Waislamu wa Tanzania, where are Black People?

Waislamu wa Tanzania, where are Black People?

Hilo lilikua kongamano la mashefa wenye pesa zao ndo maana hujaona pua ya maostadhi kasuku wanaosumbua mitaa na kelele za swalaa swalaaa
 
Uchokozi mwingine hauna mantiki yoyote, mufti wa waislamu yupo hapo, Rais wa nchi yupo hapo, tatizo liko wapi?

Hao Waarabu ndio waliotowa mpunga wao ndio wenye umuhimu na hiyo picha kutunza kwenye kumbukumbu za events zao ili tajiri anayefadhiri hizo movement aendelee kutowa mpunga zaidi.
Jengo zuri sana ila watani zangu watatandika mikeka ya kukata na shoka humooo 🙁
 
Wameshajenga shule ngapi za kusoma Watanzania wote?

Kwa karne ya sasa mgeni kutujengea nyumba ya ibada ni aibu, hakuna kitu kirahisi kama kujenga nyumba za ibada ni nguzo na kuta tuu, wenzetu walishaachana na hilo la kujengewa nyumba za ibada na wageni wanachanga wenyewe na wanafanikiwa.

Nchi yetu sio maskini mpaka kupewa msaada wa nyumba ya ibada, kwanza haina thawabu ni sawa sawa na mtu mwenye mikono miwili kuomba hela ya sadaka.

Tutumie sadaka zetu kujenga nyumba za ibada ni sio kujengewa na wageni,
Kama hujui kitu kaa kimya.
Kwanza msikiti huo sio mpya. Ulikuwepo. Umevunjwa tu kufanya maboresho.
Pili jumuiya hii ina shule ya msingi na sekondari kabla hata ya maboresho.
Hakika usilojua ni usiku wa giza.
Ninaloungana na mtoa hoja ni pale picha zina waarabu tu ikimaanisha wahusika ni wenye dhehebu la kiislamu lililo na wafuasi wa kiarabu.
 
Sasa unataka ukae kwenye picha wakati hukuwepo hata kwenye uchangiaji wa ujenzi.

Hata kwenye ndoa, si huwa wanaenda wanakamati pale[emoji1787]
Ila mmegundua watu wana chuki Sana na uislam!yaani humu tunachekewa kinafiki inshort hawatupendi asilani!!!
 
Sasa watakao kuwa wakiswali hapo ni Waoman au Wahaya? Mkuu naona haipendezi hao representative wa hilo tukio kuwa karibu 98% wageni.

Ingekuwa msikiti wa Bohora tungeelewa maana Bohora natives wapo wachache sana. Au hawapo kabisa
Kuna waswahili wamepata pa kulala na wengine wamepata mageti ya kuombea misaada
 
Ndugu zangu,
Mtu anapotaka kujadili jambo lolote nI vyema akafanya utafiti kwanza.
Hao ni viongozi wa Ibadh na asili yao ni Oman.

Mfano mzuri ni huu wa Greek Othodox Church (Hellenic).
Kanisa lao lipo Ali Hassan Mwinyi Road.

Itashangaza kuuliza kwa nini katika kanisa lao hakuna Waingereza.
Mzee Said sikuoni kwenye picha
 
Tuliaminishiwa msikiti sio kanisa kusema ni mali ya fulani. Bali wakishajenga inakua mali ya waumini wote. Ingependeza waumini wakawepo hapo
Nani kakwambia hivyo?
Hii misikiti INA wenyewe na wenyewe ni wale waliotoa viwanja ukajengwa msikiti. Kuna msikiti pale magomeni una ugomvi mkubwa sana
 
Afrika inahitaji ujenzi wa viwanda vingi na miundo mbinu imara ili kuongeza na kuboresha hali za maisha ya wananchi wake kwa sasa sio misikiti na makanisa....kwa sasa vipo vya kutosha......
.
 
Katika upuuzi wa hizi dini,muhaya muislam wa murongo border,anajiona yupo Karibu zaidi na muislam wa Zenj,kuliko ndugu yake wa hapo hapo kijijini ambaye ni mkristo
Na Mwalimu Nyerere alionya kwamba ukishaanza kula nyama ya MTU ujue hautoiacha tena !! Ubaguzi wa aina yeyote ile iwe ni ya dini au ya rangi haitoishia hapo !! Itafuatiwa na baguzi nyingine na nyingine na nyingine !! Tujiepushe na UBAGUZI UBAGUZI WA AINA YEYOTE ILE !!!
 
Ni mjinga pekee atakaye ukubali huu ujinga, kuna Uislamu na kuna uarabu. Hivi vitu huwa mnashindwa kuvitofautisha.

Mababu zako kabla ya kufikiwa na dini walikuwa wanaishi vipi ? Walikuwa na vaaje walikuwa wanapeana majina kwa kufata misingi gani ? Watu wanaitana majina Shida, Matatizo.

Embu tuambieni au tupeni ubora wa tamaduni zenu za kiafrika dhidi ya dini,mfano wa dini ya Uislamu.

Wajinga pekee wanalilia "Identity" bali wenye akili wanawaza itakuwaje baada ya kifo chao ? Wenye akili wanajiuliza kwanini wameumbwa ?

Misingi ya mababu zako ilikuwa ipi na ubora ulikuwa upi ?
Naomba unijibu hili swali?

Kabla ya kuzaliwa na kupata ufahamu hapa duniani ulikuwa wapi na ulikua unafanya nini?


#MaendeleoHayanaChama
 
Naomba unijibu hili swali?

Kabla ya kuzaliwa na kupata ufahamu hapa duniani ulikuwa wapi na ulikua unafanya nini?


#MaendeleoHayanaChama
Ujinga uliopo duniani kwa wakati huu - huko India kijana mmoja amefungua kesi Mahakamani anawashitaki wazazi wake kwanini walimzaa bila ridhaa yake !! Salaaleeh !! Huko ndiko tunakoelekea !! " The more the people becomes educated the more the world becomes Stupid " !!
 
Back
Top Bottom