Hivi wakristu funga yao inakuaje? mwenye kuelewa anieleweshe
WAKRISTO wanafunga kufanya Toba na kuomba kile wanachokitaka Mwenyezi Mungu awatendee.kwa ufupi wanafunga kwajili ya ibada.na Ibada si kati yako we na Mungu wako?basi kama ni hivo batakiwi kuhusika mtu yeyote wa tatu labda kama mmepatana wawili watatu kuombea jambo moja.mfano mume na mke wamepatana kuombea uzazi katika funga Yao watapatana kufunga wao wawili pekee,hakuna wengine kujua.
WAKRISTO wanafyatua kile bible INASEMA sio maneno ya watu.bible inakataza kumtangaza funga yako..inatakiwa iwe Siri kati yako na muumba wako.labda wanaweza jua memba wa familia unaoishi nao ndani,mfano wanapika chakula unawaambia mi msinijumuishe.wengine watahitaji sababu kwanini Huli ukiwaambia nafunga hapo sawa.lakini bado ukawaambie majirani nimefunga unakuwa umeharibu!
Sasa kama funga yako ni Siri na muumba wako kwanini jioni ujaze mazagagaza kibarazani huku unapiga kelele kukaribisha watu karibuni tufuturu jamani...hii inakuwa tangazo indirect kuwajulisha umefunga ndo unafungulia,UMEHARIBU!
Ndo mana wengi wanafuturu ndani,na futari zao ni simpo na hawali daku usiku wa manane.wengi ukila saa 12-1 ndo imetoka labda Ule baadae kidogo saa tatu Kisha unaenda kulala.usiku wa manane sio mda wa kula ni wa kusali kupeleka haja zako kutoka kwenye Ile funga yako.na pia mida hiyo inakuwa tayari siku nyingine mpya so unatanguliza Ibada ukiamka mfungo unaendelea.
Na Wanaweza kwenda hata siku tatu mfululizo bila kula.huku wanasali
Pia WAKRISTO wamegawanyika,Kuna madhehebu mbalimbali,Kuna wengine hawaufafi mfungo kama walokole,lakini wanafunga siku yoyote ya mwaka wakiamua.
Kuna wasabato hawa nao Wana taratibu zao.
Lakini Kuna madhehebu kama Lutheran kkkt,Anglican,Roman hawa wana taratibu na KWARESMA inawahusu.hata majivu wote wanapaka siku Moja,ijumaa kuu hawali nyama Wala vyakula vya starehe Wala kujihusisha na shamra.
Mwisho wa yote Mkristo hashururtishwi kufunga.ni hiari yake japo Kwa faida yake.akiamua sawa,asipoamua pia sawa.