EvilSpirit
JF-Expert Member
- Jun 15, 2017
- 13,579
- 21,407
Itaonekana ni jambo la ajabu kuwashauri kobazi kufuga nguruwe lakini ushauri huo umetolewa na Sheikh Abubakari Mwaibabile wa msikiti wa Sabasaba katika kitongoji cha Holemela,Mbarali Mbeya.Wakati akiyasema hayo aliwasisitiza waislamu kuielewa Quran zaidi na kutokubaliana na mambo ambayo hayako katika Quran,aliendelea kufafanua kuwa Quran haijakataza kufuga nguruwe bali imekataza kula nguruwe,alisema hata yeye amekuwa akifuga nguruwe ambao wamemletea manufaa ya kiuchumi ikiwemo uwezo wa kuwalipia karo watoto shuleni,alisisitiza waislamu hawakatazwi kufuga nguruwe kwa ajili ya kujikwamua kutoka katika dimbwi la umasikini.Ushauri wangu kwa waislamu wa jf na wengineo waanze kusoma nyuzi za namna ya ufugaji bora wa nguruwe au tuseme ufugaji wenye tija,pia nashauri wawe wanatumia nyama ya nguruwe ili afya zao ziimarike wawe na nuru maana wengi wamekauka,unakuta mtu kafubaa kavaa kanzu,na kanzu yenyewe imefubaa unaweza kuzani kanzu imetundikwa kwenye mti unaotembea