Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
inawafaa sana wale kule zanzibar wanao pita wakiwauliza wenzao kama "mmefunga", au wale waliofunga mikahawa na kuwatangazia watu kwamba wamefunga, wale wanaonawa na kuvaa kanzu safiii na kutembea kwa upole upole ili watu wawaone kuwa wamefunga.Hii tunaipita kama hatuioni.
WAKRISTO wanafunga kufanya Toba na kuomba kile wanachokitaka Mwenyezi Mungu awatendee.kwa ufupi wanafunga kwajili ya ibada.na Ibada si kati yako we na Mungu wako?basi kama ni hivo batakiwi kuhusika mtu yeyote wa tatu labda kama mmepatana wawili watatu kuombea jambo moja.mfano mume na mke wamepatana kuombea uzazi katika funga Yao watapatana kufunga wao wawili pekee,hakuna wengine kujua.Hivi wakristu funga yao inakuaje? mwenye kuelewa anieleweshe
Wakristo wa kweli, sio hao wa kwaresma au wanaofanana na hao, wanafunga mara nyingi sana, ila hawana kalenda kwasababu hawafungi wakisukumwa na dini, wanasukumwa na nia ya kumtafuta Mungu kwa mambo mbalimbali. ni tofauti na wengine ambao mwezi fulani tu ndio wa funga, mingine ni kuzini, kuua, kuchinja wasioamini, kufanay kila ovu alimradi kuna mwezi umepangwa wa kuja kutubu kwa funga. hi ndio tofauti kubwa sana.Hivi wakristu funga yao inakuaje? mwenye kuelewa anieleweshe
Uislam haujasema ukifunga ujitangaze, Uislam haujasema ukifunga utie unyonge au mumkataze mtu asiyefunga. Kufturu kibarazani au kujaza futari kibao hiyo ni Rizki ya mtu siyo mbaya kutenga futari nje na muislam mwenzako akipita aje afturu Kuna wengine kupata futari ni mtihani kwaiyo hatujionyeshi bali kusaidiana na ni Sunna kufturu vizuri kama ilivyo sikukuu kupika vyakula vizuri.WAKRISTO wanafunga kufanya Toba na kuomba kile wanachokitaka Mwenyezi Mungu awatendee.kwa ufupi wanafunga kwajili ya ibada.na Ibada si kati yako we na Mungu wako?basi kama ni hivo batakiwi kuhusika mtu yeyote wa tatu labda kama mmepatana wawili watatu kuombea jambo moja.mfano mume na mke wamepatana kuombea uzazi katika funga Yao watapatana kufunga wao wawili pekee,hakuna wengine kujua.
WAKRISTO wanafyatua kile bible INASEMA sio maneno ya watu.bible inakataza kumtangaza funga yako..inatakiwa iwe Siri kati yako na muumba wako.labda wanaweza jua memba wa familia unaoishi nao ndani,mfano wanapika chakula unawaambia mi msinijumuishe.wengine watahitaji sababu kwanini Huli ukiwaambia nafunga hapo sawa.lakini bado ukawaambie majirani nimefunga unakuwa umeharibu!
Sasa kama funga yako ni Siri na muumba wako kwanini jioni ujaze mazagagaza kibarazani huku unapiga kelele kukaribisha watu karibuni tufuturu jamani...hii inakuwa tangazo indirect kuwajulisha umefunga ndo unafungulia,UMEHARIBU!
Ndo mana wengi wanafuturu ndani,na futari zao ni simpo na hawali daku usiku wa manane.wengi ukila saa 12-1 ndo imetoka labda Ule baadae kidogo saa tatu Kisha unaenda kulala.usiku wa manane sio mda wa kula ni wa kusali kupeleka haja zako kutoka kwenye Ile funga yako.na pia mida hiyo inakuwa tayari siku nyingine mpya so unatanguliza Ibada ukiamka mfungo unaendelea.
Na Wanaweza kwenda hata siku tatu mfululizo bila kula.huku wanasali
Pia WAKRISTO wamegawanyika,Kuna madhehebu mbalimbali,Kuna wengine hawaufafi mfungo kama walokole,lakini wanafunga siku yoyote ya mwaka wakiamua.
Kuna wasabato hawa nao Wana taratibu zao.
Lakini Kuna madhehebu kama Lutheran kkkt,Anglican,Roman hawa wana taratibu na KWARESMA inawahusu.hata majivu wote wanapaka siku Moja,ijumaa kuu hawali nyama Wala vyakula vya starehe Wala kujihusisha na shamra.
Mwisho wa yote Mkristo hashururtishwi kufunga.ni hiari yake japo Kwa faida yake.akiamua sawa,asipoamua pia sa
Waislam wakifunga hata usiyemuislam utafaidi. Sio wachoyo, Sio wabaguzi kwenye futari. Nimewahi kupanga nyumba moja na waislam ikifika mfungo sisi wakristo tulikuwa tunafaidi sana. Kikipikwa chakula cha kufuturu na sisi tumo kwenye bajeti hata kama wanajua hatujafunga.
Wakristo tukifunga, mara nyingi futari inakiwa ya kichoyochoyo. Mtu anajifichaficha. Asiyehusika akisogelea msosi utasikia, huu ni wa waliyefunga au haujui mimi nilikuwa nimefunga.
Ile bajeti ya chakula ambayo atakuwa ameikwepa kwa kufunga badala ya kuitumia kama sadaka kwa kuwezesha wasio na chakula wengi wanachukulia kama savings. Amesevu kwa matumizi yake ya baadae.
Tumesahau
Isaya 58:6
Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Isaya 58:7
Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?Kwan kufunga si siri yako na Mungu wako au inakuaje