Waislam tumedanganywa kwa miaka mingi sana. Tuamke, tufanye siasa misikitini na popote pale

Status
Not open for further replies.
lkn bosi wenu rwanda siyo Muislamu kwanza will never allow islam …
 
Kumekucha..
Kabisa. Tunaanza kuliona jua.

Waislam tusiuonee haya Uislam wetu. Tuwe mstari wa mbele kwenye siasa na nyanja zingine zote, tunazimwa uwezo wetu na fikra kwa makusudi kabisa.

Tumepewa dawa za usingizi kisaikolojia (Brainwashed) kwa muda mrefu sana, tuziteme.

Uislam hautukatazi kufanya siasà, tena za amani kabisa bila matusi wala kejeli.

Wanasiasa wakubwa wakihistoria duniani ambao siyo Waislam walitumia Uislam kufanya siasa zao na wakafanikiwa sana.

Wasomeni Walioiunda USA. Mfano Thomas Jafferson. Alitumia Qur'an na mafunzo ya Mtume Muhammad (saw) kufanya siasa zake.

Ushahidi: Thomas Jefferson and the Covenants of the Prophet Muhammad - Maydan

Sisi Waislam wa Tanzania ambao wazee wetu walikuwa mstari wa mbele, kuliko wa imani yeyote ile, kudai uhuru, kwanini leo hii tusiingie kwenye siasa kwa Uislam wetu na kutumia majukwaa yetu, misikiti yetu na masheikh wetu kuhamasishana?

Tuteme dozi ya usingizi Waislam, tuamke.
 
Duuh umetibuliwa!
 
Nadhani kuna haja ya kuufutilia mbali na huu utaaribu wa kubadilishana Rais muislamu na mkristo tuangalie uwezo tu .
Haya mambo ya waislamu kulalamika kwamba wanaonewa huibuka zaidi kipindi ambacho muislam anaongoza...inashangaza sana!
 
Nani anayewazima uwezo wenu wa kifikra zaidi yenu wenyewe?

Wewe mwenyewe unayejisifu umeamka bado uko usingizini, tena usingizi wa pono, mnataka kufanya siasa, tena unajisifu kwa lugha nzuri!, huko kote mnaendelea kuwekeza kwenye midomo tu, hiyo USA haikujengwa kwa midomo!.

Wakati wenzenu wanatenda, nyie mnapigana kuwekeza kwa nguvu midomoni, matokeo yake wakati wenzenu wako mbele kiutendaji, nyie kwa midomo yenu mliyowekeza miaka yote, mnaanza kutafuta namna ya kuwashusha ili wafanane nanyi, jambo ambalo haliwezekani.

Amka wewe bibi, bado umelala mpaka sasa, ningekuona wa maana kama ungewashawishi waislamu wenzako muanze kujenga taasisi zenu kama mashule na hospitali, kwa jasho lenu, ili muisaidie jamii ya kitanganyika, lakini ajabu ndio kwanza unakusanya nguvu kuwekeza kwenye midomo..
 
Kwa ufupi siasa mnazifanya sana. Japo za kwenu ndo zile za KIBITI
 
Mbona wapo waislamu wasomi wengi tu! Ila shida bado ipo palepale tu. Hawaitumii elimu Dunia ili wawe independent. Dini bado inawapunguzia wigo wa kujitambua ktk maswala muhimh sana ya kidunia. Hiyo confusion inawafelisha sana sana.
 
Wakristo na waislamu ni washindani,roughs hazikosekani,badala ya kulialia wapambane
 
Mmeambiwa Mswali mara 50 kila siku na Allah wenu.. mkaweka siasa mkawa mnaswali mara tano na pia mnakwepa, sasa siasa mtafanya saa ngapi? Chagueni Salah au Siasa
 
Mbona wapo waislamu wasomi wengi tu! Ila shida bado ipo palepale tu. Hawaitumii elimu Dunia ili wawe independent. Dini bado inawapunguzia wigo wa kujitambua ktk maswala muhimh sana ya kidunia. Hiyo confusion inawafelisha sana sana.
Kwahio unawashauri waislamu waachane na kusoma dini yao?. Hapo ndio utofauti wa wagalatia nawaislamu ulipo. Mmoja dini kwake nimuhimu mwingine dini kwake ni Bonasi.
 
Kwa ufupi siasa mnazifanya sana. Japo za kwenu ndo zile za KIBITI
Hapana. Tanganyika tulifanya siasa za amani katika kudai uhuru na mpaka sasa tunafanya na tutaendelea fanya siasa za amani.

Tunataka vijana wa Kiislam waamke wagombanie nafasi zote, kuanzia ujumbe wa nyumba kumi kupanda juu.
 
Inaonekana hoja ya Mkataba wa Bandari imekukalia vibaya.

Lakini pia huenda unamchulia kiaina Rais Samia
 
Marko. 12:17

Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana.

YESU ALIMALIZA YOTE.
USICHANGANYE SIASA NA DINI.

IRP BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE
 
Ni kula Ubwabwa tu
 
Ni lini Waislamu mliacha kufanya siasa msikitini ? Hadi zile ndogo ndogo kabisaa za uchaguzi wa viongozi vyuoni ni hivyo hivyo.
Kitu cha achabu ni kuwa Rais akiwa Mwislamu ndio mnalia lia vizuri kuweni makini. Wakristu huwa tunajiuliza swali moja tu
Rais akiwa Mkristu hakuna anachoniletea kwenye familia yangu hali kadhalika akiwa Mwislamu. Hivyo ninaangalia anayofanya sio kumuonea huruma.
Kipindi cha Magu Waislamu mlikaa kimyaa waliokuwa wanaongea ni hawa
Askofu Mwamakula
Askofu Niwemugizi
Askofu Bagonza
Tundu Lissu
Sheikh Ponda
Zitto Kabwe n.k na wala hakuna siku maaskofu walisimama kutoa msimamo wa kanisa kuwa Magufuli anaonewa.
Leo akina Sheikh Ponda na Zito Kabwe wako kimyaa kwa kuwa ni Mwislamu mwenzao.
Angalizo:Rais akikosea haijalishi dini yake,maumivu yatakuja kwa watanzania wote.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…