Waislamu Mnafeli wapi?

Waislamu Mnafeli wapi?

Sio kashawapanga ila anawafahamu wale wa kuingia katika lile ziwa la moto

Basi kwa kuwa kila mmoja ana uhuru wa kufanya kila anachokipenda
Na ndivyo hivyo ya kuwa Mungu anawajua walio wake
Na siku ya mwisho atatenga wanakondoo mkono wa kuume na Mbuzi mkono wa kushoto,
Pia hata kama M/Mungu amekuandika katika wale watakaoingia motoni ila ukaamua kuacha dhambi na matendo maovi basi anakurehemu na kusamehe dhambi zako.

#Nawafahamu walio wangu
Mkuu unachokifanya ni kupingana na tulichokubaliana awali..hebu twende taratibu..
tumekubaliana kwamba mungu ndiye anayepanga kila kitu na hakuna kinachoweza kwenda kinyume na mapenzi yake si ndio?

tukakubaliana kwamba fate ya mwanadamu inakua determined na mungu si ndio?
sasa kwa muktadha huo ,nikihitimisha kwa kusema mtu aliyeuwawa kwa sababu ya wizi ,fate yake ni mungu ndie kaipanga, Tunakubaliana?
 
Siwi hai kabla ya kuzaliwa.

Na mimi nakuuliza swali.

Mungu wako muweza yote alishindwa kutupa uchaguzi kuhusu kuzaliwa, kabla hatujazaliwa na kuwa hai?

Alishindwa kutuonesha "haya maisha, ukikubali kuzaliwa utakutana na hili na lile, kuna kufa, kuna magonjwa, kuna njaa na kushiba, kuna vita na raha, nataka uishi hivi, usiishi vile, unakubali kuzaliwa?" au hukubali?"

Kwa nini hakutupa nafasi hiyo?

((Naomba nikuulize tena

Kama huwi hai kabla ya kuzaliwa, na unahitaji kupewa nafasi ya kuchagua yale utakayo sasa utachaguaje kama hauko hai??))

Nimekoti statement ya Mr bigger kwasababu ndio swala ambalo nilitaka kulisema.

Kwakuongezea

Kama haukuwa hai inamaana automatically hatuwezi kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe,yaani Sawa Sawa na hatukuwepo kabisa au hakukuwa na mpango wa kuwepo kabisa.

Lakini pili kama tungekuwa hai basi tungeweza kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe.

Kwakumalizia kama hakuna Uhai kabla ya kuzaliwa basi hakuna haki ya kuchagua kuzaliwa au kutozaliwa
 
Sasa niambie aliyeruhusu uwepo wa hayo matendo mabaya(Vishawishi) ni nani?
Mkuu baada ya Mungu kutuumba alituelekeza lipi jema na lipi Baya,kisha na akatuambia kabisa tuache mabaya na kufuata mema.

Na

Akatuambia malipo ya wafanyao mabaya na malipo ya wafanyao mema

Kwahiyo mwanadamu alipewa elimu ya kutosha,kilichobakia ni kwake yeye kuamua ipi ni njia sahihi ya kufuata
 
Cornwallis ni hivi

Mungu anajua mwanzo wetu na mwisho wetu,Kwa maana anajua kabla ya kuwepo kwetu na anajua hatima ya Maisha yetu itakuwaje huko mbeleni.

Anajua kabisa ni Nani mtu wa Motoni na yupi WA peponi,sasa kuna baadhi ya watu wanaulewa mbaya juu ya hii dhana,wanasema Mungu kashapanga tayar watu WA Motoni na peponi,kitu ambacho si kweli kwakuangalia mambo yafuatayo;

* Kama kweli Mungu alishapanga hayo basi kusingekuwa na haja ya kutuma Mitume na Manabii wake

*Kusingekuwa na haja ya kutuma vitabu vyake

* Wala kusingekuwa na haja ya kufanya ibada mbali mbali

Lakini vile vile Mungu angekuwa amefanya dhulma kubwa Sana Kwa viumbe wake,kitu ambacho sio sifa ya Mungu.

Kwahiyo Kwa kumalizia Mungu anajua Mungu anajua mwisho wa kila mmoja wetu itakuwaje

Kwa mfano

Kama Mimi nimeandikiwa mtu wa Motoni ( Mungu aepushie mbali amiin) hata nikiwa nafanya matendo mema Sasa ina maana Mungu anajua huko mbele nitabadilika na kuwa mtu muovu na Kwa hatima ya matendo yangu nitaangaamia na nitaenda kutimiza lile andiko la mwisho wangu.

Kwahiyo Mungu anayajua Yale tusiyo yajua Sisi.
 
((Naomba nikuulize tena

Kama huwi hai kabla ya kuzaliwa, na unahitaji kupewa nafasi ya kuchagua yale utakayo sasa utachaguaje kama hauko hai??))

Nimekoti statement ya Mr bigger kwasababu ndio swala ambalo nilitaka kulisema.

Kwakuongezea

Kama haukuwa hai inamaana automatically hatuwezi kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe,yaani Sawa Sawa na hatukuwepo kabisa au hakukuwa na mpango wa kuwepo kabisa.

Lakini pili kama tungekuwa hai basi tungeweza kuchagua tuzaliwe au tusizaliwe.

Kwakumalizia kama hakuna Uhai kabla ya kuzaliwa basi hakuna haki ya kuchagua kuzaliwa au kutozaliwa
Wakuu mbona mnaniangusha?

Mnaelewa kwamba kwa mujibu wenu Mungu anaweza yote na angetaka watu waulizwe kama wanataka kuishi kabla ya kuzaliwa, kabla ya kuwa hai, angeweza?

Au mnataka kusema Mungu wenu muweza yote angetaka kufanya hilo angeshindwa?

Na kama angeshindwa, kweli huyo ni Mungu muweza yote?

Mjue kwamba, uongo ukipimwa kwa logic mara nyingi unaishia kwenye fallacies, inconsistencies na contradictions.

Sasa hapa nawaonesha uongo wa kuwapo kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na anayewapa viumbe wake uwezo wa kuchagua unavyotupeleka kwenye inconsistencies, fallacies na contradictions. Ukichagua jibu lolote.

1.Ukisema Mungu katupa uchaguzi wa kuamua. Hili linatupeleka kwenye contradiction. Kwa sababu tunaona Mungu muweza yote ana uwezo wa kutupa uchaguzi tuamue tuzaliwe au tusizaliwe, lakini hakutupa uamuzi huo.

Hoja ya kwamba hakuweza kutupa uamuzi huo kwa sababu hatukuwa tumezaliwa ni hoja dhaifu. Ni hoja ya mtu anayeangalia ulimwengu huu tu kama ulimwengu unaowezekana. Ni hoja ya mtu anayempunja Mungu muweza yote nguvu zake za kuweza kumpa mtu uchaguzi wa kuamua kama anataka kuzaliwa kabla hata huyo mtu hajazaliwa.

Kama mnaamini Mungu anaweza kuhukumu watu baada ya watu kufa, kwa nini mnaona tabu kukubali kwamba Mungu huyu huyu angeweza kuwapa watu uamuzi wa kukubali au kukataa kuzaliwa kabla hawajazaliwa?

Mnaelewa kwamba mkikataa Mungu kuwa na uwezo huu wa kumpa mtu uwezo wa kuchagua kama anataka kuishi mmekataa kuwepo kwa Mungu mwenye uwezo wote na mmeanza kujiunga nami?

2. Ukisema Mungu ana upendo wote, tunarudi kwenye contradiction. Kama Mungu ana upendo wote kweli, kwa nini hakuwapa watu namna ya kufanya uchaguzi kama wanataka au hawataki kuzaliwa?

3. Ukisema watu wana uhuru wa kuchagua wanavyotaka kuishi, kuchagua mema na mabaya, tunarudi kwenye contradiction, watu wanakuwaje na uhuru wa kuishi watakavyo ikiwa hata suala la kuamua kuzaliwa au kutozaliwa hawana uamuzi nalo?

Contradictions all over.

Kwa nini?

Kwa sababu huyo Mungu hayupo. Ni character wa kutungwa na watu tu. Ni Mungu wa hadithi ya uongo.
 
Cornwallis ni hivi

Mungu anajua mwanzo wetu na mwisho wetu,Kwa maana anajua kabla ya kuwepo kwetu na anajua hatima ya Maisha yetu itakuwaje huko mbeleni.

Anajua kabisa ni Nani mtu wa Motoni na yupi WA peponi,sasa kuna baadhi ya watu wanaulewa mbaya juu ya hii dhana,wanasema Mungu kashapanga tayar watu WA Motoni na peponi,kitu ambacho si kweli kwakuangalia mambo yafuatayo;

* Kama kweli Mungu alishapanga hayo basi kusingekuwa na haja ya kutuma Mitume na Manabii wake

*Kusingekuwa na haja ya kutuma vitabu vyake

* Wala kusingekuwa na haja ya kufanya ibada mbali mbali

Lakini vile vile Mungu angekuwa amefanya dhulma kubwa Sana Kwa viumbe wake,kitu ambacho sio sifa ya Mungu.

Kwahiyo Kwa kumalizia Mungu anajua Mungu anajua mwisho wa kila mmoja wetu itakuwaje

Kwa mfano

Kama Mimi nimeandikiwa mtu wa Motoni ( Mungu aepushie mbali amiin) hata nikiwa nafanya matendo mema Sasa ina maana Mungu anajua huko mbele nitabadilika na kuwa mtu muovu na Kwa hatima ya matendo yangu nitaangaamia na nitaenda kutimiza lile andiko la mwisho wangu.

Kwahiyo Mungu anayajua Yale tusiyo yajua Sisi.
Je, kabla ya wewe kuzaliwa, Mungu anaweza kujua kwamba wewe unaishia motoni tu, halafu wewe ukapiga misele mpaka ukaingia mbinguni na kum prove Mungu kwamba alikuwa wrong kujua kwamba wewe utaishia motoni tu?

Zaidi ya yote, is it ethical kwa Mungu kuumba ulimwengu ambao kiumbe yeyote ataishia motoni tu, wakati angeweza kuumba ulimwengu ambao hakuna kiumbe atakayeishia motoni?
 
Wakuu mbona mnaniangusha?

Mnaelewa kwamba kwa mujibu wenu Mungu anaweza yote na angetaka watu waulizwe kama wanataka kuishi kabla ya kuzaliwa, kabla ya kuwa hai angeweza?

Au mnataka kusema Mungu wenu muweza yote angetaka kufanya hilo angeshindwa?

Na kama angeshindwa, kweli huyo ni Mungu muweza yote?

Mjue kwamba, uongo ukipimwa kwa logic mara nyingi unaishia kwenye fallacies, inconsistencies na contradictions.

Sasa hapa nawaonesha uongo wa kuwapo kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na anayewapa viumbe wake uwezo wa kuchagua unavyotupeleka kwenye inconsistencies, fallacies na contradictions. Ukichagua jibu lolote.

1.Ukisema Mungu katupa uchaguzi wa kuamua. Hili linatupeleka kwenye contradiction. Kwa sababu tunaona Mungu muweza yote ana uwezo wa kutupa uchaguzi tuamue tuzaliwe au tusizaliwe, lakini hakutupa uamuzi huo.

Hoja ya kwamba hakuweza kutupa uamuzi huo kwa sababu hatukuwa tumezaliwa ni hoja dhaifu. Ni hoja ya mtu anayeangalia ulimwengu huu tu kama ulimwengu unaowezekana. Ni hoja ya mtu anayempunja Mungu muweza yote nguvu zake za kuweza kumpa mtu uchaguzi wa kuamua kama anataka kuzaliwa kabla hata huyo mtu hajazaliwa.

Kama mnaamini Mungu anaweza kuhukumu watu baada ya watu kufa, kwa nini mnaona tabu kukubali kwamba Mungu huyu huyu angeweza kuwapa watu uamuzi wa kukubali au kukataa kuzaliwa kabla hawajazaliwa?

Mnaelewa kwamba mkikataa Mungu kuwa na uwezo huu wa kumpa mtu uwezo wa kuchagua kama anataka kuishi mmekataa kuwepo kwa Mungu mwenye uwezo wote na mmeanza kujiunga nami?

2. Ukisema Mungu ana upendo wote, tunarudi kwenye contradiction. Kama Mungu ana upendo wote kweli, kwa nini hakuwapa watu namna ya kufanya uchaguzi kama wanataka au hawataki kuzaliwa?

3. Ukisema watu wana uhuru wa kuchagua wanavyotaka kuishi, kuchagua mema na mabaya, tunarudi kwenye contradiction, watu wanakuwaje na uhuru wa kuishi watakavyo ikiwa hata suala la kuamua kuzaliwa au kutozaliwa hawana uamuzi nalo?

Contradictions all over.

Kwa nini?

Kwa sababu huyo Mungu hayupo. Ni character wa kutungwa na watu tu. Ni Mungu wa hadithi ya uongo.
Mkuu wenye akili wameanza kukuelewa taratibu kwa Logic zako, Hukurupuki unatoa "Hoja zenye Mashiko Halisi" Wao wanatoa Hoja zenye Mashiko ya kusadikika! Hatari sana.
 
Naendelea kusema kwamba
Mungu wetu ni pendo
Mwingi wa rehema alitupenda tangu mwanzo
Japo tulitanga mbali nae ila anatuonyesha upendo,
Ni wangapi wanaozaliwa na kufa?? Papo hapo Na wengine mimba zao zinatoka kabla hawajazaliwa?
Ila mungu katupenda sisi na ndio maana mpaka leo tupo hai
Kwa nini Mungu mwenye upendo wote na uwezo wote aumbe ulimwengu ambao mabilioni ya watu wataishia kwenda motoni, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao hakuna mtu atakayeishia motoni?
 
Mkuu wenye akili wameanza kukuelewa taratibu kwa Logic zako, Hukurupuki unatoa "Hoja zenye Mashiko Halisi" Wao wanatoa Hoja zenye Mashiko ya kusadikika! Hatari sana.
Nashukuru sana kuona kwamba kuna watu wameanza kuelewa kwamba hizi habari za kuwepo Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote zina contradictions nyingi sana.

Contradictions zinazotuonesha Mungu huyo hayupo.

Contradictions zinazotuonesha Mungu huyo ni character wa kutungwa katika hadithi ya uongo tu.
 
Mkuu baada ya Mungu kutuumba alituelekeza lipi jema na lipi Baya,kisha na akatuambia kabisa tuache mabaya na kufuata mema.

Na

Akatuambia malipo ya wafanyao mabaya na malipo ya wafanyao mema

Kwahiyo mwanadamu alipewa elimu ya kutosha,kilichobakia ni kwake yeye kuamua ipi ni njia sahihi ya kufuata
Unashindwa zoezi la kufikiri kwa fikra tunduizi na fikra dhahania.

Yani, fikra zako zinaishia kwenye ulimwengu uliopo.

Umeshindwa kujirudisha nyuma, wakati Mungu anataka kuumba ulumwengu.

Kabla ya kingine chochote kuwapo.

Kwa nini Mungu aliamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?

Kwa nini Mungu aone ni muhimu sana kuwapa watu mtihani wa kuchagua mabaya na mazuri, wakati angeweza kuwapa mazuri tu? Hususan kwa sababu kuna watu wengi sana watashundwa huo mtihani, na yeye Mungu ndiye anagawa neema ya nani atashindwa na nani atashinda mtihani?

Yani huyo Mungu wenu ni kama baba ambaye ana uwezo wa kumpa mtoto wake mchanga maziwa tu, mtoto anywe maziwa astawi.

Halafu, badala ya kumpa mtoto maziwa, anamuwekea mtoto uchaguzi, mtoto achague kati ya maziwa na sumu.

Sasa, kama baba anaweza kumpa mtoto maziwa tu, mtoto astawi, kusiwe na hatari ya mtoto kunywa sumu, kwa nini baba aone ni muhimu sana kumpa mtoto uchaguzi wa kuchagua kati ya maziwa na sumu?

Kwa nini usalama wa mtoto uwe kitu kisicho na umuhimu kama nafasi ya mtoto kuchagua (ambao hata nao tumeuona ni uongo tu hapo juu, but lets go along for the sake of argument) hususan kwa sababu mtoto mwenyewe hana hata uwezo wa kuchagua vizuri?

Huoni hili linaleta contradiction kwenye hoja ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote?
 
mkuu ETUGRUL BEY unakubali kuwa kila linalotokea ni mapenzi ya mungu au unapinga?
Mungu ndio msimamizi WA mambo yote na ndiye mpitishaji WA mambo yote

Kheri na Shari zote zinatoka kwake Kwa maana yeye ndio mwenye kupitisha hayo

Mfano,Mwenyezi Mungu akikutakia kheri hakuna mwenye uwezo wa kuizuia na akitaka Shari ikupate hakuna mwenye kuizuia,ndio maana tunasema yeye ndiye anayepitisha mambo yote

Sasa mtu Kwa mfano anataka kukuua wewe kama Mungu hajataka Hilo litokee basi hakuna litakalo kupata,na akitaka ndio iwe sababu ya kifo chako basi itakuwa hivyo

Lakini

Si kwamba Mungu amemfanya muuaji akuue wewe,Ila hayo ni maamuzi ya muuaji binafsi,je tunadhibitishaje kuwa Ni maamuzi ya mtu binafsi?

Ni kwasababu Mungu amesema tusiue nafsi isipokuwa Kwa haki,na haki ni ipi?
Ni pale Yule aliyeua Kwa makusudi basi nae anapaswa kuuwawa.
 
Wakuu mbona mnaniangusha?

Mnaelewa kwamba kwa mujibu wenu Mungu anaweza yote na angetaka watu waulizwe kama wanataka kuishi kabla ya kuzaliwa, kabla ya kuwa hai, angeweza?

Au mnataka kusema Mungu wenu muweza yote angetaka kufanya hilo angeshindwa?

Na kama angeshindwa, kweli huyo ni Mungu muweza yote?

Mjue kwamba, uongo ukipimwa kwa logic mara nyingi unaishia kwenye fallacies, inconsistencies na contradictions.

Sasa hapa nawaonesha uongo wa kuwapo kwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na anayewapa viumbe wake uwezo wa kuchagua unavyotupeleka kwenye inconsistencies, fallacies na contradictions. Ukichagua jibu lolote.

1.Ukisema Mungu katupa uchaguzi wa kuamua. Hili linatupeleka kwenye contradiction. Kwa sababu tunaona Mungu muweza yote ana uwezo wa kutupa uchaguzi tuamue tuzaliwe au tusizaliwe, lakini hakutupa uamuzi huo.

Hoja ya kwamba hakuweza kutupa uamuzi huo kwa sababu hatukuwa tumezaliwa ni hoja dhaifu. Ni hoja ya mtu anayeangalia ulimwengu huu tu kama ulimwengu unaowezekana. Ni hoja ya mtu anayempunja Mungu muweza yote nguvu zake za kuweza kumpa mtu uchaguzi wa kuamua kama anataka kuzaliwa kabla hata huyo mtu hajazaliwa.

Kama mnaamini Mungu anaweza kuhukumu watu baada ya watu kufa, kwa nini mnaona tabu kukubali kwamba Mungu huyu huyu angeweza kuwapa watu uamuzi wa kukubali au kukataa kuzaliwa kabla hawajazaliwa?

Mnaelewa kwamba mkikataa Mungu kuwa na uwezo huu wa kumpa mtu uwezo wa kuchagua kama anataka kuishi mmekataa kuwepo kwa Mungu mwenye uwezo wote na mmeanza kujiunga nami?

2. Ukisema Mungu ana upendo wote, tunarudi kwenye contradiction. Kama Mungu ana upendo wote kweli, kwa nini hakuwapa watu namna ya kufanya uchaguzi kama wanataka au hawataki kuzaliwa?

3. Ukisema watu wana uhuru wa kuchagua wanavyotaka kuishi, kuchagua mema na mabaya, tunarudi kwenye contradiction, watu wanakuwaje na uhuru wa kuishi watakavyo ikiwa hata suala la kuamua kuzaliwa au kutozaliwa hawana uamuzi nalo?

Contradictions all over.

Kwa nini?

Kwa sababu huyo Mungu hayupo. Ni character wa kutungwa na watu tu. Ni Mungu wa hadithi ya uongo.
Mkuu nawe ukisema kuwa Mungu hayupo huo ni uongo,kwasababu Mungu yupo ila mnajitoa ufahamu Tu

Ni kweli kabisa kama Mungu angetaka watu waulizwe kabla hawajazaliwa angefanya hivyo kwakuwa yeye ndio muweza wa yote na akitaka Jambo lolote litokee anasema "kuwa na linakuwa"

Lakini hakupenda kufanya hivyo kutokana sababu anazo zijua mwenyewe,na kutoruhusu hivyo hakumafanyi yeye asiwe Mungu

Binafsi ni sababu zangu ambazo naona kwanini isingekuwa Busara kuchagua tuzaliwe wapi na Nani na mambo kama hayo

# Kwanza hapa duniani tunaishi Kwa kutegemeana,kuna baadhi ya rasilimali Fulani zinapatika sehemu Fulani na nyingine sehemu Fulani,mfano kama wote tungechagua kuishi ulaya basi tungekosa mafuta ambayo yanapatikana Kwa wingi uarabuni,huo ni mfano mmoja Tu,na list inaweza endelea

# kama wote tungechagua kuzaliwa na watu matajiri basi kusingekuwa na mtu WA kumfanyia kazi mwenzake

# huenda kusingekuwa na kizazi kwasababu huenda wote watu wengi wangechagua kuwa wanaume au na kinyume chake

# huenda hata wengine Leo hii tusingekuwa binadamu tungechagua kuwa ndege au samaki na listi inaendelea

Naamini hekima ya Mungu ni kubwa zaidi katu hatuwezi kuijua
 
Nilikuwa na mzee mja wa kiislamu alinifundisha namna ya kuyatengeneza na kuyafuga
 
Unalazimisha Mungu yupo, hujaweza kuthibitisha yupo.

Mimi nimeweza kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote nanupendo wote hayupo. Kwa "proof by contradiction" ambazo mpaka sasa hujazipangua.

Ukishaanza kutoa sababu ya "Mungu kafanya hivyo kwa sababu anazozijua yeye" ushakubali kwamba unatetea uwepo wa Mungu ambaye hata wewe mwenyewe humuelewi.

Na mimi nakuambia humuelewi kwa sababu hayupo. Ndiyo maana huwezi kumuelewa.

Hastag zako zote zinaonesha hata wewe huamini Mungu anayeweza yote yupo. Kwa sababu, ungeamini hilo, usingeona hayo mapungamizi yote ni mapingamizi yanayoweza kumshinda Mungu muweza yote.

Nakwambia kwa nini Mungu hajawapa watu uchaguzi wa kuamua watazaliwa au hawatazaliwa?

Unapinga hoja kwa kusema kwamba Mungu atawapaje uchaguzi wa kuzaliwa au kutozaliwa watu ambai hawajazaliwa bado?

Hapo umekubali kwamba Mungu wako si muweza yote, ungeamini Mungu huyo ni muweza yote usingetoa pingamizi hilo.

Kifupi unakubaliana nami kwamba Mungu muweza yote hayupo.

Bila ya wewe mwenyewe kujua.
 
Unashindwa zoezi la kufikiri kwa fikra tunduizi na fikra dhahania.

Yani, fikra zako zinaishia kwenye ulimwengu uliopo.

Umeshindwa kujirudisha nyuma, wakati Mungu anataka kuumba ulumwengu.

Kabla ya kingine chochote kuwapo.

Kwa nini Mungu aliamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?

Kwa nini Mungu aone ni muhimu sana kuwapa watu mtihani wa kuchagua mabaya na mazuri, wakati angeweza kuwapa mazuri tu? Hususan kwa sababu kuna watu wengi sana watashundwa huo mtihani, na yeye Mungu ndiye anagawa neema ya nani atashindwa na nani atashinda mtihani?

Yani huyo Mungu wenu ni kama baba ambaye ana uwezo wa kumpa mtoto wake mchanga maziwa tu, mtoto anywe maziwa astawi.

Halafu, badala ya kumpa mtoto maziwa, anamuwekea mtoto uchaguzi, mtoto achague kati ya maziwa na sumu.

Sasa, kama baba anaweza kumpa mtoto maziwa tu, mtoto astawi, kusiwe na hatari ya mtoto kunywa sumu, kwa nini baba aone ni muhimu sana kumpa mtoto uchaguzi wa kuchagua kati ya maziwa na sumu?

Kwa nini usalama wa mtoto uwe kitu kisicho na umuhimu kama nafasi ya mtoto kuchagua (ambao hata nao tumeuona ni uongo tu hapo juu, but lets go along for the sake of argument) hususan kwa sababu mtoto mwenyewe hana hata uwezo wa kuchagua vizuri?

Huoni hili linaleta contradiction kwenye hoja ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote?

Mkuu Mungu asingeshindwa kutufanya tufanye mambo mazuri Tu au kutuweka katika ulimwengu ambao ni mzuri,Ila kila Jambo analofanya Lina hekima yake

Mfano aliwaruhusu Adam na Hawa kuishi peponi lakini kwa makosa Yao aliamua kuwatimua na kuwaleta hapa duniani

Na akaamua this time no free lunch! Maana Adam na Hawa walipewa nafasi na wakamuasi Mola wao

Kwahiyo hajatupa mtihani kabla Kwanza haja tufundisha ipi ni njia sahihi ya kufuata,ametupa miundo mbinu yote ya kufikia peponi Ila tushindwe Sisi Tu

Hoja ya kusema sijui wengi watashindwa Hilo sio tatizo la Mungu,Bali ni tatizo letu Sisi binadamu,kwanini wengine waweze na wengine washindwe?

Na kusema kwamba ndio anayewapa neema ya wengine kushinda na wengine kushindwa si sahihi (uongo) kwasababu kama angefanya hivyo asingetenda haki kwani yeye yeye ndio haki na kwake inatoka haki.
 
Hapana mk
Unalazimisha Mungu yupo, hujaweza kuthibitisha yupo.

Mimi nimeweza kuthibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote nanupendo wote hayupo. Kwa "proof by contradiction" ambazo mpaka sasa hujazipangua.

Ukishaanza kutoa sababu ya "Mungu kafanya hivyo kwa sababu anazozijua yeye" ushakubali kwamba unatetea uwepo wa Mungu ambaye hata wewe mwenyewe humuelewi.

Na mimi nakuambia humuelewi kwa sababu hayupo. Ndiyo maana huwezi kumuelewa.

Hastag zako zote zinaonesha hata wewe huamini Mungu anayeweza yote yupo. Kwa sababu, ungeamini hilo, usingeona hayo mapungamizi yote ni mapingamizi yanayoweza kumshinda Mungu muweza yote.

Nakwambia kwa nini Mungu hajawapa watu uchaguzi wa kuamua watazaliwa au hawatazaliwa?

Unapinga hoja kwa kusema kwamba Mungu atawapaje uchaguzi wa kuzaliwa au kutozaliwa watu ambai hawajazaliwa bado?

Hapo umekubali kwamba Mungu wako si muweza yote, ungeamini Mungu huyo ni muweza yote usingetoa pingamizi hilo.

Kifupi unakubaliana nami kwamba Mungu muweza yote hayupo.

Bila ya wewe mwenyewe kujua.
Hapana natoa maelezo ili upate point yangu mkuu

Mungu yupo na anajidhihirisha hata katika uumbaji wake pia

Ebu tumuangalie mwanadamu jinsi alivyoumbwa,kama evolution ndio imepelekea mwanadamu kutoke basi huenda angekuwa na ukuuaji WA ajabu Sana,huenda angekuwa na miguu mirefu Sana kuliko kiwiliwili chake na hivyo kukosa balance au angeendelea kukua mpaka asiweze kujimudu,ukuaji wake wa kiasi unaonyesha kuna designer ambaye amefanya yote hayo

Angalia nidhamu mbali mbali hapa duniani katika mambo ambayo ameyaumba Mungu hakika utaona kabisa kuna fundi mahiri kabisa

Mfano angalia uwiano WA jua na dunia unasapoti Maisha ya binadamu,kama jua lingekuwa limejitokea Tu Kwa bahati mbaya huenda lingekuwa mbali na dunia na kuifanya dunia iwe na baridi Kali kiasi kwamba binadamu asiweza kuishi,na lingekuwa karibu Sana basi pangekuwa na joto kubwa kiasi kwamba binadamu asingeweza kuishi

Angalia nidhamu ya usiku na mchana,tangu tumepata akili hata siku moja hatujawahi ona kunakuwa usiku Tu au mchana Tu,Bali kumekuwa na nidhamu tangu ilipoumbwa dunia mpaka siku ya hukumu

Angali mpangilio WA galaxy huko katika space hakika utaona hakika kuna Muumba WA kila kitu na list inaweza endelea

Yote hayo yanaonyesha hakika hakuna jambo lililotokea Kwa bahati mbaya Bali limetokea Kwa mpango maalum na kusudio maalum

Hakika ni uongo mkubwa kusema hakuna Mungu
 
Kama Mungu kashaona wewe utaenda motoni, kabla hujazaliwa, hapo huna nafasi ya kuukwepa moto, kqbla hujazaliwa your fate is sealed.
Is note sealed mkuu

Huenda hukunielewa,ukisema IPO sealed unamaanisha Mungu ndio amekufanya au amesababisha wewe uingie Motoni laa hasha!

Yeye ni mjuzi WA mambo ya ghaibu (mambo yajayo) ndio maana anajua kinachofuata ni nini?

Ni kama wewe unavyojua hiyo gari yako IPO siku itachoka na haitafaa tena Kwa matumizi,je kwakujua Hilo ndio inamaanisha wewe ndio utaliharibu na kulifanya lisifae Kwa matumizi?
 
Hapana mk
Hapana natoa maelezo ili upate point yangu mkuu

Mungu yupo na anajidhihirisha hata katika uumbaji wake pia

Ebu tumuangalie mwanadamu jinsi alivyoumbwa,kama evolution ndio imepelekea mwanadamu kutoke basi huenda angekuwa na ukuuaji WA ajabu Sana,huenda angekuwa na miguu mirefu Sana kuliko kiwiliwili chake na hivyo kukosa balance au angeendelea kukua mpaka asiweze kujimudu,ukuaji wake wa kiasi unaonyesha kuna designer ambaye amefanya yote hayo

Angalia nidhamu mbali mbali hapa duniani katika mambo ambayo ameyaumba Mungu hakika utaona kabisa kuna fundi mahiri kabisa

Mfano angalia uwiano WA jua na dunia unasapoti Maisha ya binadamu,kama jua lingekuwa limejitokea Tu Kwa bahati mbaya huenda lingekuwa mbali na dunia na kuifanya dunia iwe na baridi Kali kiasi kwamba binadamu asiweza kuishi,na lingekuwa karibu Sana basi pangekuwa na joto kubwa kiasi kwamba binadamu asingeweza kuishi

Angalia nidhamu ya usiku na mchana,tangu tumepata akili hata siku moja hatujawahi ona kunakuwa usiku Tu au mchana Tu,Bali kumekuwa na nidhamu tangu ilipoumbwa dunia mpaka siku ya hukumu

Angali mpangilio WA galaxy huko katika space hakika utaona hakika kuna Muumba WA kila kitu na list inaweza endelea

Yote hayo yanaonyesha hakika hakuna jambo lililotokea Kwa bahati mbaya Bali limetokea Kwa mpango maalum na kusudio maalum

Hakika ni uongo mkubwa kusema hakuna Mungu
Unasema Mungu anajidhihirisha katika uumbaji wake.

Ukibanwa uelezee kwa nini Mungu kafanya hivi, jambo linalo contradict upendo wake, na si vile, jambo linaloendana na yeye kuwa na upendo, unakosa jibu.

Unadai Mungu anafanya anavyotaka mwenyewe.

Hapo hujajibu swali, umekubali hujui jibu la swali.

Wewe kutomjua tu huyo Mungu wako inaonesha si Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote. Angekuwepo, asingekuwa mkatili hivi kukunyima kumfahamu.

Hoja zako zote za nidhamu na hashtag ni "logical non sequitur". Zimeelezewa vizuri kisayansi bila kuhitaji nadharia ya Mungu.

Kwa mfano, hatuhitaji hoja ya Mungu kuelezea usiku na mchana. Tunahitaji kujua dunia inavyojizungusha katika mhimili wake tu.

Ukimuingiza Mungu katika hili naona tatizo la elimu ndogo ya sayansi na kupenda kulazimisha habari za Mungu.

Zaidi, ukileta hoja hii ya kwamba kila kilicho complex kinahitaji muumba, kimsingi unakubali kwamba Mungu hayupo.

Kwa sababu, na mimi nitakuuliza Mungu naye kasababishwa na nini? Utahitaji kumuelezea muumbaji wa Mungu, na muumbaji wa muumbaji wa Mungu, ad infinitum, ad nauseam, ad absurdum.

Na ukishahitaji kuwa na muumbaji wa Mungu tu, huyi Mungu si Mungu muweza yote.

Kwa mara nyingine tena unakubaliana nami kwamba Mungu muweza yote hawezekani kuwapo. Bila ya kujua kwamba unakubaliana nami.

Inaonekana hata wewe mwenyewe huelewi kwa kina kirefu ukweli kwamba hoja unazozitoa si za kutetea uwepo wa Mungu. Ukiziangalia kijuuju utafikiri zinatetea uwepo wa Mungu. Lakini, ukiziangalia kwa kina, zimejikita katika kupinga uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote

Ni hivi, hapa kuna mawili.

Ama
1. Vitu vyenye order na vilivyo complex ni lazima viwe na muumbaji.

Au

2. Vitu vyenye order na vilivyo complex havihitaji kuwa na muumbaji.

Kama 1 ni kweli. Mungu muweza yote hawezi kuwapo. Kwa sababu kila anayesemwa kuwa Mungu atahitaji kuwa na muumbaji wake, na akishakuwa na muumbaji waje, huyo si Mungu muweza yote.

Kwa hivyo, kwa kufuata mantiki hii, Mungu muweza yote hayupi.

Tukigeukia 2. Kama vitu vyenye order nq complexity havihitaji muumbaji, Mungu hahitajiki kama muumbaji ili tuelezee ulimwengu umetoka wapi.

Either way, Mungu hayupo au hahitajiki.

Ila, naweka shaka sana kama utaweza kuelewa hoja zangu.

Kwa sababu hoja zako zinaonesha ulivyo shindwa kufanya fikra dhahania (abstract thinking).
 
Back
Top Bottom