Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
- Thread starter
- #301
Nakwambia hivi, kama Adam na Hawa hawakuulizwa waumbwe au wasiumbwe, wakajikuta wameumbwa tu, baada ya hapo huwezi kusema wamepeea uhuru.
Kwa sababu, uhuru wowote watakaopewa umechorewa mistari, wameshazaliwa, hawakuwa na nafasi ya kukataa kuzaliwa.
Ni sawa na kauli ya kumtuhumu mtengeneza magari wa Marekani Ford. Ford aliulizwa kama watu wana uhuru wa kuchagua rangi yoyote wanayoitaka kwenye magari anayotengeneza ya Model T. Ford akasema watu wanaweza kuchagua rangi yoyote, ili mradi rangi wanayochagua iwe nyeusi.
Nikikwambia unaweza kuchagua gari la rangi yoyote, ilimradi hiyo rangi iwe nyeusi, hapo nimekupa uhuru wa kuchagua rangi au nimekuchagulia?
Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu unaoruhusu mabaya.
Ama ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, na Mungu huyo hayupo.
Ama huyo Mungu yupo, na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo.
Viwili hivi haviwezi kuwapo pamoja vyote, that is a logical contradiction.
Tunaona ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.
Hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Hilo la Uhuru WA kuchagua kuzaliwa au kutochagua naomba tulipe time out Kwanza!
Tuje kwenye hoja yako ya Mungu na ulimwengu WA mabaya
Mungu yupo na ulimwengu WA mabaya upo, mabaya mengi yanatokana na kazi za mikono yetu Sisi wenyewe
Sisi ndio chanzo cha kuleta mazingira ya ubaya,wanadamu wamekuwa wakimuasi Mungu miaka na Miaka na hivyo kumpelekea Mungu muweza wa yote kutuletea majanga mbali mbali hapa duniani au kuruhusu ubaya utufikie kama malipo ya ubaya wetu tunao ufanya,au saa nyingine ukaidi tunao ufanya dhidi ya kuasi amri zake
Mfano Wana wa Israel waliachwa kutangatanga jangwani Kwa Mda wa miaka arobaini (40) na kupata dhiki kutokana na ukaidi wao
Kuna ambao waliletewa vimbunga,kuna ambao waliletewa ukame,na kuna ambao waliletewa gharika na listi inaendelea
Unaweza vile vile kujiuliza kwanini Mungu aliruhusu shetani kuja hapa duniani,Kwanza shetani/ iblis baada ya kuhukumiwa kuingia Motoni,aliomba apewe umri mrefu WA kuishi hapa duniani na alimwambia Mungu kuwa atawapoteza waja ili aingie nae Motoni,lakini pamoja na hayo Mungu alimpa Mda wa kuishi lakini alimwambia wewe huna mamlaka ya kuwapoteza waja wangu walioamini kweli kweli isipokuwa wale wanaotaka wenyewe.
Kwahiyo shetani yupo na mambo yake lakini anawaingiza watu katika mabaya Kwa hiari Yao wenyewe,hatushindi nguvu wala hawezi kutulazimisha kwani nguvu hizo Hana,Bali ni Sisi wenyewe ndio tuna hiari ya kujiunga nae au laa!
Lakini wakati mwingine mabaya yanatufikia kama mpango WA kuyafikia Yale ambayo yalikuwa yatufikie au tufikie katika daraja Fulani.
Mfano Nabii Yusuph alipatwa na mabaya ya kutaka kuchinjwa na ndugu zake,ingawa baadae waliamua kumtupa kwenye kisima,lakini kwakuwa ulikuwa mpango wa mungu hakupata madhara yoyote,akachukuliwa na wasafiri na kuuzwa kama mtumwa na mwisho wa siku kwa kufupisha maelezo alikuja kuwa kiongozi mkubwa WA misri,kwahiyo Kwa kila changamoto au ubaya unaotukuta nyuma yake kuna neema ambayo itatufikia,ni kama mfano wa dhahabu inapatikana baada ya kupitishwa Motoni Kwanza
Kwahiyo Mungu yupo na ubaya upo.