Kama israel wasingefanya uzembe wa kumuua Sinwar, ilikua bonge moja la asset na ingebadilisha uelekeo wa vita hii.
Wangejaribu at least kumzoom vizuri wangemkamata akiwa hai(wao wakaona wapige 💣)kisha wakamtumia Kama King katika mazungumzo(draft) na Hamas.
Wakikubaliana wanamchoma sindano ya sumu ya kuua kidogo kidogo, kisha wanamwachia.
Kichwa cha sinwan thamani yake ilikua ni sawa na mateka wooote wa israel
Isingefanikiwa Mkuu, hawa watu wanataka kuwa wafia dini "martyrs". Wanataka wafe katika mapigano wakamilishe ibada au nguzo ya kufia imani na msimamo. Kwa siyo Hamas wala Sinwar angekubali "swapping" ya mateka kisa kadakwa au kawekwa kizuizini au anateswa.
Hii ni vita ya "ideology vs existence" yaani mtu anaifia imani yake, yupo tayari kufa ili akamilishe lengo la itikadi yake.
Fuatilia Press ya Hamas kufuatia kifo cha Sinwar, hawajuti wala hawaoni kama pigo kwao, wanasema amefia vitani, amekufa anapigana, hajajitoa uhai, ametolewa uhai kwa iyo ametimiza lengo la kufia iman "Martyrs". Israel anafahamu fika kwamba hatapata mateka hao kwa vyovyote vile. Anajua kwa hakika.
NIRUDI KWENYE MADA: Myahudi hawezi kuwapa mwili wa Sinwar maana kaburi lake itafanyika "Holy place" na sehemu ya kumtukuza na kukuza ideology. US alifanya hivi kwa Osama pia kumzika baharini kuogopa kadhia kama hii.
Haman wanapigania ideology "itikadi" na wayahudi wanapigania uwepo wao yani "existence".
Waarabu hawana la kupoteza, Myahudi akiwamaliza Hamas hapo Gaza na kuigeuza majivu, watoto wa hapo Gaza watakua na wataunda Hamas nyingine na lengo litakiwa lile lile kumuondoa Myahudi juu ya uso wa dunia (Jambo ambalo haliwezekani).