Sina haja ya kuweka takwimu wala siwezi kukutukana kila kitu kipo mitandaoni. Jaribu kuangalia hata wakimbizi wa Syria, Afghanistan na Iraq walienda wapi na ukikaa nao huku ulaya wanakuwambia bbora huku kuliko nchi za kiarabu.
Kwa nn kusiwe na haja ya kuweka takwimu ili kudhibitisha madai yako?
Ww ulisha wahi kwenda Qtaar, UAE,Oman,Saudia na usiwakute hao raia kutoka Iraq,na Syria au Afghanistan?
Unajua ni nchi zipi zinazo wahifadhi wakimbizi wengi kutoka kwenye hizo nchi ulizo zitaja hapo au unajiropokokea tu? Nchi pekee yenye wakimbizi wengi kutoka mashariki ya kati ni Ujerumani tu hakuna nyingine na wenyewe walianza kwenda Ujerumani baada ya Uturuki kuzidiwa.
Hujui suala la wakimbizi kwenda Ulaya lilikuwa linakuzwa na vyombo vya habari kwa ajili ya propaganda za kisiasa na kujitukuza kwa wazungu?
Alafu kingine unacho takiwa kukijua ni kuwa kijografia ni rahisi kutoka hizo nchi kwenda Ulaya kuliko kwenda kwenye nchi za Ghuba.
Hizi ndo nchi zinazo wahifadhi wakimbizi wengi kutoka mashariki ya kati.
(1) Iran ina wahifadhi zaidi ya wakimbizi milion 4.5 kutoka Iraq na Afghanistan.
(2) Uturuki inawahifadhi wakimbizi milion 4 kutoka wengi wao wakiwa kutoka Syria.
(3) Jordan inawahifadhi wakimbizi milion 2 kutoka Syria.
(4)Lebanon imewahifadhi wakimbizi kutoka Syria milion 1.5kutoka Syria.
(5) Ujerumani iliwahifadhi wakimbizi milion 1 kutoka Syria.
Hata hivyo wakimbizi wengi wamesha rudi nchini mwao baada ya vita kupungua mfano Ujerumani zaidi ya wakimbizi laki 8 wamesha rudi nchini mwao.