Mimi sio Mkatoliki, papa kwangu ni mwanadamu yeyote sawa tu na Diamond, harmonize na wewe na wengine wote, na ninaamini ukatoliki ni upagani kama ulivyo uislam tu. labda tuanzie hapo. shida moja kwa waislam huwa wanaamini wakristo wote ni wakatoliki, sisi wengine kwenye hilo kanisa huwa tunaenda tu wakati wa misiba tunaposhirikiana na majirani kwenye mambo kama hayo.
kama umeona leo pale uwanja wa Taifa, ulijaa walokole wa dhehebu moja tu, la TAG, hao wote waliojaa pale sio wakatoliki na hawataki hata kuusikia. wengine walijaa kule kwa mwamposa, wale sio walokole ni wafuasi wa mpiga dili mwamposa, nao ni dhehebu lingine, wengine ni walutheran nao watakuja kujaa hapo taifa muda si mrefu, wengine waanglican, wengine wamorovian, wengien walokole wa makanisa ya pentecost ambao pia ni wengi. hivyo usimwone kila mkristo ni mkatoliki. kwangu ukatoliki na uislam mpo kwenye kapu moja, nyote mnaelekea kwenye moto wa jehanum kwa kukataa kuokoka na kumpa Yesu Maisha yenu ayaokoe.