Ukishakubali kwamba Mungu hana mwanzo wala mwisho, umeshalibatilisha swali la kuuliza injinia kwa yeyote, kwa sababu ushaonesha kwamba inawezekana kilicho complex kikawepo bila ya injinia wake kuhitajika au kukiumba.
Ukikubali Mungu hana mwanzo wala mwisho, halafu ukauliza injinia wa mtu ni nani, umefanya kitu Waingereza wanakiita "You want to eat your cake and still have it". Unataka kuila keki yako uimalize, halafu keki ibakie kuwapo kwenye kisahani chako.
Kwa upande mmoja unakubali kilicho complex si lazima kiwe na muumbaji wala na mwanzo, kwa kusema Mungu hana muumbaji wala mwanzo, halafu kwa upande mwingine unakanusha hilohilo kwa kuhoji mtu kaumbwaje na mwanzo wake ni nini?
This is a contradiction. Chagua upande mmoja. Je, kilicho complex ni lazima kiwe na mwanzo na muumbaji? Au si lazima?
Kama ni lazima kilicho complex kiwe na mwanzo au muumbaji, basi, Mungu hayupo, kwa sababu na yeye atahitaji muumbaji, na akihitaji muumbaji, basi huyo si Mungu.
Kama si lazima kilicho complex kiwe na mwanzo au muumbaji, basi Mungu hahitajiki kama chanzo cha kitu chochote kilicho complex.
Jibu lolote utakalolitoa linatuonesha udhaifu wa hoja ya kuwepo Mungu huyo.
Kwenye swali lako la vitu tusivyoviona lakini vipo, mimi sijawahi kukanusha uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani. Nakupa kazi ya kutafuta nilipokanusha uwepo wa Mungu kwa sababu haonekani, hutapata hilo.
Mambo mengi hayaonekani, lakini yapo. Jicho la mtu halioni the electromagnetic spectrum yote, hatuoni heat waves, hatuoni radio waves, hatuoni microwaves, hatuoni ultraviolet waves, tunaona sehemu ndogo tu ya electromagnetic waves, visibke light.
Je, hilo linamaanisha hizo waves zote tusizoziina hazipo? Zipo.
Nimegundua watu wengi wanashindwa kujadiliana kidhahania hapa, kwa sababu hawaelewi hata hoja zangu ni zipi.
Sikatai Mungu yupo kwa sababu haonekani.
Nakataa uwepo wa Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na upendo wote, kwa sababu uwepo wake ukiulinganisha na uwepo wa dunia hii inayoruhusu mabaya mengi sana kwa vinavyoitwa viumbe wake unatengeneza logical inconsistency, unatengeneza contradiction.
Uwepo wa Mungu huyo ni sawasawa na uwepo wa pembetatu ambayo hapohapo ni duara katika Euclidean geometry. Au uwepo binti mwenye miezi 6 leo, ambaye ni mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, au kuambiwa kwamba 10 ni square root ya 2.
Haya mambo yote matatu niliyoyataja hapo juu naweza kuyakanusha na kusema si kweli.
Si kwa sababu siwezi kuona pembetatu ambayo hapohapo ni duara, si kwa sababu siwezi kumuona binti mchanga wa miezi sita leo ambaye ni mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, si kwa sababu siwezi kuiona 10 ambayo ni square root ya 2, bali kwa sababu haya mambo yote yana logical inconsistency inayo contradict mantiki muhimu.
Suala la kuona si muhimu katika kuthibitisha uwepo wa kitu.
Kwa sababu.
1. Unaweza kuona kitu ambacho hakipo. Ukiwa barabarani jangwani au sehemu yenye joto, unaweza kuona maji kwa mbali, wakati hakuna maji. Ni mirage tu.
2. Unaweza ukashindwa kuona kitu ambacho kipo. Nimetoa mfano wa electromagnetic waves zilizo tofauti na visible light hapo juu.
3. Unaweza kuona kitu ambacho kipo. Mifano ni mingi hapa.
4. Unaweza kushindwa kuona kitu ambacho hakipo. Mfano pembetatu ambayo hapohapo ni duara katika Euclidean geometry.
Sasa, katika ulimwengu ambao hayo manne yanawezekana, kwa nini kitu kuonekana au kutoonekana kuwe ni muhimu katika uthibitisho kwamba kipo?
Kwa nini tunashindwa kuongelea uwepo au kutokuwepo Mungu katika ngazi ya kidhahania na kimantiki kwa hoja tunduizi, bila kushikilia hoja dhaifu kama ya kitu kuonekana au kutoonekana, ambayo mimi hata sijaitaja?