufuata mizani sahihi ya dini.

Katika Uislamu, nguruwe si adui, bali ni kiumbe wa Allah aliyekatazwa kwa matumizi ya chakula kwa waumini. Kama ulivyosema, haramu si nguruwe peke yake—damu, mizoga, kamari, zinaa, na mengineyo pia ni haramu, lakini mara nyingi watu hukazia sana baadhi ya mambo huku wakapuuza mengine.

Muhimu zaidi ni kuelewa kuwa uislamu haukufundisha kuchukia wanyama, bali umetufundisha kuwa na huruma kwa viumbe vyote vya Allah. Mtume Muhammad (SAW) aliwahimiza Waislamu kuwa na huruma hata kwa wanyama, akitufundisha kuwahudumia kwa upole na kutowadhulumu.

Kwa hiyo, mtazamo wako unahimiza usawa katika kufahamu dini—tusihamasishe chuki isiyo na msingi kwa nguruwe, lakini pia tuelewe mipaka ya halali na haramu kama ilivyoelekezwa katika Qur'an na Sunnah.

Jazaka Allahu khayran kwa tafakuri yako yenye manufaa!
 
Wanapokuwa wanatumia hiyo huwa hawakai kwa amani hofu na uoga wa kuonwa hivyo waswahili wanasema kiti kinakuwa cha 🔥, hivyo ikaitwa kitimoto.
Sasa mtu mpaka kaamua kwenda huko kukaa kwa nini aogope tena!?
 
Waislam wanapiga vita nguruwe sio kwasababu wanafuta tu maandiko ila ni njia yao ya kuwaonyesha imani zingine kuwa wao ni bora zaidi.

Sababu fikiria, mtu anaweza kula nguruwe hata miaka 10 na hayo madhara wanayosema yasionekane. Ila fanya zinaa mwaka tu lazima utakutana na balaa aidha la magonjwa,au fumanizi,au kujishushia heshima
 
kwa hiyo hapa ndo unatuambiaje ndugu yangu? maana kama vile sijakupa uzuri hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…