Hilo somo ni kuingiza ujinga wa kudumu katika jamii, kwani linaleta maarifa gani katika kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo? Litakuwa mzigo usiokuwa na faida kwa wanafunzi, halijengi nyumba, barabara, halileti ubunifu zaidi ya kuleta ugonjwa wa akili, akili kuwa ya kizembe. Hilo somo wakafundishane wenyewe kwenye nyumba zao za ibada wakajazane ujinga huko mpaka waje washituke karne nyingi zijazo. Badala ya kupanga masomo ya maana wanapanga upuuzi kuzidi kuididimiza jamii kwenye shimo refu la umasikini, ujinga na maradhi