Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Karibu taasisi zote za dini ya kikristo zilizojikita kwenye sekta ta elimu zimekuwa busy mnoo kuusoma, kuuelewa, kujiandaa na kuwaandaa watumishi wake namna ya kwenda sambamba na ujio wa mtaala (sera) mpya wa elimu. Jambo hilo limekuwa likifanyika vivyo hivyo kwa jamii za waumini wa kikristo. Ni kama wanapambana na jambo la lazima tena kwa uharaka huku wakilitazama kama fursa adimu.
Na kama vile wataalamu walivyoonya mapema kuwa, kwa namna mtaala mpya ulivyokaa na kwa namna mifumo ya taasisi nyingi za kielimu zilivyo dhaifu, Tanzania tunakwenda kuzalisha tena kizazi chenye mgawanyiko mkubwa wa maarifa na ufahamu katika jamii.
Yale malalamiko ya miongo yote ya ndugu zangu wa kiislamu kuhusu kuwepo mfumo kristo unaowanyonya waislamu na kuwabeba wakristo baada ya miaka kumi tu ijayo yataibuka upya lakini hayatakuwa na msingi wowote wa kutetewa maana hayawezi kuzuia kitu.
Ndugu zangu amkeni sasa, andaeni mazingira bora na lazima ya kuwawezesha watoto wenu kielimu. Dunia hauna huruma.