Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Magoti ni mabaki ya JPM, udikteta, nasubiri aanze kukamata pikipiki zimebeba fungu moja la mkaa mtu anaenda kupikia nyumbani.

Nasikia hako kajamaa ndio kalimuwekea mambo Mangula, kidogo afe.

Yeye awe kiongozi, sio nyampara
Nani sio mabaki ya JPM??
 
Watoto hso wana umri gani?? Kama chini ya miaka mitano walitakiwa kulala kwa wazazi wao na kulelewa nao. Kama ni zaidi ya miaka mitano walipaswa wapelekwe shule.
 
Magoti ni mabaki ya JPM, udikteta, nasubiri aanze kukamata pikipiki zimebeba fungu moja la mkaa mtu anaenda kupikia nyumbani.

Nasikia hako kajamaa ndio kalimuwekea mambo Mangula, kidogo afe.

Yeye awe kiongozi, sio nyampara
😂 Waislamu magaidi kazi mnayo Safar hii
 
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Hakuba taharuki yoyote iliyozungwa, mazingira yalikuwa tulivu.Sema kuna watu hamna akili kabisa..au mnafanya makusudi..hivi kweli mnawezaje kuwakabidhi watoto wadogo kwa maustadhi vijana, wasioleweka - hata kwa mtazamo tu wanatia mashaka ili wakae na watoto wenu wa kike na kiume??
 
Dhihaka na dharau alizozifanya je!?..
Kufanya vamizi za usiku na vyombo vya habari ni sahihi?

Alishindwa nini kuita viongozi wa msikiti na taasisi ya BAKWATA walimalize jambo hili bila ya kuzua taharuki? Huoni kama ni tukio linaloweza kuamsha hisia za waislam?
Mkielezwa ukweli huwa mnalia.

Piga spana hawa. Ndugu Magoti
 
wacha nianze kunywa konyagi mapemaaa kana nimemuudhi mtu humu tusameheane jaman nshaanza kupiga nyagi yanghuu hapa kwa njauwale wa mbezibeach mkuyeee tutoew mapepo na majini kwa konyt
Mpwa, utakuwa uko hapo kaunta, msalimie meneja Mayele, bila kumsahau Godi wa jiko la kitimoto,
 
We shanga kweli wewe huko mnapo walaza chini mnawalisha mavi ya ng'ombe? Serikali inawalipia ada ,badala ya kuwafundisha uhaini wapelekeni shule wakasome elimu bure
Hawa bibi wazee wanafundishwa mieleka
 

Attachments

  • VID-20240713-WA0001.mp4
    5.6 MB
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Watanzania tumelelewa katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano. Hii ni mizizi iliyoasisiwa na wapigania uhuru wa nchi hii na tumeweza kudumu katika misingi hiyo kwa miongo kadhaa sasa.

Anapotokea mtu, awe kiongozi ama yoyote yule, akafanya dhihaka, kukashifu, kubeza na kuingilia imani za dini fulani basi bila shaka anapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Serikali ya Rais Mama Samia ni serikali sikivu na yenye weledi inayosimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hakupaswa kuzua taharuki kwenye vyombo vya habari kwa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane msikitini, ambayo Waislamu wameitafsiri kama uvamizi dhidi ya msikiti huko Kisarawe na kuamuru kituo cha kuhifadhisha Quran kifungiwe huku akiita kuwa ni udhalilishaji.

Pia, alidai kuwa misikiti ni sehemu ya watu kuswali na kuondoka tu huku akitumia kauli za kebehi na dharau kwamba watoto wanalala kama nyanya, wamepangwa kama tofali za block, hata nguruwe hawezi kulala katika mazingira hayo. Mara aseme watoto hao walipaswa wachapwe viboko wote na wazazi wao wawekwe gerezani kwa kuwa wameshindwa kuwalea! Hizi ni dharau kwa wazazi wa Kiislamu! Mzazi anayempeleka mwanae kuisoma dini yake ili awe na maadili mema katika jamii yake aonekane ameshindwa kumlea mwanae!

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Waislamu nchini Tanzania wana taasisi yao ya BAKWATA, ambayo inashirikiana na taasisi nyingine ndogondogo kusimamia masuala ya Waislamu kwa ujumla. Petro Magoti alishindwa nini kuongea na uongozi wa BAKWATA unaoongozwa na Mufti Abubakar bin Zuber kuwa waboreshe kituo hicho cha msikiti wa Kiluvya ili kuweka mazingira rafiki ya vijana wa Kiislamu kuisoma dini yao na jambo hilo lisifike kwenye mitandao na kuzua sintofahamu kama alivyofanya yeye?

Msimamizi wa kituo cha msikiti wa Kiluvya alionekana akimueleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wanafunzi wanaishi katika hali hiyo kwa dharura tu huku jitihada mbalimbali za kuanzisha ujenzi wa mabweni zikiendelea. Nondo, mchanga, cement na matofali tayari vimeshakusanywa na jitihada za kuomba vibali vya ujenzi zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha wanafunzi wanaishi katika mazingira rafiki.

Wito wangu kwa Rais ni kuhakikisha kuwa wateule wake kama Petro Magoti hawaingilii masuala ya kidini moja kwa moja kwa sababu ni eneo nyeti linaloweza kuvunja amani ya nchi hii kwa haraka sana. Awashauri wateule wake wawe na busara katika masuala ya utawala.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.

Video ya Sheikh akitoa mapendekezo kwa serikali nini kilipaswa kufanyika.


Pia soma:Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Anataka serikali isiingie moja kwa moja. amesahau kuwa pale kuna watoto 96, wanakunya mavi kinyesi wameriririsha kwenye eneo la public, kipindu pindu kikiibuka hapo utawahitaji bakwata au serikali? mazingira yale tuliyaona, wanaishi kwa kupangwa kama kuku, jamaa anasema hiyo ni ibada. hivi unafikiri kwenye kamati ya ulinzi na usalama hamna waislam mle, hadi anakuja hapi unafikiri ni wakristo pekee walikaa kikao? ajabu sana.
 
mimi kilichonikera ni pale anasema, kama isingekuwa nyumba ya ibada ningekuweka ndani leo. who is he? mkuu wa wilaya mbona mtu mdogo sana, anatishia watu kuwaweka ndani?
 
Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.
Siasa ndiyo yenye hatari zaidi
 
Magoti kasema kuwa lengo la sheikh ni zuri tatizo mazingira, hao watoto hata wakienda kusoma wapi bado watafundishwa asiye muislam ni kafir tu, mbona ukristo unafundisha kuna miungu mitatu hiyo si imani yenu hakuna shida, mnekuwa watakatifu sana mapadri watatu wangekufa kanisani na kutupwa kwenye matenk ya maji?
Kwa hiyo hata wewe umekubali yale mazingira sio rafiki kwa wale watoto sio?
 
Back
Top Bottom