Hapana mk
Hapana natoa maelezo ili upate point yangu mkuu
Mungu yupo na anajidhihirisha hata katika uumbaji wake pia
Ebu tumuangalie mwanadamu jinsi alivyoumbwa,kama evolution ndio imepelekea mwanadamu kutoke basi huenda angekuwa na ukuuaji WA ajabu Sana,huenda angekuwa na miguu mirefu Sana kuliko kiwiliwili chake na hivyo kukosa balance au angeendelea kukua mpaka asiweze kujimudu,ukuaji wake wa kiasi unaonyesha kuna designer ambaye amefanya yote hayo
Angalia nidhamu mbali mbali hapa duniani katika mambo ambayo ameyaumba Mungu hakika utaona kabisa kuna fundi mahiri kabisa
Mfano angalia uwiano WA jua na dunia unasapoti Maisha ya binadamu,kama jua lingekuwa limejitokea Tu Kwa bahati mbaya huenda lingekuwa mbali na dunia na kuifanya dunia iwe na baridi Kali kiasi kwamba binadamu asiweza kuishi,na lingekuwa karibu Sana basi pangekuwa na joto kubwa kiasi kwamba binadamu asingeweza kuishi
Angalia nidhamu ya usiku na mchana,tangu tumepata akili hata siku moja hatujawahi ona kunakuwa usiku Tu au mchana Tu,Bali kumekuwa na nidhamu tangu ilipoumbwa dunia mpaka siku ya hukumu
Angali mpangilio WA galaxy huko katika space hakika utaona hakika kuna Muumba WA kila kitu na list inaweza endelea
Yote hayo yanaonyesha hakika hakuna jambo lililotokea Kwa bahati mbaya Bali limetokea Kwa mpango maalum na kusudio maalum
Hakika ni uongo mkubwa kusema hakuna Mungu
Unasema Mungu anajidhihirisha katika uumbaji wake.
Ukibanwa uelezee kwa nini Mungu kafanya hivi, jambo linalo contradict upendo wake, na si vile, jambo linaloendana na yeye kuwa na upendo, unakosa jibu.
Unadai Mungu anafanya anavyotaka mwenyewe.
Hapo hujajibu swali, umekubali hujui jibu la swali.
Wewe kutomjua tu huyo Mungu wako inaonesha si Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote. Angekuwepo, asingekuwa mkatili hivi kukunyima kumfahamu.
Hoja zako zote za nidhamu na hashtag ni "logical non sequitur". Zimeelezewa vizuri kisayansi bila kuhitaji nadharia ya Mungu.
Kwa mfano, hatuhitaji hoja ya Mungu kuelezea usiku na mchana. Tunahitaji kujua dunia inavyojizungusha katika mhimili wake tu.
Ukimuingiza Mungu katika hili naona tatizo la elimu ndogo ya sayansi na kupenda kulazimisha habari za Mungu.
Zaidi, ukileta hoja hii ya kwamba kila kilicho complex kinahitaji muumba, kimsingi unakubali kwamba Mungu hayupo.
Kwa sababu, na mimi nitakuuliza Mungu naye kasababishwa na nini? Utahitaji kumuelezea muumbaji wa Mungu, na muumbaji wa muumbaji wa Mungu, ad infinitum, ad nauseam, ad absurdum.
Na ukishahitaji kuwa na muumbaji wa Mungu tu, huyi Mungu si Mungu muweza yote.
Kwa mara nyingine tena unakubaliana nami kwamba Mungu muweza yote hawezekani kuwapo. Bila ya kujua kwamba unakubaliana nami.
Inaonekana hata wewe mwenyewe huelewi kwa kina kirefu ukweli kwamba hoja unazozitoa si za kutetea uwepo wa Mungu. Ukiziangalia kijuuju utafikiri zinatetea uwepo wa Mungu. Lakini, ukiziangalia kwa kina, zimejikita katika kupinga uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote
Ni hivi, hapa kuna mawili.
Ama
1. Vitu vyenye order na vilivyo complex ni lazima viwe na muumbaji.
Au
2. Vitu vyenye order na vilivyo complex havihitaji kuwa na muumbaji.
Kama 1 ni kweli. Mungu muweza yote hawezi kuwapo. Kwa sababu kila anayesemwa kuwa Mungu atahitaji kuwa na muumbaji wake, na akishakuwa na muumbaji waje, huyo si Mungu muweza yote.
Kwa hivyo, kwa kufuata mantiki hii, Mungu muweza yote hayupi.
Tukigeukia 2. Kama vitu vyenye order nq complexity havihitaji muumbaji, Mungu hahitajiki kama muumbaji ili tuelezee ulimwengu umetoka wapi.
Either way, Mungu hayupo au hahitajiki.
Ila, naweka shaka sana kama utaweza kuelewa hoja zangu.
Kwa sababu hoja zako zinaonesha ulivyo shindwa kufanya fikra dhahania (abstract thinking).