Wanabodi,
Watanzania wote waliosoma enzi za mkoloni mpaka tunapata uhuru, tumekuwa na elimu ya aina 3. Shule za serikali, Government Schools, Shule za Mission, na elimu ya madras kwa ndugu zetu Waislamu.
Shule za serikali zilikuwa chache na zilichukua wanafunzi wachache tena vichwa kweli kweli, hivyo Watanzania wengi waliemika kupitia Shule za Mission.
Elimu ya madrasa iliwahusu Waislamu pekee, lakini shule za serikali na shule za Mission zilichukua watu wa dini zote bila ubaguzi wowote.
Hivyo Watanzania wengi wa zamani waliobahatika kusoma elimu ya secondary, walisoma shule za misheni.
Kilichofanya Wakristo wengi zaidi kuwa ni wasomi kuliko Waislamu, ni changamoto ya ada za shule.
Watoto wa mikoa yenye mazao ya biashara, waliweza kusoma zaidi kwasababu wazazi wao waliweza kulipa ada, kutokana na kupata kipato, lakini watoto wa mikoa ambayo haikuwa na mazao ya biashara ikiwemo mikoa yote yenye Waislamu wengi, hawakubahatika kupata elimu ya kisasa.
Hali hii ilipelekea hata uendeshaji wa harakati za uhuru, kuongozwa na wasomi Wakristo, mfano vyama vyote vya siasa vilivyopigania uhuru, kuanzia AA kiliongozwa na Mkristo, Cecil Matola, TAA ikaongozwa na Dr. Vedastus Kyaruzi na TANU ikaongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kitu kizuri sana Shule za Mission zilichowafanyia Watanzania, akitokea Mwanafunzi very bright, akafanya vizuri mitihani yake na kufaulu vizuri, wale waalimu wa shule za Mission, usually makasisi, waliwachukua watoto hao na kuwasomesha bure, hivyo ndio wengi wa wasomi wa Kiislamu walivyopatikana, hivyo watu kama Juma Mwapachu na nduguye Bakari, kina Hamza Aziz, Inspector Rashid na Waislamu wengi wa enzi hizo, walisoma sekondari kwa hisani ya Shule za Mission.
Hisani hii, sio kwa ndugu zetu Waislamu pekee, hata Wakristo kutoka maeneo ambayo hawana mazao ya biashara, hivyo umasikini wa kipato unasababisha watoto wao hawezi kulipiwa ada, na kutosoma sana.
Hivyo wasomi wa mikoa ya Singida na Dodoma, kama kina John Samwel Malecela na nduguye Job Lusinde, washukuru sana Mission, vinginevyo bila hisani ya Shule za Mission, kuna watu wangeishia kuchunga mbuzi au kupiga dufu au kuadhini tuu lakini sasa ni wasomi wazuri na waandishi mahiri kwa hisani ya Shule za Mission.
Hivyo hili ni bandiko la kuwakumbusha ndugu zetu Waislamu waliofaidika na hisani ya kusomeshwa shule za Mission, wakumbuke fadhila, wawe ni watu wa shukrani, wawashukuru sana Wakristo, wazishukuru shule za Mission walizosomea, na kuwashukuru wale Makasisi waliowaokoa.
Ukifadhiliwa, usiwe mtovu wa fadhila, haiwezekani mtu ufadhiliwe shule za Mission, halafu kila uchao ni kuwabeza tuu Wakristo na kuwatukuza Waislamu, mara kulalamikia mfumo Kristo, mara kulalamika....
Inaendelea
Paskali