Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Kuna mmoja nilimsikia anasema aliyeongoza Tanganyika kupata Uhuru aliitwa Juma Lyus Manyere, ila wakoloni walimuita Julius Nyerere, hili kinaanza kiutaniutani, lakini ikifika 2050 misikitini kote watakuwa wameshafundishwa kwamba Juma Lyiusa Manyere ndiye rais wa Tanzania
Dah sijui kwann nmecheka sana 😂 kuna mambo ht kama huna uhakika nayo ila ukiyasikia unabaki kucheka tuu
 
Kumtukana Yesu alayhi salaam, ambae Waislam tunaamini ni mtume Kiislam, ni kuutukana Uislam.

Hata ikiwa sivyo, Waislam tushindane kwa hoja za kauli safi.
Kabisa maisha yenyewe magumu haya na hatuna usafi wowote mioyoni sio wakristu wala waislamu binafsi naamini kiichokuwa kinaendelea huko Kisarawe ni Ugaidi hata maswala sijui ya kuchezwa nayo Mh DC yafwatilie kwa kina wastaarabike hawa mabwana
 
Kwa mfano hilo lingekuwa kanisa watoto wanafundishwa mazingira mabovu je DC Magoti angelifunga? Je wakristo wangelalamika?Hata kama DC kakosea sawa lakini uongozi wa msikiti ulitakiwa ukamilishe miundombinu kabla ya masomo kuanza.Lililofanyika ni jambo jema Kwa hata wazazi wa watoto wamejua watoto wao wanaishi kwenye mazingira gani
 
Kwahiyo mlundike watoto kama nyanya bila utaratibu hakafu yakitokea maafa au madhara kwa watoto muanze kulaumu na kusema serikali ilikuwa wapi?

Elimu sio jambo la dharura, jengeni hostel nzuri zinazokidhi vigezo ndio muweke watoto..
 
UKIOWATAJA HATA WATANO HAWAFIKI! ILA NYINYI HADHARANI MNAJITANGAZA NA MAKANISANI KAMA UNALO RINDER NI MARUFUKU KUINGIA
Ongea kwa hoja Shehe wacha mihemko kanisa gani lilitoa hilo tamko?na ndio maana mnaonekana wajinga hamtaki kukubali ukweli miaka zaidi ya 60 baada ya uhuru unatetea upuuzi badilika shehe Dunia imechange
 
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Yule mwenzenu bomboko alivyovamia nyumba ya wageni Sinza na kudhalilisha wateja kwa kuwarekodi video uliona sawa sio?
 
Na ushukuru Magoti katumia maneno ya kistaarabu ety hakuna malazi mazuri 😂 pale ilikuwa ni mafunzo ya ugaidi.
Hapana, siyo kweli, Uislam haufundishi ugaidi.

Hao ni wapigaji tu.

Umejazwa ujinga na umekujaa.
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Watanzania tumelelewa katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano. Hii ni mizizi iliyoasisiwa na wapigania uhuru wa nchi hii na tumeweza kudumu katika misingi hiyo kwa miongo kadhaa sasa.

Anapotokea mtu, awe kiongozi ama yoyote yule, akafanya dhihaka, kukashifu, kubeza na kuingilia imani za dini fulani basi bila shaka anapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Serikali ya Rais Mama Samia ni serikali sikivu na yenye weledi inayosimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hakupaswa kuzua taharuki kwenye vyombo vya habari kwa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane msikitini, ambayo Waislamu wameitafsiri kama uvamizi dhidi ya msikiti huko Kisarawe na kuamuru kituo cha kuhifadhisha Quran kifungiwe huku akiita kuwa ni udhalilishaji.

Pia, alidai kuwa misikiti ni sehemu ya watu kuswali na kuondoka tu huku akitumia kauli za kebehi na dharau kwamba watoto wanalala kama nyanya, wamepangwa kama tofali za block, hata nguruwe hawezi kulala katika mazingira hayo. Mara aseme watoto hao walipaswa wachapwe viboko wote na wazazi wao wawekwe gerezani kwa kuwa wameshindwa kuwalea! Hizi ni dharau kwa wazazi wa Kiislamu! Mzazi anayempeleka mwanae kuisoma dini yake ili awe na maadili mema katika jamii yake aonekane ameshindwa kumlea mwanae!

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Waislamu nchini Tanzania wana taasisi yao ya BAKWATA, ambayo inashirikiana na taasisi nyingine ndogondogo kusimamia masuala ya Waislamu kwa ujumla. Petro Magoti alishindwa nini kuongea na uongozi wa BAKWATA unaoongozwa na Mufti Abubakar bin Zuber kuwa waboreshe kituo hicho cha msikiti wa Kiluvya ili kuweka mazingira rafiki ya vijana wa Kiislamu kuisoma dini yao na jambo hilo lisifike kwenye mitandao na kuzua sintofahamu kama alivyofanya yeye?

Msimamizi wa kituo cha msikiti wa Kiluvya alionekana akimueleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wanafunzi wanaishi katika hali hiyo kwa dharura tu huku jitihada mbalimbali za kuanzisha ujenzi wa mabweni zikiendelea. Nondo, mchanga, cement na matofali tayari vimeshakusanywa na jitihada za kuomba vibali vya ujenzi zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha wanafunzi wanaishi katika mazingira rafiki.

Wito wangu kwa Rais ni kuhakikisha kuwa wateule wake kama Petro Magoti hawaingilii masuala ya kidini moja kwa moja kwa sababu ni eneo nyeti linaloweza kuvunja amani ya nchi hii kwa haraka sana. Awashauri wateule wake wawe na busara katika masuala ya utawala.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.

Video ya Sheikh akitoa mapendekezo kwa serikali nini kilipaswa kufanyika.

Pia soma:Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Yaani waislam ndivyo mlivyo kila kitu mnawaza fujo ndio maana tunawaogopa hata mkikusanyika. hapa tu umeshindwa kujieleza kwa adabu ukaeleweka ni umefoka kwa makauli mazito mazito hujui kuwa sahivi nchi ipo kwenye hatari ya cabo del gado watoto wadogo wale darasa la saba hakielewi chochote kesho ashike mtutu waje watuue??

DC Magoti hawezi kukurupuka tu kufunga tena usiku wa manane yule ni kamati ya ulinzi na usalama wilaya anejihakikishia kupitia wataalam wa maswala ya ulinz na usalama

Utulie wewe samia ana mambo mengi ya kufanya na sio kushughulikia upuuzi wako
 
Mbona Sunday School mapafri wanafira watoto na hazifungwi? Mwamposa kaua watu moshi na hakufungiwa huduma
Acha kutoka povu kwasababu ya upuuzi wenu kuanikwa hadharani.Makosa ni makosa haijalishi kafanya nani.Kama mwamposa alifanya makosa hatua hazikuchukuliwa ndo nanyie muone ni sawa kufanya?.
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Watanzania tumelelewa katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano. Hii ni mizizi iliyoasisiwa na wapigania uhuru wa nchi hii na tumeweza kudumu katika misingi hiyo kwa miongo kadhaa sasa.

Anapotokea mtu, awe kiongozi ama yoyote yule, akafanya dhihaka, kukashifu, kubeza na kuingilia imani za dini fulani basi bila shaka anapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Serikali ya Rais Mama Samia ni serikali sikivu na yenye weledi inayosimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hakupaswa kuzua taharuki kwenye vyombo vya habari kwa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane msikitini, ambayo Waislamu wameitafsiri kama uvamizi dhidi ya msikiti huko Kisarawe na kuamuru kituo cha kuhifadhisha Quran kifungiwe huku akiita kuwa ni udhalilishaji.

Pia, alidai kuwa misikiti ni sehemu ya watu kuswali na kuondoka tu huku akitumia kauli za kebehi na dharau kwamba watoto wanalala kama nyanya, wamepangwa kama tofali za block, hata nguruwe hawezi kulala katika mazingira hayo. Mara aseme watoto hao walipaswa wachapwe viboko wote na wazazi wao wawekwe gerezani kwa kuwa wameshindwa kuwalea! Hizi ni dharau kwa wazazi wa Kiislamu! Mzazi anayempeleka mwanae kuisoma dini yake ili awe na maadili mema katika jamii yake aonekane ameshindwa kumlea mwanae!

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Waislamu nchini Tanzania wana taasisi yao ya BAKWATA, ambayo inashirikiana na taasisi nyingine ndogondogo kusimamia masuala ya Waislamu kwa ujumla. Petro Magoti alishindwa nini kuongea na uongozi wa BAKWATA unaoongozwa na Mufti Abubakar bin Zuber kuwa waboreshe kituo hicho cha msikiti wa Kiluvya ili kuweka mazingira rafiki ya vijana wa Kiislamu kuisoma dini yao na jambo hilo lisifike kwenye mitandao na kuzua sintofahamu kama alivyofanya yeye?

Msimamizi wa kituo cha msikiti wa Kiluvya alionekana akimueleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wanafunzi wanaishi katika hali hiyo kwa dharura tu huku jitihada mbalimbali za kuanzisha ujenzi wa mabweni zikiendelea. Nondo, mchanga, cement na matofali tayari vimeshakusanywa na jitihada za kuomba vibali vya ujenzi zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha wanafunzi wanaishi katika mazingira rafiki.

Wito wangu kwa Rais ni kuhakikisha kuwa wateule wake kama Petro Magoti hawaingilii masuala ya kidini moja kwa moja kwa sababu ni eneo nyeti linaloweza kuvunja amani ya nchi hii kwa haraka sana. Awashauri wateule wake wawe na busara katika masuala ya utawala.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.

Video ya Sheikh akitoa mapendekezo kwa serikali nini kilipaswa kufanyika.

Pia soma:Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Shekhe hiyo video umeiangalia vizuri ama basi tu umeamua kuongea ? Sio kila kitu tutetee tu kaka ule ni upuuzi, watoto wanakaa mazingira mabaya sana mkuu wa wilaya katumia busara sana sijaona hata maneno makali aliyoongea
Shida ni kwasababu Mkristo ndo mana mnaona taharuki ila kiukweli hakuna alichokosea. Watoto wanakaa sehemu duni, wamepangwa kama wako sokoni, ukiangalia hata udhibiti wa kinyesi haujakaa salama mkuu kila kitu ni hovyo kabisa tukubali ustadh na wazazi waliteleza. Pale kaomba watoto wote warudishwe na watakapokosa/kupungukiwa na kitu basi wamtaarifu yeye atasaidia kufanikisha watoto kurudi kwao sasa kuna tatizo gani hapo ndugu yangu???
 
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Awaite kimyakimya ili mfiche madhambi(makosa)yenu?Rekebisheni hali.
 
Back
Top Bottom