Waislam tunapaswa kuondokana na upofu wa dini la sivyo tutaonekana wote hatuna akili

Waislam tunapaswa kuondokana na upofu wa dini la sivyo tutaonekana wote hatuna akili

Mnaudhalilisha uislamu. Muislamu popote alipo kazi yake ya kwanza ni kupinga maovu kama haya ya serikali ya awamu ya 6. Maovu yamevuka mipaka mpaka wanaamua kuuza ardhi na watu walioko. Ni dhihaka.
 
Serekali imeshajua ni rahisi kuwateka waisilamu kupitia dini yao. Wanajua waisilamu hawana muda wa kuangalia ukweli ikishachomekwa hisia ya dini yao. Kibaya zaidi viongozi wao ndio wamekuwa wepesi kupotezwa kwenye hoja, na kuachwa wakipayuka kushambuliwa kwa dini yao kwa jambo lisilo na uhusiano na dini, ili mradi msimamizi wa jambo ni muislamu, basi wao hilo jambo hulifanya ndio uislamu!
Ktk suala hili la Bandari, Waislamu tumejifedhehesha kidogo. Tunakurupuka. Tunatumiwa. CCM wajanja sana.
 
Kwaimani yetu waislam hatuna kitukingine chakutufunza zaidi ya kitabu tukikiacha tumekwisha
Dini ya kweli ni pesa. Pesa ndio zinaweza kufanya mambo yako mengi yakakaa sawa, sio dini boss. Waislamu, wakristo na wasio kuwa dini, wote hao maisha yao yananyooka wakiwa na pesa, na sio wakiwa wameshika sana dini.
 
Raisi akiufuta huo Mkataba atapita kwa kishindo 2025.
Pia liwe somo kwake kuwa nchi imemkabidhi raslimali zote aziongoze na kuzilinda.

"Dunia ya leo haina rafiki bali ina fulsa tele. Hakuna Tabasamu la kweli bali la mali" by Mimi,

Nchi imeahidi kumhudumia maisha yake yote.
Awe makini asiingizwe tena kwenye Mkenge na Wasaka Tonge.
 
Kama kuna kitu Waislamu tunapaswa kukifanya katika kuandika HISTORIA yetu na ikasomwa kila baada ya sala ni hii ya Ikulu ya Magogoni hapa Dar es salaam maana ni historia yetu na ni halali kwetu kufanya hivyo ila sio kwenye suala la Mkataba wa Bandari; huko tunahitaji kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu mikataba ya kimataifa.

Viongozi wetu hasa Ma-Imamu wetu na wengine wanaokaribishwa kutoa neno, wakumbuke kwamba suala la Bandari linahitaji udadavuzi wa SHERIA na SIO SHARIA. Hili la Bandari halihitaji MUAZINI kulisimamia, linahitaji wataalamu wa sheria kulichambua nando maana hatua yakwanza kabisa kupinga ilipelekwa mahakamani kupata ufafanuzi wa kisheria, hukumu ikatoka kwamba mkataba unazo dosari unatakiwa kurekebishwa. Kitaalamu hii ilishindikana mahakama kutengua maamuzi ya Bunge bali ilishauri Bunge lipitie sheria hizo litekebishe huo mkataba. Kwa kifupi ni kwamba MKATABA hauna faida kwa taifa.

Katika eneo ambalo Waislam tunapaswa kuliellewa ni kwamba tunapaswa kulizingatia ni hili viongozi wetu kuweka maneno ya chuki dhidi ya imani zingine, tukishindwa kuwahoji misikitini basi tutoke tuwaache waendelee na SOGA zao baada ya IBADA.

Kuna ujinga unasambazwa kwamba UJIO wa DP World utalifanya KANISA lisiingize makontena yao kwa msamaha wa kodi. Innalillah Wainalillah rajiun; kwanza tutambue masuala yote ya kikodi yanapangwa na serikali yetu, ni suala la DP World kukabidhiwa list ya misamaha ya KODI kwa taasisi husika. Na hapo hakuna atakaepinga. DP World hawaji kupanga masuala ya kodi ama tozo za bandarini; bei elekezi za bandari zitaendelea kusimamiwa na TPA na TRA. Hili Waislam tulielewe; tusipuyange.

Yaani kwa kifupi ile misamaha ambayotuliipeleka ya kuomba kuondolewa kodi ya TENDE, msamaha wa kodi ya MAJI ya ZAMZAM na mengineyo DP WORLD watayakuta mezani. Halafu pia wataikuta list ya misamaha ya kodi ya VIFAA TIBA, VIFAA VYA KUJIFUNZIA WANAFUNZI SUNDAY SCHOOLS, SECONDARY, COLLEGES nk wataikuta pale. Kwa hiyo hakuna kitu KANISA watapoteza bali wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kuangalia uhalali wa mkataba na sio kuhusu misamaha ya kikodi au kwa sababu mwekezaji ni kampuni kutoka taifa la kiarabu. Mataifa mangapi ya kiarabu yamewekeza hapa? Ukienda pale Ngorongoro kuna kampuni ngapi za kiarabu? Ukienda Loliondo pale kuna maeneo ukifika unakaribishwa UAE 🇦🇪, umewahi kuona kanisa linaongelea hayo?

Hawa akina Arab contractors wanaojenga Bwawa la Mwalimu Nyerere si wanatoka Misri? Au wale mnawachukulia kuwa ni wajukuu wa FARAO? Na hawa wanaojenga SGR si ni waarabu wa Uturuki 🇹🇷 ? Au wale mnawachukulia ni ndugu zake Ottoman? Jikiteni katika kuzijadili hojaza TEC na sio kuwajadili waliokaa kuzichambua hizo hoja.

Anyway; ngoja niwarudisheni kwenye historia kidogo kuhusu Ikulu ya Magogoni na hili mkalikalie vikao mlijadili pengine mnaweza kulidai iwe mali yetu Waislam maana kihistoria ni mali ya Waislam na hata Magufuli aliamua kuhamisha makao makuu Dodoma ili ikulu hii iwe sehemu ya historia mkapate kuijua hii Ikulu vema.

Pale mlango wa kuingia Ofisi ya Rais (Ikulu) kuna maandishi yanasomeka hivi (ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ), maandishi haya yanatoka katika Aya ya Quran Surat Al HIJR Aya Ya 46 inayosema
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ
Wataambiwa "Wacha Mungu" Ingieni kwa salama na amani. Ikisomeka (Udkulu_Ha_Bi_Salamin_Aminina)

Jina Hili la (Dare Salaam) lilibadilishwa na Wajerumani Kutoka katika jina la Asili la (DARU SALAAM) baada ya Wajerumani kuwatoa Waislamu kimabavu katika eneo hilo na kuiweka Ikulu mwaka 1870.

Ikumbukwe kwamba Ikulu hii ilikuwa msikiti uliojengwa na Sultan Majid kutokea Zanzibar Mwaka 1865 kwa ajili ya watu kujifunzia Quran na kusoma elimu ya Dini ya kiislam (leo tungesema ulikuwa msikiti wenye chuo cha Madrasa ) ambako watu mbalimbali kutoka Congo, Malawi, walifika kusoma hapa. Jengo hili likaitwa #DAR_U_SALAAM (Dar es salaam) kama walivyo zoea wengi. Neno hilo ni neno la Kiarabu lenye maana ya NYUMBA YA AMANI. Neno hili sio geni Duniani, ukienda LEBANON utakuta Dar Salaam..

Kwa hiyo katika mambo tunayoweza kuyafundisha kama historia ni haya lakini sio huku tunakotaka kwenda.

Tujisahihishe
Siku likija suala la Mahakama ya Kadhi sijui itakuajee kwakweli, ambalo kimsingi ndilo linaweza kua sura ya kidini.

Wakati huo sijui akina jakaya watasema kuchanganya bongo flavor na hip hop au itakuaje,
Maana dipi weldi wamesema ni kuchanganya dini na siasa
 
Dini ya kweli ni pesa. Pesa ndio zinaweza kufanya mambo yako mengi yakakaa sawa, sio dini boss. Waislamu, wakristo na wasio kuwa dini, wote hao maisha yao yananyooka wakiwa na pesa, na sio wakiwa wameshika sana dini.
Endelea kuamini dini yako wewe nipesa Mao asingekufa kwangu Mimi na waminio pesa nimapito
 
.. mahakama haijatupilia mbali hoja zote za kina Mwabukusi.

..kuna baadhi ya hoja imekubaliana nazo na imeshauri, kwa hofu ya kuliingilia bunge, mkataba urekebishwe.

..mahakama pia imeeleza kwamba kilichopitishwa na bunge ni mkataba na sio makubaliano kama ambavyo watetezi wa serikali wamekuwa wakisisitiza.

..wakosoaji wa mkataba wamesisitiza mara nyingi kwamba hawapingi dini ya mtu, au dini ya muwekezaji wa Dubai Port.

..wako waliokwenda mbali kwa kuweka msisitizo kwamba mkataba hauna mahusiano yoyote na imani ya Kiislamu. Na kwamba mkataba na Dp ni mbaya hata kama ungesainiwa na Mkristo, au Mpagani.

..mimi nadhani CCM inawatumia vibaya ndugu zetu Waislamu. Kwasababu CCM wamekosa hoja za kutetea mkataba wao mbovu wameamua kujificha kwenye kichaka cha udini, na haswa dini ya Rais Samia.

..Ni kitu cha kushangaza kwamba Mashekhe na Maimamu wanatetea mkataba na Dp kuliko wabunge walioupitisha na makada wa CCM.
Ikiwa mahakama imeshauri mkataba urekebishwe nyinyi nani wa kusema mkataba haufai?
Hakuna kitu kitakachofnaywa na mwanadamu kikawa kamili kwa mwanadamu mwingine.
Ikiwa mnaona CCM inawatumia vibaya waislamu, je nitakuwa sahihi kusema na CHADEMA inawatumia baadhi ya wakristo na makanisa vibaya kwa kupinga mkataba?
 
Endelea kuamini dini yako wewe nipesa Mao asingekufa kwangu Mimi na waminio pesa nimapito
Kifo hakihusiani na dini, labda useme mtu akiwa kwenye dini yako hafi. Lakini ni dhahiri mtu mwenye pesa ama maisha mepesi kuliko mshika dini.
 
Kanye kanisani
Hata akinya kanisani unadhani wakristo huwa tunafanya fujo yoyoye? Sana sana tutasafisha huo uchafu na kulaani kitendo hicho. Hatutachoma misikiti kama nyinyi mnavyofanya mkiwa provoked.
 
Kama kuna kitu Waislamu tunapaswa kukifanya katika kuandika HISTORIA yetu na ikasomwa kila baada ya sala ni hii ya Ikulu ya Magogoni hapa Dar es salaam maana ni historia yetu na ni halali kwetu kufanya hivyo ila sio kwenye suala la Mkataba wa Bandari; huko tunahitaji kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu mikataba ya kimataifa.

Viongozi wetu hasa Ma-Imamu wetu na wengine wanaokaribishwa kutoa neno, wakumbuke kwamba suala la Bandari linahitaji udadavuzi wa SHERIA na SIO SHARIA. Hili la Bandari halihitaji MUAZINI kulisimamia, linahitaji wataalamu wa sheria kulichambua nando maana hatua yakwanza kabisa kupinga ilipelekwa mahakamani kupata ufafanuzi wa kisheria, hukumu ikatoka kwamba mkataba unazo dosari unatakiwa kurekebishwa. Kitaalamu hii ilishindikana mahakama kutengua maamuzi ya Bunge bali ilishauri Bunge lipitie sheria hizo litekebishe huo mkataba. Kwa kifupi ni kwamba MKATABA hauna faida kwa taifa.

Katika eneo ambalo Waislam tunapaswa kuliellewa ni kwamba tunapaswa kulizingatia ni hili viongozi wetu kuweka maneno ya chuki dhidi ya imani zingine, tukishindwa kuwahoji misikitini basi tutoke tuwaache waendelee na SOGA zao baada ya IBADA.

Kuna ujinga unasambazwa kwamba UJIO wa DP World utalifanya KANISA lisiingize makontena yao kwa msamaha wa kodi. Innalillah Wainalillah rajiun; kwanza tutambue masuala yote ya kikodi yanapangwa na serikali yetu, ni suala la DP World kukabidhiwa list ya misamaha ya KODI kwa taasisi husika. Na hapo hakuna atakaepinga. DP World hawaji kupanga masuala ya kodi ama tozo za bandarini; bei elekezi za bandari zitaendelea kusimamiwa na TPA na TRA. Hili Waislam tulielewe; tusipuyange.

Yaani kwa kifupi ile misamaha ambayotuliipeleka ya kuomba kuondolewa kodi ya TENDE, msamaha wa kodi ya MAJI ya ZAMZAM na mengineyo DP WORLD watayakuta mezani. Halafu pia wataikuta list ya misamaha ya kodi ya VIFAA TIBA, VIFAA VYA KUJIFUNZIA WANAFUNZI SUNDAY SCHOOLS, SECONDARY, COLLEGES nk wataikuta pale. Kwa hiyo hakuna kitu KANISA watapoteza bali wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kuangalia uhalali wa mkataba na sio kuhusu misamaha ya kikodi au kwa sababu mwekezaji ni kampuni kutoka taifa la kiarabu. Mataifa mangapi ya kiarabu yamewekeza hapa? Ukienda pale Ngorongoro kuna kampuni ngapi za kiarabu? Ukienda Loliondo pale kuna maeneo ukifika unakaribishwa UAE 🇦🇪, umewahi kuona kanisa linaongelea hayo?

Hawa akina Arab contractors wanaojenga Bwawa la Mwalimu Nyerere si wanatoka Misri? Au wale mnawachukulia kuwa ni wajukuu wa FARAO? Na hawa wanaojenga SGR si ni waarabu wa Uturuki 🇹🇷 ? Au wale mnawachukulia ni ndugu zake Ottoman? Jikiteni katika kuzijadili hojaza TEC na sio kuwajadili waliokaa kuzichambua hizo hoja.

Anyway; ngoja niwarudisheni kwenye historia kidogo kuhusu Ikulu ya Magogoni na hili mkalikalie vikao mlijadili pengine mnaweza kulidai iwe mali yetu Waislam maana kihistoria ni mali ya Waislam na hata Magufuli aliamua kuhamisha makao makuu Dodoma ili ikulu hii iwe sehemu ya historia mkapate kuijua hii Ikulu vema.

Pale mlango wa kuingia Ofisi ya Rais (Ikulu) kuna maandishi yanasomeka hivi (ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ), maandishi haya yanatoka katika Aya ya Quran Surat Al HIJR Aya Ya 46 inayosema
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ
Wataambiwa "Wacha Mungu" Ingieni kwa salama na amani. Ikisomeka (Udkulu_Ha_Bi_Salamin_Aminina)

Jina Hili la (Dare Salaam) lilibadilishwa na Wajerumani Kutoka katika jina la Asili la (DARU SALAAM) baada ya Wajerumani kuwatoa Waislamu kimabavu katika eneo hilo na kuiweka Ikulu mwaka 1870.

Ikumbukwe kwamba Ikulu hii ilikuwa msikiti uliojengwa na Sultan Majid kutokea Zanzibar Mwaka 1865 kwa ajili ya watu kujifunzia Quran na kusoma elimu ya Dini ya kiislam (leo tungesema ulikuwa msikiti wenye chuo cha Madrasa ) ambako watu mbalimbali kutoka Congo, Malawi, walifika kusoma hapa. Jengo hili likaitwa #DAR_U_SALAAM (Dar es salaam) kama walivyo zoea wengi. Neno hilo ni neno la Kiarabu lenye maana ya NYUMBA YA AMANI. Neno hili sio geni Duniani, ukienda LEBANON utakuta Dar Salaam..

Kwa hiyo katika mambo tunayoweza kuyafundisha kama historia ni haya lakini sio huku tunakotaka kwenda.

Tujisahihishe
Mkuu wewe ni muislam na mzalendo wa kweli!
 
Uko sahihi. Masheikh wapo kwenye majibizano ya kushindana, wakati maaskofu wanaweka mbele mustakbali wa Taiifa zima ndiyo maana huoni maaskofu wakiandika neno "sheikh", "uislamu", "waislamu" katika waraka wao.

Hao DP World wametimuliwa Djibouti nchi ya asilimia 98 waislamu tupu sembuse hapa kwetu!

Ishu hapa ni mkataba mbovu, siyo habari za uislamu wala Ukiristo

Mbona waislamu wa Uturuki wanajenga SGR maaskofu hawajatoa waraka?
Mbona Waislamu wa Misri wanajenga bwawa la Stieglers maaskofu hawajatoa waraka?

Qur'an inasema simamia haki na sema ukweli hata kama ukweli unakutandika wewe mwenyewe!

Usiposimamia haki na ukweli utaonekana kituko tu, bali yule asimamiaye ukweli atapata heshima!

Na ukweli haujalishi kausema paroko, askofu au imamu na sheikh!

Kwenye hili la bandari, maaskofu wapo katika ukweli na haki!
NEW WORLD ECONOMIC ORDER ndio inayowafanya DPW wakutane na upinzani hapa Tanzania. Ukubwa wa hiyo kampuni ya Dubai huwezi kuulinganisha na hao waturuki wanaojenga SGR.

Wanamiliki meli 400 kwa ufupi ni watawala wapya wa biashara ya usafiri wa kwenye maji.

Kuondoka Djibouti ni masuala ya kuingia mikataba bila ya kuwa na utaalam mzuri, na kwenye utaalam Tanzania tupo vizuri sana kuliko Djibouti.
 
Ikiwa mahakama imeshauri mkataba urekebishwe nyinyi nani wa kusema mkataba haufai?
Hakuna kitu kitakachofnaywa na mwanadamu kikawa kamili kwa mwanadamu mwingine.
Ikiwa mnaona CCM inawatumia vibaya waislamu, je nitakuwa sahihi kusema na CHADEMA inawatumia baadhi ya wakristo na makanisa vibaya kwa kupinga mkataba?

..uamuzi wa mahakama huwa haufuti mtizamo au maoni ya mhusika / wadau kuhusu shauri husika.

..Unaweza usikubaliane na hukumu lakini unawajibika kuheshimu maamuzi ya mahakama.

..hivyo basi hukumu ya mahakama haizuii wananchi kusema kuwa mkataba na Dubai haufai kabisa, unahitaji marekebisho, au unafaa.

..dhana kwamba CCM inawatumia vibaya Mashekhe na Maimamu inatokana na hoja ambazo huzijenga, na uzito wa hoja hizo.

..Kwa mfano, kuna Mashekhe na Maimamu badala ya kuujadili mkataba na vipengele vyake wanawajadili wale walioupinga mkataba huo.

..Mazingira hayo ndio yanayosababisha uwepo wa tuhuma kwamba hawa ndugu zetu wanatumiwa vibaya na CCM kushambulia wanaopinga mkataba wa Dp.

..Kwa upande mwingine kuna Mashekhe na Maimamu ambao wamejisimamia wenyewe na wametoa maoni yenye kujenga.

..Shura ya Maimamu kipindi cha nyuma walitoa maoni ambayo yako very constructive na maoni hayo yalipokelewa vizuri.
 
mkuu unaweza ukaonyesha popote katika walaka wa TEC uislam wa rais ukihusishwa katika mkataba wa DP world??maana tuna uhakika hata markez wa SGR ni waislam wazuri kabisa lakini TEC hawana shida nao.
mnataka kutumia kete ya dini mkiwa na nia gani na taifa hili enyi wachumia tumbo mliokosa elimu mpaka busara???

tofauti ya TEC na hawa masheikh ni moja tu,wao wamejikita kwenye ubovu wa mkataba,nyinyi mnajikita kwenye kuwaparua wao,ndio maana inabidi uislam uingizwe kwa nguvu,bahati nzuri waislam walio wengi hawana imani na bakwata,hivyo itakuwa ngumu sana kueleweka mbele ya waislam kwa kete hii,hapa waislam hawana namna zaidi ya kutafiti kwanza wanachoambiwa watakataa kuwa ngamia tu.

mkataba ule sio code za nuclear,unasomeka na unaeleweka na yeyote tu,ni mpumbavu pekee atakayeamua kuukumbatia,bahati mbaya hata wanaoutetea wanaonekana hawakuusoma kabisa.

ni kweli kabisa elimu ya kiislam ni pana kabisa,lakini haihusiki kabisa kwenye mikataba ya bandari na raslimali za nchi,ndio maana unaona masheikh wanashihirisha hapa kwamba wameiva kwenye sharia ila wanatutangazia upumbavu walio nao.na kukusahihisha sharia hiyo haihusiani kabisa na maendeleo ya arab ya leo.
mkorinto kwanza ujifunze kiswahili vizuri, hakuna kitu kinaitwa "walaka" ni waraka, asili ya neno hili ni kiarabu lenye maana ya jani la mti, kwa kuwa watu wa zamani walikuwa wakiandika kwenye baadhi ya majani ya miti au vitu mfano wa majani, kwa kiswahili waraka ni karatasi iliyoandikwa taarifa maalum.
TEC ni wawakilishi wa wakristo wa kikatoliki, waraka waliyoutoa wa kupinga uwekezaji wa DPW kwenye bandari zetu kwa kusema wao wanawawakilisha watanzania wengi wenye kuukataa uwekezaji huo, swali huo wingi wa wanaowakilshwa na TEC wamepimwaje? Ikiwa TEC inawawakilisha wapinga mkataba na miongoni mwao wamefika kumshutumu raisi kwa imani yake na uasili wake kwa kusema kwa kuwa yeye ni mzanzibari na muislamu ndiyo maana anataka kuiuza nchi ya Tanganyika kwa waarabu, kwa muktadha huo ndiyo maana TEC inaingia kwenye shutuma hiyo. Ni kweli wachungaji wengi wana shahada za juu lakini kwa hili wamekosa hekima kabisa, taasisi ya kidini unaona kuna moto unawaka wewe unakwenda kumwagilia petroli! TEC wamezungumza na raisi wamezungumza na wizara, wamezungumza na vyombo mbalimbali kuhusu suala hili, ambalo serikali imelitia saini, bunge imelipitisha, mahakama imeliridhia, sasa kutoa huo waraka ni kama kudharau maamuzi ya serikali, bunge na mahakama? Huo waraka hauna afya ya usalama kwa nchi kama yetu, hayo mambo wawaachiye vyama vya siasa vya upinzani vilishughulikie haya mambo ya kuipinga serikali, wao wabaki na kondoo wao katika kuimarisha imani za wafuasi wao. Baadhi ya masheikh wamekasirika si kwa sababu ya kupinga uwekazaji wa bandari bali jinsi upingaji ulivyowasilishwa na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini ya kikristo kwenye mitandano na hata mikutano ya hadhara.
Mkataba unautaalamu wake katika kuandika na hata kuusoma na kuelewa ndiyo maana wanasheria wasomi wamekwenda mahakamani kutafuta msaada wa kishreia katika mambo ambayo wao wameyaona ni mapungufu ya kuufanya mkataba uwe batili, hatima yake mahakama imetoa ushauri kama kuna maboresho yafanywe kwenye huo mkataba na kuitupilia mbali kesi na uwekezaji uendelee.
Waislamu kutokana na misingi ya sheria zao za dini, ndiyo zimewafanya kuwa na mikataba bora yenye kuwa na uaminifu, haki na uadilfu katika kutekeleza makubaliano yao.
 
Back
Top Bottom