Waislam waruhusiwe kwenda Msikitini leo Ijumaa

Waislam waruhusiwe kwenda Msikitini leo Ijumaa

Mimi binafsi naenda kuswali,nishawahi acha kazi kwa kuambiwa nichague kuswali au kufanya kazi,nikachagua kuswali

Najua anayetoa ridhiki ni Allah,na kweli baadae nikapata kazi nyingine tena bora kuliko ile

Ila kwa ujumla ni bora kuheshimu siku ya ibada ya waislamu ya ijumaa,kwani hawawezi panga mda mwingine?
Si unaona sasa , uliacha kazi , Ndio mana tunasema dini ni ujinga zinaleta umasikini ...
 
Si unaona sasa , uliacha kazi , Ndio mana tunasema dini ni ujinga zinaleta umasikini ...
Unajua kuna tatizo moja ambalo wengi wenu mnalo,kama wewe huamini Mungu wala dini kumbuka ni tatizo lako binafsi na usitake liwe letu

Sasa sisi ambao tunaamini juu ya uwepo wa Allah na kuwa yeye ndio kila kitu huwa hatupagawishwi na kazi za watu au mambo ya watu,tunajua mwisho wa siku mwenye kumiliki ridhiki ni Allah,kama alinipa kazi ya mwanzo basi atanipa nyingine

Ridhiki haipo katika mamlaka ya binadamu yoyote yule,je umewaona ndege wanalima au wanafanya kazi? Lakini wanatoka asubuhi matumbo yakiwa matupu na jioni wanarudi wakiwa wameshiba,huyo ni Allah al razaq mwenye kuruzuku
 
Siamini kama kuna sehemu wanazuiwa kwenda. Tuache uchochezi
Sasa nikushangaze zaidi aliyenikataza kuswali swala tano ni muislamu mwenzangu,tena kumbuka naswali hapo hapo ofisini,naenda chemba sehemu nachukua dakika zisizo zidi 10 tu
 
Pole sana. Wanadamu ndivyo tulivyo.
Mtihani sana,mwanadamu mwenzako anapokwambia chagua kazi au kuswali kwa maana nyingine anakwambia mchague Mungu au kazi,kama sio upuuzi ni nini?

Je kabla ya hiyo kazi nilikuwa naishi vipi?

Ukimuamini Mungu katu hatokutupa,utapata mitihani na dhiki za mda fulani lkn atakupa rehema zake kwa kuwa umeamini juu yake kwamba yeye ndio muweza wa kila kitu

Asante
 
Back
Top Bottom