Waislamu Mnafeli wapi?


Hilo la Uhuru WA kuchagua kuzaliwa au kutochagua naomba tulipe time out Kwanza!

Tuje kwenye hoja yako ya Mungu na ulimwengu WA mabaya

Mungu yupo na ulimwengu WA mabaya upo, mabaya mengi yanatokana na kazi za mikono yetu Sisi wenyewe

Sisi ndio chanzo cha kuleta mazingira ya ubaya,wanadamu wamekuwa wakimuasi Mungu miaka na Miaka na hivyo kumpelekea Mungu muweza wa yote kutuletea majanga mbali mbali hapa duniani au kuruhusu ubaya utufikie kama malipo ya ubaya wetu tunao ufanya,au saa nyingine ukaidi tunao ufanya dhidi ya kuasi amri zake

Mfano Wana wa Israel waliachwa kutangatanga jangwani Kwa Mda wa miaka arobaini (40) na kupata dhiki kutokana na ukaidi wao

Kuna ambao waliletewa vimbunga,kuna ambao waliletewa ukame,na kuna ambao waliletewa gharika na listi inaendelea

Unaweza vile vile kujiuliza kwanini Mungu aliruhusu shetani kuja hapa duniani,Kwanza shetani/ iblis baada ya kuhukumiwa kuingia Motoni,aliomba apewe umri mrefu WA kuishi hapa duniani na alimwambia Mungu kuwa atawapoteza waja ili aingie nae Motoni,lakini pamoja na hayo Mungu alimpa Mda wa kuishi lakini alimwambia wewe huna mamlaka ya kuwapoteza waja wangu walioamini kweli kweli isipokuwa wale wanaotaka wenyewe.

Kwahiyo shetani yupo na mambo yake lakini anawaingiza watu katika mabaya Kwa hiari Yao wenyewe,hatushindi nguvu wala hawezi kutulazimisha kwani nguvu hizo Hana,Bali ni Sisi wenyewe ndio tuna hiari ya kujiunga nae au laa!

Lakini wakati mwingine mabaya yanatufikia kama mpango WA kuyafikia Yale ambayo yalikuwa yatufikie au tufikie katika daraja Fulani.

Mfano Nabii Yusuph alipatwa na mabaya ya kutaka kuchinjwa na ndugu zake,ingawa baadae waliamua kumtupa kwenye kisima,lakini kwakuwa ulikuwa mpango wa mungu hakupata madhara yoyote,akachukuliwa na wasafiri na kuuzwa kama mtumwa na mwisho wa siku kwa kufupisha maelezo alikuja kuwa kiongozi mkubwa WA misri,kwahiyo Kwa kila changamoto au ubaya unaotukuta nyuma yake kuna neema ambayo itatufikia,ni kama mfano wa dhahabu inapatikana baada ya kupitishwa Motoni Kwanza

Kwahiyo Mungu yupo na ubaya upo.
 
Fikiria kabla ya sisi kuwepo.

Mungu yuko yeye tu.

Ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Ana uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea.

Kwa nini hajaumba ulimwengu huo ambao mabaya hayawezi kutokea, kaumba ulimwengu huu ambao mabaya yanaweza kutokea?
 
Mungu ana mpango wa kila kitu au WA kila Jambo
Huo ulimwengu unao sema unakuja huko mbeleni mara baada ya kumaliza Maisha ya hapa duniani

Huko kutakuwa hakuna mabaya wala maradhi,hakuna uzee hakuna kufa,kifupi watao jaaliwa au watao faulu katika ulimwengu huu hao ndio watauona huo ulimwengu mpya

Kwahiyo alipanga mambo yake hata kabla hatujaumbwa sisi
 
Kusema Mungu ana mipango yake si jibu, kwani mimi wapi nimesema hana mipango yake?

Hujajibu swali langu.

Huwezi kujibu swali hilo.

Kwa sababu Mungu huyo hayupo.

Huyo Mungu ni character katika hadithi ya kutungwa na watu tu.

Ndiyo maana hadithi imejaa logical inconsistencies na contradictions.

Ndiyo maana nikikubana umuelezee huyo Mungu unakosa majibu.

Unaishia kusema Mungu ana mipango yake.

Mungu kaumba ulimwengu unaotesa watu, wakati ana uwezo wa kuumba ulimwengu usiotesa watu, huyo Mungu wako ni sadist?
 
Kama huo ulimwengu mzuri upo kulikua na haja gani ya yeye kuweka na ulimwengu huu wa mateso?
 
Mkuu unajua kuna tatizo moja naliona kwako

Kuna Mungu Fulani ambaye umemtengeneza wewe kichwani mwako sasa hata ukiambiwa Kwa mfano kuwa kuna Maisha ya huko mbeleni ambayo yatakuwa na Amani Bila mabaya wewe bado haitaingia akilini mwako

Unatamani Mungu asingeruhusu ubaya hapa duniani lkn hivi Ni vitu ambavyo vipi nje ya uwezo wetu,kwani yeye anafanya alitakalo na hashurutishwi na mtu

Kwahiyo kwako wewe Kwa majibu yoyote utakayo pewa bado hutaona ni majibu

Any way huu ni mjadala ambao Una pande mbili zenye mtazamo tofauti,tunatarajia kutofautiana kutokana na namna tunavyo yachukulia mambo au tunavyoyaelewa au tunavyo yaamini.
 
Kama huo ulimwengu mzuri upo kulikua na haja gani ya yeye kuweka na ulimwengu huu wa mateso?
Ulimwengu huo lazima ulipie gharama

Gharama yake ni kuwa mcha Mungu

Fanya mema na Acha mabaya
 
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote atubanie maisha mazuri, ayaweke huko mbele, asitupe maisha mazuri hayo sasa, atupe mateso makubwa sana?

Nimekuuliza swali hili, hujajibu.

Pia, hayo maisha ya huko mbeleni huwezi kuthibitisha yapo.

Au unabisha?

Unaweza kuthibitisha maisha ya huko mbeleni yapo kweli?

Maana naona nakuhoji kuhusu uongo mmoja (kuwapo kwa Mungu), unashindwa kujibu maswali, unatengeneza uongo mwingine (maisha ya huko mbeleni) ambao pia huwezi kuthibitisha kwamba ni kweli.

You are building a house of cards. Mungu wako ni wa uongo, hayupo, ndiyo maana katika kutetea uwepo wake, inakubidi uongeze uongo mwingine kama huo wa habari za "maisha ya mbeleni", uongo ambao nao huwezi kutuonesha kwamba ni ukweli.

Mpaka sasa.

1. Hujathibitisha Mungu yupo.
2. Hujaeleza kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu mabaya.
3. Hujathibitisha hayo maisha ya mbeleni yapo kweli na si hadithi za watu tu.
4. Hujaeleza utasemaje tuna uhuru, wakati hatuna uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe, hatuna uhuru wa kuchagua tuzaliwe wapi, lini, na wazazi gani, na vinasaba gani etc.

Umeshindwa kujenga hoja ya kimantiki kutetea uwe[o wa huyo Mungu, kwa sababu hayupo, huyo Mungu ni character wa hadithi za kutungwa na watu tu.
 
Si tulikubaliana kuna majini wazuri na wabaya..leo wewe unasema majini wote wabaya..utakua muislamu wa mchongo wewe.

#MaendeleoHayanaChama
Kwani majini walitoka wapi??

Kulingana na imani yangu walitupwa huku duniani wakiwa pamoja na shetan

Sasa iweje useme wapo wazuri na wabaya?? Jini ni jini tu mkuu

Au kuna majini wataenda mbinguni??
 
Kile unachosema uongo ni kile ambacho hujakiamini Hilo ndio jibu sahihi

Atheist wengi mnakataa uwepo wa Mungu kwakuwa mnaamini sayansi ndio ina majibu ya kila kitu,wakati kiuhalisia haitoi maelezo Kwa kila kinachotokea hapa duniani

Msingi wenu mkubwa ni kuwa dunia na viliomo ndani yake ni matokeo ya mabadiliko ambayo yalianza kutokea miaka mingi iliyopita ndio mpaka akaja kupatikana mwanadamu,lakini mabadiliko ni process basi tungetegemea mwanadamu abadilike na kuwa kiumbe kingine tena,lakini mpaka Leo hatujaona Hilo hapo INA maana sayansi imefeli

Na ndio maana hata mkiambiwa kuna Maisha mengine baada ya haya bado mtakataaa kwasababu hamjapata evidence kutoka katika Sayansi,kama sayansi imeshindwa kudhibitisha evolution kuendelea basi haitaweza pia kudhibitisha uwepo wa ulimwengu mpya

Ndio tunarudi pale kuwa maelezo pekee ambayo yamenyoka na hayana Shaka ni kutoka Kwa Mungu muweza wa yote ambaye ndio muumbaji WA kila kitu
 
Lengo
Kulikuwa na haja ya yeye kutuwekea hizo gharama? lengo la hizo gharama ni nini? kutuchuja? kwa nini atuchuje?
Lengo ni kupata viumbe watiifu ambao wamefuata amri za Mola wao walipwe Kwa matendo Yao mema

Na

Wabaya walipwe Kwa matendo Yao,kwenda motoni
 
Kwa swali ulilouliza hapo juu

Mungu alitupenda na ndio maana akatupa bustani ya edeni tuishi ndani yake tukila na kufanya chochote bila kutumia nguvu kubwa. Lakini alitoa maagizo ya kwamba katika bustani hiyo kuna mti wa ujuzi wa mema na mabaya kwa hivyo msiule

Basi uasi ukaingia na ndipo akasema kwamba hakika mtakula kwa jasho(wanaume) na mtazaa kwa uchungu( wanawake)
*MWANZO 3:17-20

Lakini Kama tunavyofahamu ya kuwa Mungu wetu ni pendo mwingi wa rehema alitupenda tangu mwanzo japo tulitanga mbali nae ila yeye katuonesha upendo
Na ndipo akasema nitamtuma mkombozi aje awakomboe katika dhambi na mateso mnayopata huko duniani.. (Mwanae wa pekee)

Na hta hivyo ukisoma kitabu cha Danieli, alitabiri kuhusu yatakayo ikumba dunia hii huko mbeleni ambao muda huo ni sasa na kwa sababu Mungu etu ni pendo basi akasema nitawakomboa katika ulimwengu huu wa dhambi kama mkinitumainia. Akaahidi kutupa uzima wa milele kwa wale washindi wa dhambi.


*WARUMI 1:28
*1YOHANA 3,1-4

[emoji120]
 
Nakwambia hivi.

1.Hujathibitisha Mungu yupo.
2. Hujaeleza kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba dunia inayoweza kuwa na maovu, wakati aliweza kuumba dunia isiyowezekana kuwa na maovu.
3. Unajitahidi kujibu kwa kusema kuna maisha huko mbeleni.Hujathibitisha kuna maisha huko mbeleni.
4. Hujaeleza kwa vipi tuna uhuru wa kuchagua wakati hata hatuchagui tunazaliwa au hatuzaliwi, tunazaliwa wapi, lini, na wazazi gani etc.

Huwezi kujibu maswali haya in a logically consistent way, kwa sababu huyo Mungu unayemsema hayupo, ni wa kutungwa na watu tu. Ni wa uongo tu.

Ndiyo maana huyo Mungu anabaki kuwa jambo la imani, hayupo, hawezi kuthibitishika yupo, kwa sababu hayupo.

Ni suala la kujidanganya yupo kwa imani tu.
 
Kwa nini Mungu hakuumba dunia ambayo uasi hauwezekani kuwapo na wala haujulikani ni nini, akaamua kuumba ulimwengu ambao uasi unawezekana?
 



Majibu ya maswali yako
1. Hapo mwanzo alikuwepo neno...
YN 1:1-14
Pia
MWANZO 1:1

I' m a scientist
Huwezi kusema kwamba earth evoluved from Solar nebula 4.5b years ago halafu sasa nakuuliza ya kwamba where do that heat came from iliyoisaidia earth kuform?
Au gravity nayo ilitokana na evolution? Je earth's movement ni evolution? Je hiyo solar nebula ilitoka wapi?
Kama wewe n mwansayansi kweli hebu define Nature kwa ufasaha

Kama kila kitu kilitokana na evolution process, na je ni kwa namna gani binadam aliweza kuongea na kuwa na ufahamu? Kupitia hiyo evolution process?

Na kwanini tunakufa kama kuna evolution process kwanini tusirudi kwa ma ancestral wetu wa zamani? Au tuevolve tiwe kiumbe mwingine??

*MWANZO 2:17
Kama tulitokana na evolution kwanini tuvute pumzi? Na tuitegemee kwa maisha yetu yote? Nafikiri kwa kuwa tulitokana na evolution hakukuwa na namna ya kutumia hii pumzi ya uhai


2. Mwenyezi mungu alipoumba kila kitu aliona ya kuwa ni chema na cha kuvutia machoni pake hivyo akamkabidhi mwanadamu kila kitu akitawala kila kiumbe, kiwe chini yake huku akiwa na agizo moja tu la kutokuugusa ule mti wa kati kati na alipofanya hivyo akawa kinyume na mungu
*MWANZO 3:7-10
Kwa hivyo mungu aliwapa kila walichohitaji isipokuwa ufahamu wa mema na mabaya na aliwapa kama agizo la kupima utii wao kwake


3. Soma kitabu cha danieli vyema utaelewa kila kitu kilichotabiriwa na Danieli yote na malizia kwa kusoma ufunuo yote


4. *KUTOKA 20:12
Hauwezi kuwa na uhuru wa kuchangua nchi uitakayo, labda nikuulize ulipokuwa mdogo uliweza kuchagua kunyw amaji badala ya maziwa? Au kula ugali badala ya kunyonyeshwa?
Kama hukuweza na basi hauwezi kujipangia mahali pa kuzaliwa na wala kuishi ila umepewa uhuru wa kufanya chochote kile katika dunia hii kwa maana siku zetu si nyingi hapa duniani au kuna mtu anakupangia namna ya kupumua au anakupimia kiasi cha oksijeni unachopaswa kutumia kwa siku??

Nakuuliza tena
Kabla hujazaliwa ulikuwa hai?? Kwa maana maswali yako yanaonyeaha ya kuwa ulizaliwa tu kwa bahati ila ulikuwa hai kabla hata hujazaliwa.

Ni hayo tu kwa leo
 
Kwa nini Mungu hakuumba dunia ambayo uasi hauwezekani kuwapo na wala haujulikani ni nini, akaamua kuumba ulimwengu ambao uasi unawezekana?
Aliufahamu uasi na ndio maana akawatolea wanadamu ujuzi wa mema na mabaya ili wasijue uasi na mabaya wala mema wao waishi tu kama viumbe wengine
Na hapo kilikuwa ni kipimo cha utii kwa viumbe aliowaumba kwa mfano nikuulize swali
Je mwanao anaweza kuwa na sauti katika familia kukuliko wewe??
 
Kongole Kwa kuongezea nyama zaidi katika majibu yako
 
Hujajibu swali nililouliza, umeleta mambo ya evolution ambayo mimi hata sijayasema.

Halafu umekubali kwamba hatukupewa uhuru wa kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe, kimsingi suala zima la kwamba tuna uhuru wa kuchagua linayeyuka hapo.

Mungu kumfanya mtu ajikute amezaliwa tu, bila ya kukubali kuzaliwa, ni kumnyima huyo mtu uchaguzi wa kuamua azaliwe au asizaliwe. Na hivyo, chochote kitakachotokea katika maisha hayo, huyo mtu hawezi kusemwa kwamba ana uhuru wa kuchagua.

Hana hata uhuru wa kuchagua azaliwe au asizaliwe!

Utasemaje ana uhuru katika kuzaliwa huko?

Yani umemfanya mtu mtumwa, kajikuta yuko shambani kwako. Halafu unasema mtumwa huyu ana uhuru wa kuchagua kulima au kumwagilia maji shamba.

Wakati hata hujamuuliza kama anataka kuwa mtumwa au hataki.

Sasa hapo napo unasema huyu mtumwa ana uhuru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…