Kadhi Mkuu 1
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 19,687
- 23,689
Kwani kuku na ng'ombe wameumbwa kumwabudu Allah?Majini wanatupa utajiri bwashee, kwann tusishirikiane nao?
Wao pia ni viumbe wa Allah
Mbn wengine wanafuga kuku na ng'ombe?
Jibu swali Kwanza mkuuHii ina uhusiano gani na majini mkuu?
Kila kiumbe kinamwabudu Allah, Hata jua linanwabudu AllahKwani kuku na ng'ombe wameumbwa kumwabudu Allah?
Mbona wewe unakwepa swali langu mkuu?Jibu swali Kwanza mkuu
Lile jua linalozama kwenye matope ama jua gani ?Kila kiumbe kinamwabudu Allah, Hata jua linanwabudu Allah
Mkuu Imani si sayansi kwamba unaweza kudhibitisha kila kitu,ndio maana Kwa mfano katika Dini yangu ya Uislamu,kuna Aya inasema ''enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga kama walivyofunga wenzenu waliopita ili mpate kuwa wacha mungu'' hapo wanatakiwa wale walioamini TuUnaweza kuthibitisha haya yalitokea kweli na si stories za watu tu?
Jibu ninalo Ila Nataka nione mantiki ya uelewa wako juu ya swali nililo uliza Ila kama huna jibu niambieMbona wewe unakwepa swali langu mkuu?
Wewe mtazamo wako ni UPI mkuu?Kulikuwa na ubishi mtaani kukawa na pande mbili moja ikisema majambazi,wachawi,wezi...huwa wanamuomba mungu na kupewa na upande wa pili ukisema mharifu au mtenda dhambi huwezi kupewa/ruhusiwa na mungu kwa uhalifu wake.
Sent from my BBF100-6 using JamiiForums mobile app
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]Ngoja tuone masheikh mkipeana ilmu.
Mkuu nilishawahi kukwambia wewe mjanja Sana WA manenoKwa nini swali liwe "umeumbwa na nani?"
Huoni kwamba hata swali lako limelenga kwenye jibu unalolitaka?
Umekuta jani la muembe mlangoni mwako, unauliza "Mmasai gani kaweka hili jani la muembe hapa mlangoni mwangu?".
Unajuaje aliyeweka hilo jani ni Mmasai?
Kwa nini swali lako liulize Mmasai?
Kwa nini swali lako lilenge kwenye "nani?"
Hilo hiloLile jua linalozama kwenye matope ama jua gani ?
Unafuga majini ila unaona haramu kitimoto🤣🤣😀Majini wanatupa utajiri bwashee, kwann tusishirikiane nao?
Wao pia ni viumbe wa Allah
Mbn wengine wanafuga kuku na ng'ombe?
Kitimoto amekatazwa hata kwenye biblia.Unafuga majini ila unaona haramu kitimoto🤣🤣😀
Imani unaruhusiwa kuamini chochote, ukweli, uongo, mchanganyiko wa ukweli na uongo, vitu visivyokuwepo, vilivyopo na kadhalika.Mkuu Imani si sayansi kwamba unaweza kudhibitisha kila kitu,ndio maana Kwa mfano katika Dini yangu ya Uislamu,kuna Aya inasema ''enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga kama walivyofunga wenzenu waliopita ili mpate kuwa wacha mungu'' hapo wanatakiwa wale walioamini Tu
Ninachotaka kusema Imani ndio mtihani ambao wanadamu tumepewa,tuamini yasiyo onekana maadamu yasemwa na Muumba wetu
Uamuzi ni wetu,kama wewe ulivyoamini hakuna Mungu
Hoja hapa si ujanja wa maneno. Hapo kuna hoja ya kimantiki iliyo na msingi kuliko ujanja wa maneno.Mkuu nilishawahi kukwambia wewe mjanja Sana WA maneno
Labda nibadilishe swali ''wewe asili yako ni ipi au umetokana na nini''
Mkuu Kwanza nakupa kongole Kwa maelezo yako yenye mifano mingi,ungekuwa Mwalimu naamini wanafunzi wako wangenufaika SanaHoja hapa si ujanja wa maneno. Hapo kuna hoja ya kimantiki iliyo na msingi kuliko ujanja wa maneno.
Unaponisema mimi ni mjanja wa maneno unanifanya nionekane kama mtu asiye na hoja ya msingi ya kimantiki (logic), lakini anayejua kuhadaa watu kwa kupanga maneno (rhetoric).
Hili si kweli. Nina hoja ya msingi ya kimantiki ambayo umeshindwa kuijibu. Kwa hivyo usinidogoshe kwa kuniita mjanja wa maneno.
Polepole tunaelekea pazuri.
Tumeondoka kwenye swali lenye kasumba (bias), tunaelekea kuuliza swali la msingi.
Kwanza kabisa, naweza kukuambia kwamba, nikijua mantiki fulani ya msingi, sihitaji kujua jibu la swali fulani ili kujua kwamba jibu jingine si jibu sahihi.
Kwa mfano, naweza kujua kwamba square root ya namba nzima yoyote ni lazima iwe ndogo kuliko namba yenyewe. Hii ni mantiki ya msingi ya kihesabu.
Nikijua mantiki hii, mtu akiniambia square root ya 2 ni 10, naweza kukataa mara moja, nikamwambia mtu huyu kwamba square root ya 2 haiwezi kuwa 10, kwa sababu 10 ni kubwa kuliko 2. Hata bila kujua square root ya 2 ni nini.
Nitoe mfano mwingine ambao utaeleweka zaidi kwa watu wasiooenda kusikia "square root".
Tukijua kwamba mama mzazi wa mtoto ni lazima awe mkubwa kuliko huyo mtoto, halafu tukaambiwa kwamba, kuna mwanamme wa miaka 30 leo, ambaye mama yake mzazi ni binti mchanga wa miezi 6 leo, yani tukiambiwa huyu binti mchanga ambaye ana miezi 6 leo ndiye mama mazazi aliyemzaa huyu mwanamme mwenye miaka 30 leo, tunaweza kukataa katakata na kusema hilo jambo haliwezekani kuwa kweli.
Kwa nini tunaweza kukataa kwamba huyu binti wa miezi 6 keo ndiye mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30? Kwa sababu tunajua mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 ni lazima alikuwapo miaka 30 iliyopita kumzaa huyi mwanamme, na hivyo hawezi kuwa binti wa miezi 6 leo.
Hatuhitaji kumjua mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo ili kujua kwamba huyu binti wa miezi 6 leo si mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo.
Hatuhitaji kujua jibu sahihi la swali fulani ili kujua jibu fulani si sahihi.
Sihitaji kujua asili yangu ni nini ili kujua kwamba jibu la Mungu si jibu sahihi.
Ukichofanya hapo ni kama vile mimi nakuambia mtu mzima wa miaka 30 leo hawezi kuwa na mama mzazi mwenye miezi 6 leo, kwa sababu that is not logically cinsistent, halafu wewe bado unaniukiza "sasa kama huyu binti wa miezi 6 leo si mama mzazi wa huyu mtu mwenye miaka 30 leo, mama mzazi wa huyu mtu mwenye miaka 30 ni nani?"
Swali lako ni irrelevant kwenye hoja yangu.
Hoja yangu si kwamba mimi najua asili yangu ni nini. Hili ni swali tofauti, tutatafiti mpakantujue. Tatizo watu wengi wanatakankulazimisha majibu, hawawezi kusema hapa hatujui tutafiti tujue.
Hoja yangu ni kwamba asili yangu haiwezi kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote. Kwa sababu, Mungu huyo hayuko logically consistent na ulumwengu tunaouona.
Nakwambia mwanamme wa miaka 30 leo hawezi kuwa na mama mzazi aliye na miezi 6 leo. Kwa sababu hili halina logical consistency.
Unaniuliza, sasa mama mzazi wa huyu mwanamme ni nani?
Hiyo si hoja yangu. Sijawahi kusema namjua mama mzazi wa huyu mwanamme mwenye miaka 30 leo, nimesema mama yake mzazi si huyo binti mwenye miezi 6 leo.
Sihitaji kumjua mama mzazi wa huyu mwanamme mwenye miaka 30 leo ili kujua kwamba huyu binti wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa huyo mwanamme.
Vivyo hivyo, sihitaji kujua asili yangu ili kujua jibu la kwamba asili yangu ni Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote si jibu la kweli.
Kwa kuangalia logical consistency tu.
Asante mkuu.Mkuu Kwanza nakupa kongole Kwa maelezo yako yenye mifano mingi,ungekuwa Mwalimu naamini wanafunzi wako wangenufaika Sana
Umesema hauhitaji kujua asili yako na hii inaweza kutokana na ukweli kwamba unajua kabisa huwezi jua asili yako hata ufanye utafiti kiasi gani
Hudhani kwamba option pekee iliyobaki inaleta taswira kwamba kuna injinia ambaye ndo atakuwa designer WA kila kitu?
Asante mkuu.
Kwanza kabisa, sijasema kwamba sihitaji kujua asili yangu.
Nimesema kwamba sihitaji kujua asili yangu ili kujua kwamba asili yangu si Mungu.
Kuna tofauti hapo.
Na nimesema watu wengi hawataki kusema kwamba hili hatulijui, tulifanyie utafiti zaidi. Wakiona kitu hawakijui, wanaweka jibu rahisi la Mungu. Nikasema tunachotakiwa kufanya ni kufanya utafiti mpaka tujue jibu la kweli.
Kwa hivyo sijasema kwamba siwezi kujua asili yangu hata nifanye nini.
Na hata ningesema hivyo, kutokujua asili yako ni nini hakumaanishi asili yako ni Mungu.
Kutokujua asili yako ni nini maana yake hujui asili yako ni nini. Usifanye kitu kinachoitwa "argument from ignorance" kwamba, kwa sababu hujui jibu la swali, basi lazima jibu ni Mungu. Kama hujui hujui tu, hilo halimaanishi jibu ni Mungu.
Halafu pia, ukiweka hoja ya kwamba kila kilicho complex ni lazima kimeumbwa na injinia wake, huoni kwamba hapo unatuletea swali la kuhoji huyo Mungu wako naye injinia wake aliyemuumba ni nani, na injinia wa injinia wake ni nani?
Na kama Mungu naye atahitaji injinia, je, huyo kweli ni Mungu?
Kama hahitaji injinia, je, hoja yako ya kwamba kila kilicho complex kinahitaji injinia ina mashiko?
Ukishakubali kwamba Mungu hana mwanzo wala mwisho, umeshalibatilisha swali la kuuliza injinia kwa yeyote, kwa sababu ushaonesha kwamba inawezekana kilicho complex kikawepo bila ya injinia wake kuhitajika au kukiumba.Kiukweli kabisa mambo ya Imani yatabakia kuwa ya Imani
Kuna kitu uligusia hapo kuwa kama kila kitu complex kitahusishwa na Mungu ambaye ndio injinia inamaana huenda ukajiuliza je na injinia WA Mungu ni Nani?
Kwa jibu Hilo Kwa Imani yangu inasema kwamba Mungu Hana mwanzo wala mwisho,hakuzaliwa wala hakuzaa,Kwa maana nyingine Mungu amekuwepo siku zote,Kwa atheist kama wewe najua inakupa ukakasi kidogo.
Sasa naomba tuje kwenye engo hii
Siku zote huwa unasisitiza upate udhibitisho kama Mungu yupo lkn kuna vitu ambavyo hatuvioni lakini vipo,Kwa mfano Upepo hatuuoni lkn upo,je huoni kwamba Mungu hatumuoni lakini anajidhihirisha katika namna nyingine ingawa hatuweki umakini kuligundua Hilo?